Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WAKATi zimebaki siku nne (4) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kwa msimu wa 2017/18, tunazikumbusha klabu 16 za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL); timu 24 za Ligi Daraja la Kwanza na 24 Ligi Daraja la Pili kukamilisha usajili kwa Mfumo wa Mtandao wa TMS – Transfer Matching System.
Taarifa ya Alfred Lucas, Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imekumbusha kwamba dirisha la usajili litafungwa Agosti 6, mwaka huu na ametoa angalizo kwamba hakuna klabu itakayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kama haitapata leseni ya klabu.
Baadhi ya klabu hazijachukua hata fomu za leseni ya klabu wakati zile zilizochukua kuna baadhi hazijarejesha na pamoja kwamba kuna zile ambazo zimerejesha, lakini baadhi inaonekana hazikujazwa kwa usahihi.
Kikao cha Kamati ya Leseni za Klabu, chini ya Msomi Wakili Lloyd Nchunga kinatarajiwa kuketi Jumamosi Agosti 5, mwaka huu kwenye ofisi za TFF, Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam ambako kitapitia fomu zilizorejeshwa kabla ya kufanya uamuzi wa kutoa leseni kwa klabu zilizotimiza masharti.
Klabu ambayo haitapata leseni kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), haitakuwa na nafasi ya kushiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2017/18.
Suala la leseni linakwenda pia kwa wachezaji. Kama ilivyokwisha kutangazwa, hakuna mchezaji atakayeshiriki Ligi Kuu ya Vodacom, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili - michuano inayoendeshwa na kusimamiwa na TFF kama hakutimiza masharti ya kupata leseni ya kumruhusu kucheza.
Wakati hayo yakiagizwa, maandalizi ya ujio mpya wa msimu wa mashindano yanaendelea ambako kwa kesho Alhamisi, Agosti 3, mwaka huu Kampuni ya Vodacom - inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano nchini Tanzania itatoa vifaa vya mchezo kwa timu zote 16 za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kuwa ndiyo Mdhamini Mkuu wa michuano hiyo yenye ushindani mkali. Vodacom wanafanya hivyo kwa mujibu wa mkataba wa udhamini.
KUNA VIGEZO SITA (6) VYA MCHEZAJI KUPATA LESENI AMBAVYO NI: -
1. Kujazwa fomu ua utimamu wa afya (Medical Form).
2. Bima ya matibabu kwa mchezaji.
3. Barua ya uhamisho (Release Letter).
4. Hati ya Uhamisho wa Kimataifa kwa wachezaji wa kigeni.
5. Mikataba ya wachezaji iliyosajiliwa kwenye mfumo wa usajili TMS
6. Ada ya wachezaji wa kigeni ambayo ni Sh 2,000,000 badala ya dola 2,000 za Marekani.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2tZviec
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang TFF YATOA TAHADHARI KWA KLABU KUHUSU USAJILI LIGI KUU. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/08/tff-yatoa-tahadhari-kwa-klabu-kuhusu.html. Terimakasih atas perhatiannya.