Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
KIPA Muivory Coast wa Simba SC, Vincent Paul Angban anatarajiwa kuondoka nchini leo kurejea kwao, baada ya kumalizana na klabu ya Simba.
Akizungumza na Bin Zubeiry Sports - Online jana, Angban alisema kwamba baada ya kumalizana na Simba SC ataondoka Jumapili kurejea kwao.
“Natarajia kuondoka Jumapili baada ya kukutana na uongozi wa Simba na kukamilishiana malipo. Nawashukuru wapenzi wote wa Simba kwa sapoti yao kwangu kipindi chote, maisha yanaendelea,”alisema.
Vincent Angban anatarajiwa kuondoka nchini leo kurejea kwao, baada ya kumalizana na klabu ya Simba
Simba ilimuacha Angban na kiungo Mussa Ndusha kutoka Jamhuriya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika dirisha dogo Desemba ili kupata nafasi ya kusajili Wathana, Kipa Daniel Agyei na kiungo James Kotei.
Lakini haikuweza kuwapatia haki zao wachezaji hao mapema hadi ilipofanya hivyo juzi – na sasa wote wanaondoka kurejea kwao kuendelea na maisha mengine.
Kipa huyo aliibukia katika klabu ya vijana ya Rio Sport d'Anyama kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza mwaka 2005, ambako hata hivyo miaka miwili baadaye aliondoka na kwenda kujiunga na Sawe Sports msimu wa 2006/2007.
Mwaka 2007, Angban akajiunga na ASEC Mimosas ambako alikuwa kipa wa kwanza hadi mwanzoni mwa msimu wa 2009 alipoumia na nafasi yake kuchukuliwa na Daniel Yeboah.
Yeboah akawavutia zaidi makocha wa timu hiyo kwa ubora wake wa kuokoa michomo na akaendelea kudaka hata Angban alipopona.
Baada ya kumaliza Mkataba wake ASEC, Angban akarejea Jeunesse na baadaye akaenda London kudakia U21 ya Chelsea.
Amewahi kudakia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Ivory Coast katika michuano ya Afrika nchini Benin mwaka 2005 na aliiwakilisha pia nchi yake katika Michezo ya Olimpiki mwaka 2008.
Amedakia pia timu ya taifa ya wakubwa ya Ivory Coast ‘Tembo’ katika michuano ya CHAN ikiwemo ile ya mwaka 2009 na ndiye aliyesimama langoni katika mechi na Tanzania, Taifa Stars ikishinda 1-0 bao pekee la Mrisho Ngassa.
Na anaondoka Simba SC baada ya kuidakia jumla ya mechi 56 na kufungwa mabao 25 huku mechi 34 akisimama langoni bila kuruhusu nyavu zake kuguswa.
Bocco asema Azam FC inafuata Kombe Zenji
Na Mwandishi Wetu
NAHODHA Azam FC, John Bocco ‘Adebayor’ amesema kwamba wanakwenda Zanzibar kwa lengo moja kubwa, kubeba Kombe la Mapinduzi.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi ilianza juzi visiwani Zanzibar na akizungumza na Nipashe jana mchana wakati wa safari yao ya kwenda visiwani humo, Bocco alisema kwamba wao kama wachezaji wamekubaliana kwenda kubeba Kombe.
“Mashindano ya Mapinduzi si mageni kwa Azam FC, michuano hiyo si miepesi ni migumu, sisi kama wachezaji tunaenda kushindana, naamini ni sehemu moja ya msimu huu ambayo tukiweza kuchukua Kombe itakuwa ni faraja kwa klabu na mashabiki wetu pamoja na sisi wachezaji, tukitoka huko hata tukirudi kwenye ligi tutakuwa na morali nzuri ya kuendeleza ushindi kwenye ligi, michuano ya FA na Kombe la Shirikisho Afrika,” alimalizia Bocco.
Azam FC inayodhaminiwa na na Azam Cola na benki ya NMB, inaenda huko ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kulitwaa taji hilo mara mbili mfululizo katika miaka ya 2012 na 2013. Azam itaanza kuwnaia taji la tatu la Mapinduzi kwa kumenyana na Zimamoto Jumatatu Saa 10.15 jioni kabla ya baadaye kucheza na Yanga ya Dar es Salaam na Jamhuri ya Pemba kukamilisha mechi za Kundi B.
Bocco pia amewatakia mashabiki wa timu hiyo heri ya mwaka mpya 2017 na kuwashukuru kwa sapoti yao waliyoionyesha mwaka huu.
“Kwanza tunawashukuru mashabiki wetu kwa uvumilivu waliouonyesha, kwa sapoti waliotupa katika kipindi chote kigumu tulichopitia, kama wachezaji na timu kwa ujumla tunawaomba waendelee kuwa na moyo huo huo na pia tunawatakia kheri ya mwaka mpya (2017) na wamalize mwaka huu vizuri, tuendelee kuwa pamoja ili kuisaidia timu yetu iweze kufanya vizuri,” alisema ,
Mbali ya taji la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati maarufu kama CECAFA Kagame, Azam pia inajivunia taji la Ngao ya Jamii waliyobeba Agosti 17, mwaka 2016 kwa kuichapa Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2 ndani ya dakika.
Toto Africans yawapania Stand, JKT Ruvu na Lyon
Na Mwandishi Wetu
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo miwili kwenye viwanja viwili tofauti nchini.
Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, wenyeji African Lyon wataikaribisha JKT Ruvu mchezo ambao awali ulipangwa kufanyika jana na Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans wataikaribisha Stand United ya Shinyanga.
Kocha wa JKT Ruvu, Bakari Shime alisema jana kwamba baada ya vijana wake kupoteza mechi mbili zilizopita mbele ya Yanga na Simba, leo watapaswa kupigana kiume washinde.
Shime alisema kwamba kwa kitambua JKT wapo kwenye nafasi mbaya katika msimamo wa Ligi Kuu, basi wamekubaliana na kupigana kiume kupata matokeo mazuri kuanzia sasa.
Kwa upande wake, Meneja Toto Africans, Khalfan Ngassa alisema kwamba baada ya sare ye ugenini na Mbeya City mjini Mbeya, vijana wake wamerejea na nguvu mpya mjini Mwazna kwa ajili ya kuwafunga Stand United.
“Mimi ninafahamu Stand United ni wazuri na mzunguko wa kwanza walifanya vizuri, lakini sisi tumejipanga vyema kuwafunga,”alisema Ngassa.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2hB5nm2
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang SIMBA YAMALIZANA VIZURI NA ANGBAN, NDUSHA WAREJEA KWAO LEO. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2016/12/simba-yamalizana-vizuri-na-angban.html. Terimakasih atas perhatiannya.