Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
YANGA na Azam FC zimezidi kujitoa katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kutoa sare ya 0-0 katika mchezo baina yao jioni ya leo Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yaliyopokewa kwa furaha na wapinzani wao katika mbio za ubingwa, Simba SC yanazifanya timu hizo zilizokuwa zikitawala soka ya Tanzania kwa miaka minne iliyopita ziendelee kusuasua katika Ligi Kuu.
Yanga inafikisha pointi 15 baada ya mechi nane, ikitoa sare ya tatu, baada ya kufungwa mechi moja na kushinda nne, wakati Azam FC inafikisha pointi 12 baada ya kucheza mechi tisa, ikitoa sare ya tatu baada ya kufungwa mechi tatu na kushinda tatu – wakati Simba SC yenye pointi 23 za mechi tisa kutokana na kushinda mara saba na sare mbili, inagonoza Ligi Kuu.
Wachezaji wa Yanga na Azam wakiwani mpira wa juu leo
Katika mchezo huo, timu zote zilishambuliana kwa zamu na Yanga ndiyo waliokuwa wa kwanza kulitia majaribu lango la Azam FC dakika ya kwanza tu kufutia kiungo Mzimbabwe, Thabani Kamusoko kupiga shuti kali liliookolewa na kipa Aishi Manula na kuwa kona ambayo iliokolewa pia.
Winga Muivory Coast wa Azam, Ya Thomas Gonza aliunganishia nje krosi ya Erasto Nyoni dakika ya 13 na dakika ya 16 Mzambia Obrey Chirwa alimdakisha mpira wa kichwa Manula kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Juma Abdul.
Kipa wa Yanga, Deo Munishi ‘Dida’ aliokoa shuti la kiugo wa Azam, Mudathir Yahya dakika ya 23 na kuna ambayo haikuwa na madhara.
Yanga ilipata pigo dakika ya 31 baada ya beki wake tegemeo wa kulia, Juma Abdul kuumia kufuatia kugongana na Kangwa dakika ya 27 na kushindwa kuendelea na mchezo baada ya matibabu ya takriban dakika tatu, nafasi yake ikichukuliwa na Mbuyu twite.
Nahodha wa Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ alifumua shuti kali dakika ya 41 ambalo hata hivyo liliokolewa na Dida. Yanga wakajibu dakika ya 44 kwa Chirwa kuunganisha krosi ya winga Simon Msuva, lakini Manula akaokoa.
Dida akaokoa shuti la Kangwa dakika ya 55 baada ya Azam kupandisha shambulizi zuri la haraka.
Azam ilipata pigo nayo dakika ya 78 baada ya Bocco kushindwa kuendelea na mchezo kufuatia kugongana na beki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ na nafasi yake ikachukuliwa na Mzimbabwe Francesco Zekumbawira.
Dakika mbili baadaye Dante naye akashindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia kufuatia kugongana na kiungo wa Azam, Himid Mao ‘Ninja’ na nafasi yake kuchukuliwa na Nahodha, Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Kikosi cha Azam FC kilikuwaAzam FC; Aishi Manula, Bruce Kangwa/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk87, Erasto Nyoni, Aggrey Morris, Daniel Amoah, Jean Baptiste Mugiraneza, Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco/Francesco Zekumbawira dk78 na Ya Thomas Gonazo.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Mbuyu Twite dk31, Mwinyi Hajji, Andrew Vincent/Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dk80, Kevin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Deus Kaseke/Geoffrey Mwashiuya dk57.
Wakati huo huo: Mkutano Mkuu wa dharula wa Yanga utafanyika Jumapili katika Uwanja wa Kaunda, Dar es Salaam ajenda kuu ikiwa kujadili klabu kukodishwa.
Pamoja na hayo, ajenda nyingine ni kuthibitisha Wajumbe wa Baraza ya Wadhamini na kumpumzisha Mjumbe mmoja na kuongeza mwingine, uongozi kuomba ridhaa ya kumteua Mjumbe mmoja bila ya kuitisha mkutano mkuu kupunguza gharama kwa klabu.
Kupitia na kujadill muhtasari ya makubaliano ya Barza la Wadhamini kulingana na maagizo ya wanachama kukodisha timu na nembo ya Yanga kwa kipindi cha miaka 10 na kupanga tarehe ya uchaguzi mdogo kujazia nafasi zilizo wazi na kupata mwongozo wa Katiba ya kutumia kati ya 2010 au 2014.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2dtqF6p
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang YANGA NA AZAM ZAZIDI KUJICHUJA MBIO ZA UBINGWA LIGI KUU. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2016/10/yanga-na-azam-zazidi-kujichuja-mbio-za.html. Terimakasih atas perhatiannya.