Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya soka ya taifa vijana chini ya umri wa chini ya miaka 14, leo Desemba 4, 2016 inaanza kambi rasmi katika Hosteli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Vijana hao 22, wanaingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli unaotarajiwa kufanyika Desemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ambao una baraka za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), umepangwa kufuata taratibu zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na kupigiwa Nyimbo za Taifa kwa timu zote sambamba na kupandisha Bendera za Mataifa husika.
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu wa timu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 14, Oscar Mirambo anayepata ushauri kutoka kwa Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana, Kim Poulsen kinatarajiwa kuwa na michezo minne ya kirafiki ya nyumbani kabla ya kucheza na Shelisheli.
Michezo hiyo ya kirafiki ni dhidi ya Moro Kids ya Morogoro Desemba 8, 2016 saa 10.00 jioni kabla ya mchezo wa marudiano Desemba 9, mwaka huu saa 3.00 asubuhi kwenye Uwanja wa Jamhuri na baadaye timu hiyo itarejea Dar es Salaam mchana kujiandaa na safari ya Zanzibar Desemba 11 ambako itakuwa na michezo miwili mingine ya kirafiki.
Zanzibar itacheza na Kombaini ya timu ya Vijana wa Zanzibar Desemba 12, 2016 kabla ya kurudiana Desemba 14, mwaka huu na timu hiyo na Kombaini kabla ya kurejea Bara Desemba 15, kujiandaa na mchezo kirafiki wa kimataifa dhidi ya Shelisheli.
Kikosi kamili cha timu hiyo makipa ni Shaban Hassan Kimwaga na Abdulatif Noor Lema wakati walinzi ni Kareem Bakari Mfaume, Asante Hamis Bwatam, Rashid Hamisi Rashid, Moris Michael Njako, Harubu Juma Tanu, Cosmas Lucas Jakomanya, Salim Abubakar Lupepo na Dastan Daniel Matheo.
Viungo ni Edson Jeremiah Mshirakandi, Jonathan Raphael Kombo, Alphonce Mabula Msanga, Erick Boniface Bunyaga, Gssper Godfrey Gombanila, Sabri Dahari Kondo na washambuliaji ni Jafari Juma Rashid, Ludaki Juma Chasambi, Steven Emmanuel Sodike, Michael Mussa Mpubusa na Edmund Geofray John.
Timu hii inaundwa na vijana ambao TFF iliwakusanya tangu 2014 na kuwaunganisha kwa pamoja katika Shule ya Msingi na Sekondari ya Kukuza Vipaji ya Alliance iliyoko Mwanza. Mbali ya kutoa elimu ya msingi na sekondari, pia Alliance inatoa elimu ya awali kwa watoto wa kuanzia umri wa miaka miwili hadi sita.
Timu hii inaandaliwa kuja kwa time mpya ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ambao watashiriki fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana mwaka 2019 ambako Tanzania imeteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa mwenyeji. Kambi itavunjwa Desemba 18, mwaka huu.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2gohYsS
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang U-14 YAINGIA KAMBINI LEO KUJIANDAA NA SHELISHELI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2016/12/u-14-yaingia-kambini-leo-kujiandaa-na.html. Terimakasih atas perhatiannya.