TIMU ya taifa ya Angola jana imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu Hatua ya Mtoano Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mauritania katika mchezo wa Kundi D Uwanja wa La Paix mjini Bouaké, Ivory Coast.
Mabao ya Angola yalifungwa na washambuliaji Gelson Dala wa Al Wakrah ya Qatar mawili dakika ya 30 na 50 na Deivi Miguel Vieira 'Gilberto' wa Petro de Luanda ya kwao dakika ya 53, wakati ya Mauritania yalifungwa na washambuliaji pia, Sidi Amar wa Nouadhibou ya kwao na Aboubakary Koita wa Sint-Truiden ya Ubelgiji.
Mechi nyingine ya Kundi D jana, Algeria ilitoka sare ya 2-2 Burkina Faso hapo hapo Uwanja wa La Paix mjini Bouaké.
Mabao ya Burkina Faso yalfungwa na washambuliaji Mohamed Konaté wa Akhmat Grozny ya Urusi dakika ya 45 na Bertrand Traoré wa Aston Villa dakika ya 71 kwa penalti, wakati ya Algeria yalifungwa na mshambuliaji wa Al Sadd ya Qatar,Baghdad Bounedjah yote dakika ya 51 na 90 na ushei.
Kwa matokeo hayo, Angola na Burkina Faso zinafikisha pointi nne zikiongoza Kundi D mbele ya Algeria yenye pointi mbili na Mauritania haina pointi na itakamilisha mechi zake kwa kumenyana na Algeria.
Mechi ya Kundi E jana Tunisia ilitoa sare ya 1-1 na Mali Uwanja wa Amadou Gon Coulibaly mjini Korhogo. Mshambuliaji wa Auxerre ya Ufaransa, Lassine Sinayoko alianza kuifungia Mali dakika ya 10, kabla ya kiungo wa Lecce ya Italia, Hamza Rafia kuisawazishia Tunisia dakika ya 20.
Mali inaendelea kuongoza Kundi E kwa pointi zake nne, ikifuatiwa Namibia pointi tatu, Tunisia yenye pointi moja, wakati Afrika Kusini haina pointi mkiani.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/1qaeCFX
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms