Na Mwandishi Wetu, NAKURU
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC leo wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalti 3-2 dhidi ya Kariobangi Sharks kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
Shujaa wa Simba SC leo alikuwa ni kipa wake hodari, Aishi Salum Manula aliyeokoa penalti na sasa Wekundu hao wa Msimbazi watakutana na mshindi wa mchezo wa kesho kati ya wenyeji wengine, AFC Leopards dhidi ya Singida United kwenye Nusu Fainali.
Simba SC pia imeifutia aibu Tanzania baada ya jana Yanga SC na JKU ya Zanzibar kutolewa na timu za Kenya katika hatua ya kwanza tu ya michuano hiyo.
Wachezaji wa Simba SC, Moses Kitandu (kulai) na Shiza Kichuya (katikati) wakimpongeza mwenzao, kipa Aishi ManuIa aliyeokoa penalti
lianza Yanga SC kuchapwa 3-1 na Kakamega Homeboyz hapo hapo Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Allan Watende Wanga akifunga mabao mawili dakika za 26 na 30 na linguine la Kakamega Homeboyz likifungwa Wycliffe Opondo dakika ya 85, huku la timu ya Jangwani mjini Dar es Salaam likifungwa na Matheo Anthony dakika ya 38.
JKU nayo ikafuatia baada ya kuchapwa 3-0 na mabingwa watetezi, Gor Mahia mabao ya George Odhiambo, Godfrey Walusimbi na Meddie Kagere na sasa wanapanda ndege moja na ndugu zao, Yanga SC kurejea Dar es Salaam kila timu ikipatiwa kifuta jasho cha dola za Kimarekani 2,500 kiasi cha Sh. Milioni 6.
Kakamega Homeboys sasa watakutana na Gor Mahia katika Nusu Fainali Juni 7, na Nusu Fainali ya pili itaikutanisha Simba SC na washindi wa mechi za kesho.
Na fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup 2018 itafanyika Juni 10 na mshindi pamoja na kupata dola za Kimarekani 30,000 pia atapata nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England.
Mshindi wa pili atajipatia dola za Kimarekani 10,000, wa tatu dola 7, 500 na wa nne dola 5,000 wakati timu nyingine zitapewa kifuta jasho cha dola 2,500.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2Jh8H4C
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms