• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2026 (306)
    • ►  Juli (36)
    • ►  Juni (53)
    • ►  Mei (40)
    • ►  April (34)
    • ►  Maret (34)
    • ►  Februari (42)
    • ►  Januari (67)
  • ►  2025 (318)
    • ►  Desember (70)
    • ►  November (4)
    • ►  September (1)
    • ►  Juli (2)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ►  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ►  November (405)
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ►  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (411)
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ►  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ►  Oktober (535)
    • ►  September (484)
    • ►  Agustus (487)
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ▼  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ►  November (567)
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ▼  Agustus (555)
      • MAKAMU WA RAIS TFF, WAMBURA ALIKUWA KAMISAA JANA K...
      • OKWI AIPAISHA UGANDA KILELENI KUNDI E KUFUZU KOMBE...
      • UBELGIJI NOMA, YAIFUMUA GIBRALTAR 9-0, LUKAKU APIG...
      • RONALDO APIGA HAT TRICK, URENO YASHNDA 5-1 KUFUZU ...
      • LEMAR 'WA ARSENAL', AIPIGIA MBILI UFARANSA YAILAZA...
      • MBAPPE ATUA PSG KWA MKOPO KUTOKA MONACO
      • MSUVA KUJIUNGA NA STARS JUMATANO, BANDA ANATUA LEO
      • APR YAMSAJILI MCHEZAJI ALIYEGOMA KUCHEZA BURE HISP...
      • SIMBA WAPANGA KUMFIKISHA MAHAKAMANI BUSWITA KWA UT...
      • World Cup Qualifier: Uruguay v Argentina Preview
      • 2018 UEFA World Cup Qualifier: Spain v Italy Preview
      • Pro 14: Ulster vs Cheetahs Preview
      • Pro 14: Scarlets v Southern Kings Preview
      • Aviva Premiership: Gloucester vs Exeter Chiefs Pre...
      • World Cup Qualifiers: Selected Quad Preview
      • Opinion: Rights and wrongs of T20 Global League pl...
      • CAF World Cup Qualifiers: Round 3 Preview
      • European Tour: D&D Real Czech Masters Preview
      • World Cup Qualifier: Cape Verde v South Africa Pre...
      • KESI YA AVEVA, KABURU YAPIGWA KALENDA TENA, WARUDI...
      • PGA Tour: Dell Technologies Championship Preview
      • Bangladesh Claim Historic Win in Mirpur
      • Kenilworth Wednesday 30 August 2017 Best Bets
      • Windies Shock England by winning 2nd Test
      • ABDI BANDA NDANI YA NDEGE ANAKUA DAR KUJIUNGA NA S...
      • HATIMA YA CHIRWA WA YANGA KUJULIKANA KESHOKUTWA
      • MSUVA KUJIUNGA NA STARS JUMATANO, BANDA ANATUA LEO
      • MSUVA KUJIUNGA NA STARS JUMATANO, BANDA ANATUA LEO
      • SANGA WA YANGA AWANIA UENYEKITI BODI YA LIGI
      • European Rugby Champions Cup: Pool 2 Preview
      • Currie Cup Round 8: Blue Bulls v Griquas Preview
      • Aviva Premiership: Outright Preview
      • Mbappe: PSG’s Missing Link
      • Sri Lanka v India: Fourth ODI Preview
      • Atletico and Chelsea reach Compromise?
      • Alexis Sanchez on the brink of Arsenal Exit
      • MBAO FC YAPATA UDHAMINI MWINGINE, GF TRUCKS WAMWAG...
      • 3 Chelsea Transfer Deadline Signings?
      • Vaal Tuesday 29 August 2017 Best Bets
      • WACHEZAJI STARS WAINGIA KAMBINI, ‘MAPRO’ KUANZA KU...
      • 2017 US Open: Men Draw Preview
      • 2017 US Open: Women's Draw Preview
      • MAPEMA TU, TFF WABOMOA RATIBA YA LIGI KUU
      • SIMBA KUMPELEKA NDUNDA INDIA KWA MATIBABU YA GOTI
      • 2017 US Open Preview
      • DEMBELE ALIPOWASILI RASMI BARCELONA KUANZA KAZI
      • KIMWAGA AZUA HOFU AZAM BAADA YA KUUMIA DHIDI YA ND...
      • Fairview Monday 28 August 2017 Best Bets
      • MSUVA APIGA BAO KOMBE LA MOROCCO, JADIDA YASHINDA 3-1
      • T20 Global League 2017 Squads
      • YANGA NA LIPULI KATIKA PICHA JANA TAIFA
      • REAL MADRID 2-2 VALENCIA
      • WAFALME WA SOKA HISPANIA, ULAYA NA DUNIANI
      • REAL MADRID YALAZIMISHWA SARE LA LIGA, 2-2 NA VALE...
      • CHELSEA 2-0 EVERTON
      • LIVERPOOL 4-0 ARSENAL
      • KAPTENI MKUCHIKA NA MKWASA WAKIISHUHUDIA YANGA YAO...
      • MAYWEATHER 'ALIVYONOGA' KATIKA PATI LA USHINDI
      • LIVERPOOL YAIFANYIA MAMBO YA AJABU ARSENAL...4-0
      • CHELSEA YAWASHA MOTO ENGLAND, YAIPIGA 2-0 EVERTON
      • YANGA YAANZA NA SARE, 1-1 NA LIPULI TAIFA
      • SIMBA NA RUVU SHOOTING KATIKA PICHA JANA UHURU
      • KUTOKA SERENGETI BOYS HADI ETOILE DU SAHEL, MUNGU ...
      • KOCHA TWIGA STARS AENDA MASOMONI UJERUMANI
      • Boks Dominate in Salta
      • MAYWEATHER V MCGREGOR
      • AFC BOURNEMOUTH 1-2 MAN CITY
      • MAN UNITED 2-0 LEICESTER CITY
      • Mayweather defeats McGregor by TKO
      • MAYWEATHER AMUADHIBU MCGREGOR 'KAMA MTOTO' ULINGONI
      • MZEE KAWAWA ALIISHUHUDIA MAJI MAJI IKIPIGWA 3-0 NA...
      • HII YA BUSWITA MBONA IMEZUKA ZUKA TU NA HAIONYESHI...
      • SAMATTA ATOKEA BENCHI BADO DAKIKA SABA GENK YASHIN...
      • Scottsville Sunday 27 August 2017 Best Bets
      • English Premier League: Week 3 Results
      • Italian Serie A: Round 2 Results
      • German Bundesliga: Week 2 Results
      • Spanish La Liga: Week 2 Results
      • Dutch Eredivisie: Week 3 Results
      • French Ligue: Round 4 Results
      • OKWI AITWA KUIBEBA UGANDA KUFUZU KOMBE LA DUNIA
      • MESSI AFUNGA ZOTE MBILI, BARCA YAUA 2-0 LA LIGA
      • MAN UNITED YAENDELEZA UBABE ENGLAND, YAILIMA 2-0 L...
      • SIMBA YAANZA LIGI KUU NA MOTO WA UBINGWA, OKWI API...
      • STERLING AIFUNGIA LA USHINDI MAN CITY DAKIKA YA MW...
      • MAYANGA AWAREJESHA YONDAN NA MWADINI TAIFA STARS
      • New Zealand Edge Australia in Dunedin Thriller
      • Sri Lanka v India: Third ODI Preview
      • MAYWEATHER NA MC GREGOR WAKUTWA NA UZITO SAWA
      • NIYONZIMA: SIMBA NAJIONA KAMA NIMEZALIWA UPYA
      • VPL: LIGI BORA AFRIKA MASHARIKI INAYOLETWA NA VODA...
      • HAZARD ASEMA CHELSEA INA UWZO WA KUTANDIKA BIFFON
      • MTIBWA SUGAR YAAHIDI KUFANYA KWELI LIGI KUU
      • AZAM FC IPO KAMILI GADO KWA AJILI YA NDANDA MTWARA
      • BARCELONA YATANGAZA KUMSAJILI DEMBELE KWA PAUNI MI...
      • VILLA AREJESHWA KIKOSINI HISPANIA BAADA YA MIAKA M...
      • VAN PERSIE AREJESHWA KIKOSINI UHOLANZI BAADA YA MI...
      • SIMBA NA RUVU, YANGA NA LIPULI KUPIGWA SHAMBA LA BIBI
      • RAIS FIFA AUPONGEZA UONGOZI MPYA TFF, AAHIDI KUEND...
      • MIYEYUSHO ULINGONI NA BAINA 'SIMBA' MAZOLA KINONDO...
      • Turffontein Saturday 26 August 2017 Best Bets
      • Kenilworth Saturday 26 August 2017 Best Bets
      • Women’s Rugby World Cup: Round 5 Preview
      • F1 2017: Belgian Grand Prix Preview
      • ARSENAL YAPANGWA NA FC COLOGNE, BATE LIGI YA ULAYA
      • Pro 14: Pool 2 Preview
      • Women's Rugby World Cup 2017: England vs New Zeala...
      • MAYWEATHER AWEKEWA ULINZI MKALI KUELEKEA PAMBANO N...
      • Fairview Friday 24 August 2017 Best Bets
      • EVERTON FC YASONGA MBELE EUROPA LAGUE 2017
      • NI RONALDO MWANASOKA BORA TENA ULAYA
      • MAN UNITED YAPANGWA NA BENFICA, SPURS NA CHELSEA Z...
      • UEFA Champions League: 2017/18 Group Stage Draw Re...
      • AZAM FC WAPO KAMILI MTWARA TAYARI KUIVAA NDANDA JU...
      • Currie Cup Round 7: Western Province v Sharks
      • MESSI AWASILI KWA HELIKOPTA KWENYE 'TUZO YA RONALDO'
      • Currie Cup: Round 7 Preview
      • Italian Serie A: Week 2 Preview
      • England vs West Indies: Second Test Preview
      • Rugby Championship: Argentina vs South Africa
      • SANCHEZ AKAMILISHA UHAMISHO WA DAU LA REKODI SPURS
      • WAYNE ROONEY AAMUA KUSTAAFU SOKA YA KIMATAIFA
      • WAYNE ROONEY AAMUA KUSTAAFU SOKA YA KIMATAIFA
      • English Championship: Week 5 Preview
      • Daniel du Preez on the Brink of a Springbok Cap
      • MTN 8 Semi-Finals: First Legs Preview
      • PSL: Week 2 Results
      • LIVERPOOL 4-2 HOFFENHEIM
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ►  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ►  November (509)
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE » TUNAHITAJI NINI ZAIDI YA VURUGU KAMA ZA OKTOBA 1 SIMBA NA YANGA?

TUNAHITAJI NINI ZAIDI YA VURUGU KAMA ZA OKTOBA 1 SIMBA NA YANGA?

REFA Martin Saanya aliyechezesha mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga Oktoba 1, mwaka jana alifungiwa miaka miwili kwa pamoja na Msaidizi wake, namba moja, Samuel Mpenzu.
Na pamoja na kuwafungia waamuzi huo kwa makosa ya kutoa maamuzi ya utata, pia Kamati ya Masaa 72 ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilifuta Kadi nyekundu ya mchezaji Jonas Mkude baada ya kubaini hakufanya kosa.
Maamuzi ya utata ya Saanya yalisababisha vurugu Uwanja wa Taifa Jumamosi ya Oktoba 1, mwaka jana baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Tambwe alifunga bao hilo dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
Kwa hali hiyo, mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani. Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya.
Na Mpenzu naye alidaiwa kukataa bao safi la Simba lililofungwa na Ibrahim Hajib mapema kipindi cha kwanza akidai aliotea.
Mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu baina ya miamba hiyo ulichezeshwa na refa Mathew Akrama kutoka Mwanza Februari 25, mwaka huu pale pale Taifa. 
Winga Shiza Ramadhani Kichuya, kwa mara nyingine aliibuka shujaa wa Simba baada ya kutokea benchi na kuisaidia timu yake kushinda 2-1.
Kichuya aliyempokea beki Novatus Lufunga dakika ya 55, kwanza alimsetia mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo kuifungia bao la kusawazisha Simba dakika ya 66 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la ushindi dakika ya 81.
Kama Oktoba 1, na Februari 25 Yanga SC walitangulia kwa bao la mapema tu dakika ya tano la Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti, baada ya kiungo Mzambia, Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi na Lufunga.
Akrama alimtoa nje kwa kadi nyekundu beki Mkongo wa Simba, Janvier Besala Bokungu dakika ya 55 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu Chirwa.
Akrama alikuwa mwiba kwa timu zote mbili siku hiyo kutokana na maamuzi yake ya kufuata sheria 17 za soka bila kusita pale tu lilipotokea kosa, hali ambayo ilisababisha wachezaji wenyewe waamue kuwa na nidhamu uwanjani.
Na kazi nzuri ya Akrama Oktoba 1 ilikuwa sawa na kusahihisha makosa yake ya Oktoba 3, mwaka 2012 alipochezesha kwa mara ya kwanza mechi ya watani hao wa jadi, ikiwa ya Ligi Kuu pia timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa. 
Katika mchezo huo ulioanza Saa 1:02 usiku, Akrama alimtoa kwa kadi nyekundu winga Simon Msuva wa Yanga dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu beki wa Simba, Juma Nyosso.
Siku hiyo, Simba ndiyo walitangulia kwa bao la kiungo Amri Kiemba dakika ya pili, kabla ya mshambuliaji Said Bahanuzi kuisawazishia Yanga dakika ya 63 kwa penalti baada ya beki Paul Ngalema kuunawa mpira kwenye boksi.
Lakini Akrama alilaumiwa kwa kumuonyesha kadi ya njano badala ya nyekundu kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ licha ya kumchezea rafu mbaya beki wa Yanga, Kevin Yondan hadi akashindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul.
Na pia alilaumiwa kuwa kutomchukulia hatua yoyote kipa Juma Kaseja aliyeonekana kupoteza muda tangu mwanzo, na alimpa onyo tu zaidi ya mara tatu.
Haikuwa ajabu Oktoba 6 Akrama alipoondolewa kwenye orodha ya wamuzi wa kuchezeaha Ligi Kuu baada ya kuvurunda mechi hiyo namba 80, huku aliyekuwa mshika kibendera namba mbili, Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam akipewa onyo.
Lakini bado kazi nzuri ya Akrama Februari 25 haiwezi kunibadilisha msimamo wangu wa muda mrefu wa kutaka mechi za watani hawa wa jadi zichezeshwe na marefa wa nje – ila kwa kuwa wenye mamlaka, TFF na Bodi ya Ligi hawajaona umuhimu wa hilo chochote nitakachoandika kitakuwa sawa na kelele za chura, hazitamzuia ng’ombe kunywa maji. 
Lakini ukweli unabaki pale pale, marefa wetu wamesababisha adha kubwa kwenye mechi za watani, achilia mbali za Oktoba 1, mwaka jana kuna matukio mengine makubwa ya kihistoria yamewahi kutokea na kuhatarisha hata maisha ya viongozi wetu wakubwa wa nchi.
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi alinusurika katika tukio la hatari Machi 31, mwaka 2002 katika fainali ya Kombe la Tusker, Simba ikishinda 4-1.
Siku hiyo refa Abdulkadir Omar ‘Msomali’ aliivuruga mechi na kuhatarisha amani uwanjani pia kwa madudu yake.
Mechi hiyo ya fainali ambayo Alhaj Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa alikuwa mgeni rasi – chupuchupu  ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka Suleiman kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. 
Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. 
Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania, (FAT), sasa TFF kabla ya kujiuzulu uongozi wa klabu hiyo baadaye.
Ni marefa wachache sana wamewahi kuziongoza vizuri mechi za Simba na Yanga na zikamalizika bila manung’uniko, akiwemo mwanamama mwenye beji ya FIFA, Donisya Rukyaa wa Kagera anayefuata nyayo za marefa wakongwe kama Nassor Hamdon wa Kigoma.
Tathmini mbalimbali za kitaalamu za vyombo vya habari vya kimataifa zimekwishaipitisha mechi ya Simba na Yanga kama moja ya mechi kubwa mno za watani wa jadi Afrika.
Tatizo kubwa ni marefa, kweli ilipofikia na kama kweli lengo ni kuiongezea msisimko zaidi mechi ya watani, waamuzi wa Tanzania wawekwe kando na watumike waamuzi kutoka nje ya nchi, tena ikibidi nje kabisa ya nchi tatu za Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.
Rejea hata mchezo wa Machi 5, mwaka 2011 Uwanja wa Taifa, refa Orden Mbaga aliivuruga mno mechi hiyo, kutokana tu na pengine mchecheto ama kutaka kufanya kile ambacho kinaitwa ‘kubalansi’ mchezo au kukwepa lawama, matokeo yake akafanya madudu.
Dakika ya 58 Juma Said Nyosso alimkwatua Mzambia Davies Robby Mwape kwenye eneo la hatari akawapa penalti Yanga na kilichofuatia wengi walijua beki huyo wa Simba atatolewa nje kwa kadi nyekundu, badala yake akampa kadi ya njano.
Ngumu kuamini Mbaga, refa mwenye beji ya Shrikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hajui alipaswa kufanya nini kwa Nyosso, lakini kwa sababu ni refa wa nyumbani na aliongoza wapinzani wa jadi katika mechi ya nyumbani, alihofia kumtoa mchezaji kwa kadi nyekundu angeshushiwa lawama nzito. Marefa hufanyiwa fujo na kupigwa na mashabiki, labda alihofia hali hiyo pia.
Dakika ya 73 Simba walipata bao safi la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Mussa Hassan Mgosi, aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa Mghana Yaw Berko kufuatia shuti la mpira wa adhabu, lililogonga mwamba wa juu na kudondokea nyavuni kabla ya kuokolewa na mabeki wa Yanga.
Halikuwa bao lenye shaka yoyote, hakukuwa na kuotea wala dosari yoyote, lakini haieleweki kwa nini Mbaga alilikataa bao hilo awali.
Ilikuwa offside au mpira haukutinga nyavuni hadi akalikataa kwanza? Haijulikani, lakini alilikubali baada ya wachezaji wa Simba kumuambia aangalie kwenye TV kubwa iliyopo uwanjani marudio ya tukio lile na baada ya hapo akaenda kujadiliana na msaidizi wake, ndipo akalikubali.
Tujiulize, kusingekuwa na ile TV, Simba wangedhulumiwa bao lao?
Mbaga alichemsha- lakini si Mbaga tu, marefa wengi wa Tanzania waliwahi kutokota kabla yake na nitakumbushia baadhi ya mechi.   
Agosti 18, mwaka 2002 Simba na Yanga zikitoka sare ya 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu, refa Victor Mwandike aliwaacha mashabiki wa Simba midomo wazi kwa kuwapa Yanga penalti ya utata dakika ya 89 na ushei, ambayo Sekilojo Chambua aliitumia vema kuisawazishia bao timu yake, baada ya Simba kutangulia kufunga kupitia kwa Madaraka Suleiman dakika ya 65.
Oktoba 24, mwaka 2007, refa Osman Kazi alikataa mabao matatu yaliyofungwa na Yanga, yote akidai kipa Juma Kaseja alisukumwa na wachezaji wa Yanga, lakini kwa yeyote atakayerudia kuangalia DVD ya mchezo ule, hawezi kuona ukweli wa madai ya Kazi.
Awali ya hapo, Kazi aliwahi kupuliza filimbi ya kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza katika Nusu Fainali ya Kombe la Tusker mwaka 2005 mjini Mwanza, wakati mchezaji wa Yanga, Said Maulid ‘SMG’ amekwishawatoka mabeki wa Simba na anakwenda na mpira mbele yake amebaki Juma Kaseja tu.
Refa ni mwamuzi wa mwisho- lakini kwa wana Yanga walijutia mno tukio lile kwenye mchezo ambao mwishowe walifungwa 2-0, kwa mabao ya kipindi cha pili ya Emmanuel Gabriel na Mussa Mgosi.
Aprili 19, mwaka 2009, Jerry Tegete aliifungia Yanga bao la kusawazisha kwa mkono na kutengeneza sare ya 2-2, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Refa makini asingeweza kukubali bao lile, hivyo kwa haya yote lazima tukubali marefa wa Tanzania hawawezi tena kuchezesha mechi za watani wa jadi.
Sababu nyingine za marefa wetu kuzishindwa mechi hizo ni hiyo ya mapenzi yao kwa moja ya timu hizo, kitu ambacho Misri wamekiepuka na mechi ya Zamalek na Ahly inachezeshwa na marefa kutoka nje ya nchi yao.
Nakumbuka refa kutoka Uganda, Dennis Bate aliyechezesha fainali ya mwisho ya Kombe la Tusker mwaka 2009 kati ya Simba na Yanga, aliiongoza vizuri mechi hiyo na akadhibiti ujanja wote wa wachezaji kutaka kumdanganya na hatimaye aboronge.
Kuna wachezaji wanaitwa wazoefu wa mechi za Simba na Yanga na hawa wamekuwa wakiwapoteza sana marefa kwa uzoefu wa kucheza mechi hizo, lakini kama marefa watatoka nje ya Tanzania, tena wa kiwango cha beji za FIFA, uhondo wa mechi za watani utaongezeka maradufu. 
Sijui TFF wanahitaji nini zaidi ya vurugu kama za Oktoba 1 mwaka jana ili kuacha kukaidi na kuanza kutumia marefa wa kigeni kwenye mechi watani? 


from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2wdjjhC best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang TUNAHITAJI NINI ZAIDI YA VURUGU KAMA ZA OKTOBA 1 SIMBA NA YANGA?. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/08/tunahitaji-nini-zaidi-ya-vurugu-kama-za.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 23.01
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • SHIME ANAAMINI TANZANIA ITAICHAPA UGANDA KESHO KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U-17
    SHIME ANAAMINI TANZANIA ITAICHAPA UGANDA KESHO KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U-17
    Na Stella Theopist, DAR ES SALAAM  KOCHA Mkuu wa timu ya wanawake u-17  ya Tanzania, Bakari Shime amesema kuwa kikosi kimejipanga kufanya v...
  • MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MSHIRIKI MISS AFRIKA UINGEREZA AHADITHIA MAMBO YALIVYO
    MTANZANIA Alice Gyunda miongoni mwa washiriki 20 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliofanikiwa kuingia kwenye kinyang'anyiro cha taj...
  • GYNAH ASHINDA TUZO ZA LIPFF KENYA
    GYNAH ASHINDA TUZO ZA LIPFF KENYA
    MWANDISHI, muigizaji na mwanamitindo, Regina Kihwele 'Gynah', mwanamziki ameibuka mshindi wa  muigizaji bora kike kwenye tuzo  za...
  • TUZO ZA LIGI KUU ZABORESHWA, SASA WACHEZAJI KUPEWA NA KING'AMUZI CHA AZAM TV
    Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura, akionyesha tuzo atakayokuwa akipewa Mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vod...
  • BARCELONA 3-1 ALAVES
    BARCELONA 3-1 ALAVES
    from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2s2Iqyx
  • EPL: Week 36 Preview
    EPL: Week 36 Preview
    We preview week 36 of the 2017/18 English Premier League season which is set to get underway on Saturday 28 April.  We’re into the final s...
  • Hollywoodbets Extends Horse Racing Sponsorship with Grooms' Initiative
    Hollywoodbets Extends Horse Racing Sponsorship with Grooms' Initiative
    Hollywoodbets have extended their original R10 million three-year sponsorship of Gold Circle by a further R1.5 million per year with the an...
  • CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
    BAO pekee la beki wa kimataifa wa England, Ben Chilwell dakika ya 45 limeipa Chelsea ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Brentford Uwanja wa...
  • ARSENAL YAMUONGEZEA MSHAHARA SANCHEZ ASIENDE BAYERN MUNICH
    KLABU ya Arsenal imempa ofa nyingine mshambuliaji wake, Alexis Sanchez aachane na mpango wa kwenda Bayern Munich na abaki Emirates. Ofa mp...
  • ENGLAND YALAZIMISHWA SARE WEMBLEY
    ENGLAND YALAZIMISHWA SARE WEMBLEY
    WENYEJI, England wamelazimishwa sare ya 1-1 na Hungary katika mchezo wa Kundi I kufuzu Kombe la Dunia kwa Ulaya usiku wa kuamkia leo Uwan...
Copyright Viral Sports: TUNAHITAJI NINI ZAIDI YA VURUGU KAMA ZA OKTOBA 1 SIMBA NA YANGA?