Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BAO pekee la beki Aggrey Morris limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Timu ya Manispaa ya Kinondoni, ijulikanayo kama KMC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam Ijumaa jioni.
Mchezo huo ulikuwa ni wa mwisho wa kikosi hicho kabla ya kuelekea nchini Uganda kuweka kambi ya siku 10 katika maandalizi ya mwisho mwisho kabla ya kuanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL),
Nahodha huyo Msaidizi wa Azam FC, Aggrey Morris alifunga bao hilo dakika ya 57 kwa mkwaju wa penalti kufuatia mshambuliaji mpya, Wazir Junior kuangushwa kwenye eneo la hatari.
 |
| Aggrey Morris akishangilia baada ya kufunga bao pekee dhidi ya KMC |
Azam FC iliutawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa hasa kipindi cha pili ikicheza soka safi la pasi na kasi huku ikishuhudiwa Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo, Junior, Enock Atta, Yahya Zayd, Bruce Kangwa, waking’ara vilivyo kwa kupeleka mashambulizi makali langoni mwa KMC.
Ushindi huo ulikuwa zawadi nzuri kwa kocha Mromania, Aristica Cioaba aliyekuwa anasherehekea siku ya kuzaliwa Agosti 4 na baada ya mchezo huo akaenda kukata keki na wachezaji wake.
Huo ni mchezo wa tano kwa timu hiyo ya kocha Mromania, Aristica Cioaba katika mechi za kujiandaa na msimu mpya, ikiwa imeshinda mbili, sare moja na kufungwa mbili.
Azam ilianza kwa kufungwa 4-2 na Rayon Sport mjini Kigali, Rwanda kabla ya kutoka sare ya 0-0 na Mbeya City mjini Mbeya, kufungwa 2-0 na Mji Njombe FC huko Makambako na kushinda 4-0 dhidi ya Lipuli mjini Iringa.
Mara baada ya mchezo huo, kikosi cha Azam FC kinatarajia kupumzika kwa siku moja kabla ya keshokutwa alfajiri kuanza safari ya kuelekea nchini Uganda itakapocheza mechi nne za kirafiki dhidi ya KCCA, Vipers, URA na SC Villa, zote zikiwa timu kongwe za nchini humo.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2v6J009
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms