Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
YANGA SC imefuzu raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Ngaya Club de Mde ya Comoro jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inafuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 6-2, baada ya Jumapili iliyopita kushinda 5-1 ugenini mjini Moroni, Comoro.
Mchezo huo uliochezeshwa na marefa Alex Muhabi, washika vibendera Ronald Katenya na Lee Okello hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1.
Na Ngaya ndiyo waliokuwa wa kwanza kuepata bao dakika ya 19 kupitia kwa Zahir Mohammed aliyefuua shuti baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Yanga na mpira ukampita kipa namba moja Tanzania, Deo Munishi ‘Dida’.
Yanga ilisawazisha bao hilo dakika ya 43 kupitia kwa beki wa kushoto Mwinyi Hajji Mngwali, aliyefumua shuti kali kutoka umbali wa mita 25, baada ya pasi ya Kevin Yondan.
Kipindi cha pili, timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu na kosa kosa zikawa za pande zote mbili.
Lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao na kwa matokeo hayo, Yanga sasa itamenyana na Zanaco ya Zambia, ambayo imeitoa APR ya Rwanda.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Justin Zulu, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Deus Kaseke, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin.
Ngaya SC; Said Mmadi, Said Hachim, Chadhuili Mradabi, Said Anfane, Franck Said Abderemane, Youssouf Ibrahim Moidjie, Rakotoarimanana Falinirino, Berthe Alpha, Zamir Mohammed, Mounir Moussa na Said Toihir.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2lVq1Ef
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms