Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MJUMBE wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Samuel Lukumay yupo mjini Victoria, Shelisheli tangu Alhamisi kuandaa utaratibu wa timu itakapowasili huko kesho hadi kuondoka baada ya mchezo na wenyeji, Saint Louis Suns United.
Yanga SC inatarajiwa kuondoka kesho mchana kwenda mjini Victoria kwa ajili ya mchezo wa marudiano hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Saint Louis Suns utakaofanyika siku ya Jumatano mjini humo.
Na katika kuhakikisha wanafikia katika mazingira salama na kuepuka hujuma za wenyeji kuelekea mchezo huo, ambao wanahitaji kuulinda ushindi wao mwembamba wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza ili kwenda kuwania kuingia hatua ya makundi.
Obrey Chirwa atakosekana Yanga SC kwenye mchezo wa marudiano na Saint Louis nchiji Shelisheli
Samuel Lukumay (kushoto) yupo mjini Victoria, Shelisheli tangu Alhamisi kuandaa utaratibu wa timu itakapowasili
Lukumay amekwishaandaa mazingira ya timu kufikia mjini kuanzia hoteli ya kuishi, chakula salama hadi Uwanja wa kufanyia mazoezi. Na kwa miaka ya karibuni, Lukumay ndiye amekuwa akitangulizwa na Yanga ugenini kufanya kazi hiyo na kwa kiasi kikubwa amekuwa akiifanya vizuri.
Yanga itaondoka kesho bila wachezaji wake wanne, beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na washambuliaji watatu, mzawa Yohanna Oscar Nkomola, Mrundi Amissi Tambwe na Mzimbabwe Donald Ngoma hawatasafiri kwa sababu wote bado majeruhi.
Yanga wanahitaji kuulinda ushindi wao mwembamba wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam
Pamoja na hayo, kocha Mzambia, George Lwandamina anajivunia kikosi chake kipana kinachojumuisha wachezaji chipukizi ambao wamekuwa wakiibeba timu katika wakati mgumu.
Yanga ilionekana kufanyia kazi makosa yake baada ya Jumatano kushinda 4-1 dhidi ya Maji Maji ya Songea katika mchezo uliofuata wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2CuCfaM
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms