Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TANZANIA imeanza kuandaa kikosi kipya cha timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 - Serengeti Boys kitakachoshindana kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka hiyo.
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), limeiteua Tanzania kuandaa fainali hizo mwaka 2019 hivyo sasa TFF imeanza kuandaa vijana wake.
Kwa kuanzia tu, imeanza kuwamulika vijana 22 wanaosoma Shule za Alliance zilizoko Mwanza.
Mapema wiki hii, ilimuagiza Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu kwa Vijana, Kim Poulsen kupima uwezo wa vijana hao kwa kufanya nao mazoezi kwenye viwanja vya Alliance ambako amemaliza leo asubuhi na kusema: “Tuna timu bora ya taifa.”
“2019 si tu kwamba Tanzania itashiriki, bali kushindana. Lakini naipongeza TFF na Alliance kwa kuanza program ya kuandaa timu bora. Serengeti Boys ya sasa inayomaliza muda wake iliandaliwa kwa mwaka mkoja, lakini vijana hawa wenye umri wa miaka 12 na 13 ni hazina nyingine kubwa kwa taifa…
“Kwa jinsi nilivyowaona itoshe kusema tu tayari tuna timu. Nimesikia viongozi wa TFF wakisema kwamba jicho lao si kwa vijana hawa tu, bali pia kwa vijana wengine Tanzania nzima. Hili ni jambo zuri lenye manufaa mazuri,” amesema Poulsen alipozungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya mazoezi ya asubuhi.
Nahodha wa timu hiyo ya vijana, alishukuru Alliance kwa malezi mazuri na TFF kwa kuendelea kuwajali hasa kwa sasa ambako nao wamesema ndoto zao ni kutaka kung’ara zaidi ya Serengeti ya sasa ambao walitolewa na Congo Brazzaville katika harakati za kuwania nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika, zitakazofanyika mwakani nchini Madagascar.
Vijana waliotolewa kwa sasa wanajipanga upya kwenda Korea Kusini kwa ajili ya kujiandaa na ratiba mpya ya CAF na FIFA kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 ambako timu ya taifa kwa hapa Tanzania inaitwa Ngorongoro Heroes. Ratiba za michuano ijayo ya kimataifa, itatolewa baadaye mwaka huu.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2eaqJun
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang SERENGETI BOYS YA FAINALI ZA AFRIKA 2019 YAANZA KUANDALIWA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2016/10/serengeti-boys-ya-fainali-za-afrika.html. Terimakasih atas perhatiannya.