Na Mwandishi Wetu, MBEYA
KIUNGO mshambuliaji mpya wa Mbeya City FC, Zahor Pazi amemshukuru Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kwa kufanikisha kupatikana kwa hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) iliyokuwa imekwama Jamhuri ya KIdemokrasia ya Kongo (DRC) kwa miaka miwili.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mazoezi asubuhi ya leo kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, Zahor amesema kuwa anafuraha kubwa kuona amerudi rasmi kwenye ulimwengu wa soka baada ya kukaa nje kwa miaka miwili, licha ya jitihada kubwa alizokuwa akizifanya.
Zahor Pazi amemshukuru Rais wa TFF, Jamal Malinzi kwa kufanikisha kupatikana kwa ITC yake
"Namshukuru Mwenyezi Mungu, hakika natanguliza sifa kwake, nimekuwa nje ya soka la ushindani kwa miaka miwili sasa, mara kadhaa nimejaribu kufanya jitihada za kuhakikisha naokoa kipaji changu lakini sikufanikiwa, namshukuru rais wa TFF amefanikisha ndoto zangu za kuendelea kucheza mpira, niseme wazi kuna wakati nilikata tamaa kabisa, ingawa pia niliendelea kujipa moyo na kumuomba Mungu, nashukuru sasa niko huru na naweza kuitumikia timu yangu mpya, alisema.
Akiendelea zaidi Zahor alisema anawashukuru viongozi wa Mbeya City Fc kwa kumpa nafasi ya kuitumikia timu hii licha ya kutokuwa kwenye soka la ushindani kwa muda mrefu.
Nawashuruku viongozi wa mbeya city, wameniamini na wamenipa nafasi ya kujiunga na timu licha ya kutokucheza kwa muda mrefu, najua sitakuwa na miujiza ila nitajitahidi kutumia uwezo wangu wote niliojaaliwa na Mwenyezi muMungu na kwa kushirikiana na wenzangu naamini tutaifikisha mbali timu yetu, alisema Zahor na kuongeza kuwa anaimani kubwa City itaibuka na ushindi dhidi ya Mbao Fc jumamosi kufuatia mazoezi mazuri yaliyofanyia leo.
Aidha Zahor ametoa wito kwa wachezaji wenzake kuwa makini katika hatua zote zinazohusu usajili na uhamisho pale wanapohitaji kutoka timu moja kwenda nyingine.
Kwa wachezaji wenzangu kikubwa tuwe makini, nafahamu kuwa mara nyingi huwa tuna kiu kubwa ya kucheza nje, kila mmoja ana ndoto hizo ni vyema kuangalia na kufanya mambo kwa makini, yaliyonikuta mimi sikuyapanga ila kuna njia ambazo zilitumika ndivyo sivyo mpaka ikafika hapo ilipofika hivyo ni vyema kuwa na watu makini na madhubuti ambao wanaosiamamia mambo yetu, alimaliza.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2ii19Ex
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms