Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva jana amefikisha mabao sita ya kufunga tangu amejiunga na Difaa Hassani El-Jadida (DHJ) ya Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola.
Hiyo inafuatia Msuva jana kufunga bao moja katika mechi yake nane DHJ ikifungwa 2-1 na timu ya Daraja la Kwanza, Union Sportive Musulmane Oujda (USMO) Uwanja wa El Abdi mjini Jadida.
“Jana nimefunga tena, hilo ni bao langu la sita sasa katika mechi nane zote za kirafiki. Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri na hapa kila siku ninachojua ni bidii tu ili nitimize malengo yangu,”amesema Msuva akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo.
Simon Msuva akiichezea DHJ jana na kufunga bao japo timu yake ilifungwa 2-1
Sasa Simon Msuva amefikisha mabao sita katika mechi nane za kirafiki
Kwa sasa Simon Msuva ni mchezaji wa kuchungwa sana kwenye mechi DHJ
Msuva sasa anaanza kwenye kikosi cha kwanza cha Difaa Hassan El-Jadida
Msuva alisaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na DHJ Julai 28, mwaka huu baada ya kucheza Yanga ya nyumbani, Tanzania tangu mwaka 2012 akitokea Moro United iliyokuwa tayari imehamishia maskani yake Dar es Salaam kutoka Morogoro.
Awali ya hapo, Msuva alipitia akademi ya Azam akitokea kituo cha kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi, Wakati Ujao baada ya kuibuliwa na iliyokuwa taasisi ya Pangollin ya kocha Charles Boniface Mkwasa, ambaye sasa ni Katibu wa Yanga, klabu aliyoichezea na kuifundisha awali..
Na baada ya kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mfungaji bora mara mbili – Msuva amehamia Morocco kusaka changamoto mpya na mafanikio zaidi kisoka.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2wIsrrL
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms