MWENYEKITI wa Chama cha Marefa wa Soka Tanzania (FRAT), Omar Abdulkadir Isasc usiku wa kuamkia kwenye hospital ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Abdukadir ambaye ni refa wa zamani wa Kimataifa nchini aliyefanya kazi kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, amefariki dunia baada ya kusumbuliwa na maradhi ya kisukari kwa muda.
Msiba upo nyumbani kwake, Mtoni kwa Aziz Ally na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Moja kati ya mechi za kukumbukwa alichezesha Abdulkadir ni Fainali ya Kombe la Tusker baina ya watani wa jadi, Machi 31, mwaka 2002 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru Jijini Dar es Salaam ambayo Simba iliichapa Yanga 4-1.
Mabao ya Simba sik hiyo yalifungwa na winga Mkenya, Mark Sirengo mawili, dakika ya tatu na 76 na washambuliaji wazawa, Madaraka Selemani dakika ya 32 na Emanuel Gabriel dakika ya 83, wakati la Yanga lilifungwa na Sekilojo Chambua dk 16.
Lakini mechi hiyoiliyohudhuriwa na rais mstaafu, marehemu Ali Hassan Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa.
Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Abdulkadir alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) ndipo akaendeleza mchezo.
Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo na baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa Shirikisho, TFF.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/QuSEyrx
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms