Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MGOMBEA nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mulamu Erick Ng'ambi ameahidi kuendeleza mpira wa miguu kwa kushirikiana na mikoa yote kwa kutumia mpango mkakati wa kitaifa, ambao ndio utakuwa ndio dira ya mchezo huo nchini endapo atachaguliwa katika uchaguzi wa Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
Akizungumza kwenye mkumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Dar es Salaam leo kwenye uzinduzi wa kampeni zake, Ng’ambi amesema endapo atapata nafasi hiyo ataitendea haki kutokana na uzoefu alionao baada ya kutumikia nyadhifa mbalimbali katika soka hapa nchini.
Mulamu Ng'ambi ameahidi kuendeleza soka nchini akichaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TFF katika uchaguzi wa Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma
Ng’ambi amesema dira yake imegawanyika katika maeneo matatu, ambayo ni mipango muda mfupi, wa kati na muda mrefu – ambayo italeta mapinduzi makubwa katika soka ya Tanzania.
Kuhusu mipango ya muda mfupi, amesema kwamba atasimamia udhibiti wa fedha kwenye shirikisho kwa kuziba mianya yote ya upotevu au matumizi ambayo hayana ulazima pamoja na kuongeza mapato kwa kutumia njia ya mawasiliano kwa kutumia njia maalum watakazotengeneza.
Kuhusu mipango ya muda wa kati, Ng’ambi amesema atashirikiana na Kamati ya Utendaji katika kuboresha Ligi, kuanzia Ligi Kuu hadi Ligi ya Mabingwa wa Mkoa kwa kuongeza udhamini kwenye ligi hizo.
Na kwenye mipango ya muda mrefu, Ng’ambi amesema atafanya marekebisho makubwa katika hosteli za TFF zilizopo makao makuu ya shirikisho hilo, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam ziwe katika kiwango cha nyota tatu, ili ziweze kutumika kwa timu za taifa pale zitakapohitajika kuingia kambini.
“Hii itasaidia kupunguza gharama kubwa ambazo zimekuwa zikitumika kulipa kambi katika hoteli mbalimbali, ili kuhakikisha mpira unapiga hatua kwa kushirikiana na mashirikisho mengine duniani kwa kuandaa semina mbalimbali kwa ajili ya viongozi wa klabu,”amesema Ngambi.
Katika nafasi hiyo, Ng’ambi anachuana na Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa wakati wagombea Urais ni Ally Mayay, Frederick Mwakalebela, Imani Madega, Wallace Karia, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2uhFhfc
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang MGOMBEA TFF AJA NA MIPANGO ‘BABU KUBWA’, NI MULAMU NG’AMBI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/08/mgombea-tff-aja-na-mipango-babu-kubwa.html. Terimakasih atas perhatiannya.