Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
YANGA SC imesema imeanza mawasiliano na Taasisi ya Kupambaa na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) ili waichunguze Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania au Kamati ya Saa 72 Ijumaa kwa madai wanataka kucheza mchezo mchafu kwa kushirikiana na klabu ya Simba.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani mjini Dar es Salaam kwamba kamati hiyo kwa kushirikiana na klabu ya Simba wanataka kufoji taarifa za michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ili kuibeba klabu hiyo.
Mkemi alisema baada ya Simba kufungwa 2-1 na Kagera Sugar Aprili 2, mwaka huu na kupoteza mwelekeo kwenye mbio za ubingwa wamehamishia nguvun zao nje ya Uwanja kuhakikisha wanatwaa ubingwa.
Salum Mkemi (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam
Amesema Simba wanadai beki wa Kagera Sugar, Mohammed Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano, wakati si kweli kwani beki huyo wa zamani wa JKT Ruvu alikuwa ana kadi mbili tu.
“Hiyo kadi nyingine wanayotaka kuchomekea, alioonyeshwa kwenye mechi ya Kombe la TFF. Siyo Ligi Kuu,”alisema.
Kwa sababu hiyo, Mkemi amesema kwamba wameanza kuwasiliana na TAKUKURU ili waingilia kati suala hilo kwa kuwachunguza Kamti ya Saa 72.
Amesema pia wamewasiliana na Kitengo cha kukabiliana na uhalifu wa mitandaoni na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kuchunguza taarifa za michezo za waamuzi na makamisaa kuhusu kadi za njano za Fakhi ili kujua zilitumwa lini.
Kwa ujumla Mkemi amesema kwamba wanataka vyombo vya dola vilifanyie kazi suala hilo kikamilifu ili mbivu na mbichi zijulikane.
Pamoja na hayo, Mkemi ameishutumu Kamati ya Saa 72 kwamba inaundwa na wajumbe wengi ambao ni wapenzi wa mahasimu wao, Simba na maamuzi yao yanaegemea ktika ushabiki.
Amewataka Wajumbe hao kuwa Ahmed Iddi Mgoyi, Baruan Muhuza, Boniphace Wambura, Jonas Kiwia, Charles Ndagala, Issaro Chacha, Stephen Mnguto na Philemon Ntahilaja ambaye ndiye pelee mwenye mapenzi na Yanga.
Simba iliwasilisha malalamiko ikitaka ipewe ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kutokana na Kagera Sugar kumchezesha Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mechi yao namba 194 iliyofanyika Aprili 2, 2017 Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kamati baada ya kupitia malalamiko hayo, imeahirisha shauri hilo hadi Alhamisi Aprili 13, 2017 kwa vile bado inafuatilia baadhi ya vielelezo kuhusu malalamiko hayo kabla ya kufanya uamuzi.
Mkemi pia akawapongeza Simba kwa ushindi wa jana wa 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba mijini Mwanza ingawa aliubeza ulitokana na ‘kulegea’ kwa wapinzami wao dakika za mwishoni.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2ppeY3C
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms