Na Mwandishi Wetu, DJIBOUTI CITY
SIMBA SC imesonga mbele Raundi ya Kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika kwa ushindi wa jumla wa 5-0 dhidi ya Gendarmerie Tnare ya Djibouti baada ya ushindi wa 1-0 jioni ya leo mjini Djibouti City.
Katika mchezo wa leo uliofanyika Uwanja wa El Hadj Hassan Gouled, bao pekee la ushindi la Simba limefungwa na mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi dakika ya 55.
Kwa kuunganisha na ushindi wa 4-0 kwenye mechi ya kwanza jumapili ya wiki iliyopita, Simba SC inayofundishwa na kocha Mfaransa Pierre Lechantre anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma, Mtunisia Mohamed Aymen Hbibi ambaye ni mchua misuli na Muharami Mohamed, kocha wa makipa inasonga mbele kwa ushindi wa 5-0 na sasa itasubiri mshindi wa jumla wa mechi kati ya El Masry ya Misri na Green Buffaloes ya Zambia ikutane raundi ijayo.
Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi ameifungia Simba bao pekee leo ikishinda 1-0 dhidi ya Gendarmerie Tnare mjini Djibouti City
Ikumbukwe, mchezo wa kwanza El Masry iliishindilia 4-0 Green Buffaloes mjini Cairo na kesho zitarudiana nchini Zambia.
Katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam, Okwi alifunga pia bao moja, la nne baada ya kiungo Said Ndemla kufunga la kwanza na mengine mawili kufungwa na Nahodha John Raphael Bocco, aliyekosekana kwenye mechi ya leo kutokana na kuwa majeruhi.
Kikosi cha Simba SC kilichoanza leo kilikuwa; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Yussuph Mlipili, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, James Kotei, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi na Muzamil Yassin.
Kikosi cha Simba kilichoanza leo mjini Djibouti City dhidi ya Gendarmerie Tnare
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2GwMTA9
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms