Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji amesema kwamba anaanza kupambana ili atimize ndoto za kumiliki ndege binafsi.
Samatta ameposti picha akiwa kweye mlango wa ndege binafasi ya klabu yake, Genk na kuandika; “Ndoto za kumiliki ndege binafsi zimeanza baada ya kupiga picha hii, siyo kila ndoto inaweza kutimia. Ila, acha vita ianze,”.
Samatta amerejea Ulaya baada ya Jumamosi kuichezea Taifa Stars mechi ya Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Cameroon ikilazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, Uganda Jumamosi Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala.
|
Mbwana Samatta amesema kwamba anaanza kupambana ili atimize ndoto za kumiliki ndege binafsi |
Lakini Samatta amerejea Ubelgiji akiwa hana furaha baada ya kukosa bao la wazi Jumamosi Namboole kiasi cha kulazimika kuwaomba radhi Watanzania, akisema kwamba hakuwa na bahati siku hiyo, kwani amekuwa akifunga mabao katika mazingira magumu mno, lakini siku hiyo alishindwa kutumia nafasi nyepesi.
“Mimi ninafikiri huwa nakuwa sina shaka na ubora wangu hususan za ufungaji. Na kitu ambacho nilikuwa nacho pale ni kwamba naenda kufunga, hiyo ilikuwa haina shaka kwamba naweza kufunga. Na ilikuwa ni nafasi nyepesi ukilinganisha na nafasi nyingine ambazo huwa ninafunga,”.
“Kwa hiyo naweza kusema sikuwa na bahati labda, inaweza kuwa hivyo ilitokea (juzi) bahati mbaya sijafunga, lakini ninadhani ni kitu ambacho kiliniumiza sana kwa sababu ni nafasi ambayo nilikuwa nikiitafuta katika mchezo mzima niweze kuipata, lakini baada ya kuipata nikashindwa kuitumia,”.
Samatta alisema kwamba si kitu kizuri kwa mshambuliaji kupoteza nafasi nzuri za aina ile na ndiyo maana usiku wa kuamkia jana hakupata usingizi akikesha anafikiria nafasi ile na kujutia kwa kuipoteza.
“Siyo kitu kizuri kwa mshambuliaji, ni kitu ambacho kwa kweli kilinifanya nisipate usingizi usikuwa jana (juzi) nikijaribu kuikumbuka ile nafasi nikijaribu kuitafuta kuiangalia, kuirudia rudia nione ni wapi nilishindwa na kwa nini ilikuwa vile,”alisema Samatta aliyejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya DRC, ambayo nayo ilimnunua Simba SC ya nyumbani, Tanzania.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2x9Y2Uj
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms