KOCHA mpya wa Yanga SC, Muargentina Miguel Angel Gamondi ameahidi mchezo wa kuvutia kesho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo kwenye mkutano na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Gamondi amesema kwamba watajaribu kucheza vizuri ili kuwapa furaha mashabiki.
"Tunatarajia kuwa na malengo makubwa zaidi kwa sababu hii ni klabu kubwa yenye mashabiki wengi wenye nguvu na ushawishi kutaka klabu hii iendelee kufanya vizuri zaidi hasa kwenye mashindano ya kimataifa," amesema Gamondi.
Gamondi kwa upande wa timu bado wapo kwenye maandalizi na mchezo wa kesho dhidi ya Kaizer Chiefs watautumia kama sehemu ya maandalizi yao kuelekea msimu mpya.
"Kesho ni siku kubwa kwa mashabiki wa Yanga pamoja na sisi wote tunakwenda kupata nafasi ya kusherehekea kufunguliwa kwa msimu huu mpya tukiwa na matarajio ya kuendelea kuipambania klabu hii kubwa yenye historia kubwa,"ameongeza Gamondi.
Kwa upande wake winga mpya wa timu hiyo aliyesajiliwa kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Skudu Mahlatse Makudubela amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi Uwanja wa Mkapa kwani watawapa burudani nzuri.
"Tupo kwenye maandalizi ya awali kujiandaa na msimu mpya, kwa niaba ya wachezaji wenzangu kwanza niseme ni heshima kubwa sana kwangu kuwawakilisha kwenye mkutano huu na ujumbe wetu kwenu tunaomba kesho mje kwa wingi tumewaandalia burudani nzuri,"amesema Mahlatse.
Kilele cha Wiki ya Mwananchi ni siku maalum ambayo Yanga hutumia kutambulisha kikosi chake kizima cha msimu pamoja na benchi la Ufundi kabla ya mchezo maalum wa kirafiki, ambayo yote hutanguliwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/u8XloQT
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms