• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2025 (243)
    • ►  Juli (2)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ►  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ►  November (405)
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ►  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (411)
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ▼  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ►  Oktober (535)
    • ▼  September (484)
      • Flamingo Park Monday 1 October 2018 Best Bets
      • MECHI YA MAHASIMU WA JADI, SIMBA NA YANGA YAMALIZI...
      • BALE ALIUMIA JANA REAL MADRID IKILAZIMISHWA SARE N...
      • CRISTIANO RONALDO JANA ALISETI MBILI JUVE IKIUA 3-...
      • JANA BARCA CHUPUCHUPU WAFIE CAMP NOU, SARE 1-1 A B...
      • NEYMAR ALIVYOFURAHI BAADA YA KUIPIGIA MBILI PSG JANA
      • ZAHERA AMSIMAMISHA MAKAMBO KAMA MSHAMBULIAJI PEKEE...
      • WEZI WAVAMIA MAKAO MAKUU YA KLABU YA LIPULI FC IRI...
      • KUELEKEA PAMBANO LA WATANI SAA 11:00 JIONI TAIFA; ...
      • CAF YAITHIBITISHA TANZANIA KUWA MWENYEJI WA FAINAL...
      • KOCHA MSAIDIZI AZAM FC, JUMA MWAMBUSI AWATAKA MARE...
      • KIKOSI CHA SIMBA SC MECHI NA WATANI HIKI HAPA; OKW...
      • KASEJA ASEMA KMC WANAELEKEZA NGUVU ZAO KWENYE MCHE...
      • KATWILA ASEMA MTIBWA SUGAR HAWADHARAU MECHI KWA SA...
      • MBEYA CITY WAPANIA KUMALIZIA HASIRA ZAO KWA STAND ...
      • NGOMA: NIMEFURAHI SANA KURUDI UWANJANI SASA SUBIRI...
      • MATOEKO YA MECHI ZOTE NA LIGI KUU SIMBA NA YANGA:
      • MBUNA, SMG, TASHI NA LUNYAMILA KABLA YA YANGA KUIP...
      • KAZI NJEMA JEONISYA RUKYAA, KUMBUKA SOKA NI SHERIA...
      • SAMATTA NI BALA, NA LEO AMAPIGA HAT TRICK TENA KRC...
      • LIVERPOOL YACHOMOA DAKIKA YA MWISHO, YAPATA SARE 1...
      • SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI ‘SIMBA DAMU’ MGENI RASMI...
      • ALLIANCE FC YAZINDUKA YAPATA USHINDI WA KWANZA LIG...
      • AGUERO AFUNGA LA PILI MAN CITY YAIKANDAMIZA BRIGHT...
      • OZIL AFUNGA ARSENAL YAICHAPA 2-0 WATFORD EMIRATES
      • POGBA ACHEZA, ATOLEWA MAN UNITED YAPIGWA 3-1 NA WE...
      • CALLUM SMITH ATWAA UBINGWA WA WB SERIES BAADA YA K...
      • POGBA AKIINGIA KAMBINI MAN UNITED TAYARI KUIVAA WE...
      • SPORTPESA WAMKABIDHI ABDALLAH SELEMAN ALLY WA MBAG...
      • Strong Dolphins batting day in Tshwane
      • NGOMA AANZA KAZI AZAM FC YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA ...
      • MBAO FC YAICHOMOLEA COASTAL MKWAKWANI NA KUREJEA K...
      • MASHABIKI WATAKAOHUDHURIA PAMBANO LA SIMBA NA YANG...
      • 5 things to look out for in the Premier League thi...
      • Gauteng Summer Cup 2018 - Ante-Post Betting
      • Hard-working day for Dolphins at SuperSport Park
      • MSUVA: NILITAKA KUPIGWA NA MASHABIKI ETI NAIHUJUMU...
      • HAJAWAHI KUTOKEA SIMBA NA YANGA TAMU KULIKO HIII L...
      • LIVERPOOL WAKIJIFUA KWENDA KULIPA KISASI KWA CHELS...
      • MBONDE AIPELEKA MTIBWA SUGAR KILELENI LIGI KUU, RU...
      • UJERUMANI WENYEJI WA EURO 2024, UTURUKI CHALI UEFA
      • YANGA SC KUENDELEA KUWAKOSA JUMA WOTE, ABDUL NA MA...
      • South Africa vs Zimbabwe: First ODI Preview
      • Italy - Genova 5/90 - Lucky Numbers
      • Italy - Firenze 5/90 - Lucky Numbers
      • Italy - Torino 5/90 - Lucky Numbers
      • AMUNIKE ‘AWAKAUSHIA’ NYONI NA KICHUYA TAIFA STARS,...
      • SAMATTA AIZUNGUMZIA MECHI YA SIMBA NA YANGA MOJA T...
      • Fighting start from the Dolphins on day one at Cen...
      • Asia Cup Final: India vs Bangladesh Preview
      • WEST HAM UNITED YAICHPA 8-0 MACCLESFIELD 8-0 KOMBE...
      • BARCELONA NAO HOI, WACHAPWA 2-1 LA LIGA NA LEGANES
      • REAL MADRID 'ROJO ROJO', WACHAPWA 3-0 NA SEVILLA L...
      • WELBECK AFUNGA MAWILI ARSENAL YASHINDA 3-1 KOMBE L...
      • HAZARD ATOKEA BENCHI KUIFUNGIA LA USHINDI CHELSEA ...
      • KOCHA MBELGIJI WA SIMBA SC ASEMA KWA NINI AMEKATAA...
      • SINGIDA UNITED WAZINDUKA, WAITANDIKA MBEYA CITY 3-...
      • Greyville Sunday 30 September 2018 Best Bets
      • Durbanville Saturday 29 September 2018 Best Bets
      • Turffontein Saturday 29 September 2018 Best Bets
      • Fairview Friday 28 September 2018 Best Bets
      • Greyville Friday 28 September 2018 Best Bets
      • HAJATOKEA KAMA ABDALLAH ‘KING’ KIBADENI MECHI ZA W...
      • Rugby Championship 2018: Argentina vs New Zealand ...
      • 2018 MTN8 Final: SuperSport United v Cape Town Cit...
      • Bakkie Selfie Competition: Terms and Conditions
      • KZN Cricket Union scoops Federation of the Year at...
      • JEONESIYA RUKYAA KUCHEZESHA MECHI YA MAHASIMU WA J...
      • EPL: Week Seven Preview
      • Pro14: Round 5 South African Matches Preview
      • Rugby Championship 2018: South Africa v Australia ...
      • EPL: Chelsea vs Liverpool Preview
      • GRIEZMANN AFUNGA ATLETICO MADRID YASHINDA 3-0 WANDA
      • F1 2017: Russian Grand Prix Preview
      • French Top 14: Clermont v Toulon Preview
      • English Premiership: Round 5 Preview
      • MOURINHO AMVUA UNAHODHA POGBA BAADA YA KUMUAMBIA A...
      • Pro14: Round 5 South African Matches Preview
      • Pro 14: Round 5 European Games Preview
      • Derby Knock Manchester United out of EFL Cup
      • The Ryder Cup: Comprehensive Preview
      • SIMBA SC KUINGIA KAMBINI LEO KUNDUCHI MAANDALIZI M...
      • MAN CITY WAVUKA KIKWAZO CHA KWANZA CARABAO, WASHIN...
      • MANCHESTER UNITED YATOLEWA MAPEMAA KOMBE LA LIGI E...
      • KMC YAENDELEA KUSUASUA LIGI KUU…NA LEO PIA WAMETOK...
      • PLUIJM AIWEKEA MKAKATI MZITO LIPULI, AWAAMBIA MAPE...
      • Italy - Cagliari 5/90 - Lucky Numbers
      • French Top 14: Stade Francais v Racing 92 Preview
      • Mitre 10 Cup: Auckland v Otago Preview
      • Mitre 10 Cup: Bay of Plenty v Manawatu Preview
      • Mitre 10 Cup 2018: Hawke's Bay v Northland Preview
      • Exciting season-opening Pretoria trip for Dolphins
      • #ChooseDay: Did Salah Deserve the Puskas Goal Award
      • Italy - Venezia 5/90 - Lucky Numbers
      • Italy - Nazionale 5/90 - Lucky Numbers
      • Opinion: Miller's white-ball focus a sign of drive...
      • Elgar Replaces injured Amla in ODI squad; Duminy t...
      • Bari 5/90 - Italy - Lucky Numbers
      • NYOTA REAL MADRID WAKIWA NA TUZO ZAO FIFA MAZOEZIN...
      • Turffontein Thursday 27 September 2018 Best Bets
    • ►  Agustus (487)
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ►  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ►  November (567)
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ►  Agustus (555)
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ►  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ►  November (509)
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE » KAZI NJEMA JEONISYA RUKYAA, KUMBUKA SOKA NI SHERIA 17 TU

KAZI NJEMA JEONISYA RUKYAA, KUMBUKA SOKA NI SHERIA 17 TU

KWA mara ya tatu, refa wa kike, Jeonisya Rukyaa kutoka Kagera atachezesha mpambano wa watani wa jadi wa soka ya Tanzania, Simba na Yanga leo jioni Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, huo ukiwa mchezo wa kwanza wa msimu wa Ligi Kuu ya Bara.
Jeonisya atasaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Mohamed Mkono wa Dar es Salaam pembezoni mwa Uwanja na Mezani atakuwepo Elly Sasii.
Hili si jina geni kwenye mechi za watani, kwani Jeonesia tayari ana uzoefu wa kupuliza kipyenga katika michezo ya watani wa jadi, baada ya awali kuchezesha mechi mbili.

Kwanza ilikuwa Desemba 13, mwaka 2014 mechi ya Mtani Jembe, Simba SC wakishinda 2-0, mabao ya Awadh Juma na Elias Maguri na ya pili Februari 20, mwaka 2016 Yanga SC wakishinda 2-0, mabao ya Donald Ngoma na Amissi Tambwe. 
Mechi iliyopita Aprili 29, mwaka huu ilichezeshwa na Emmanuel Mwandembwa wa Arusha aliyesaidiwa na Frank Komba wa Dar es Salaam na Mohammed Mkono wa Tanga, wakati refa wa akiba atakuwa Heri Sasii Simba ikashinda 1-0 bao pekee la Erasto Nyoni.
Mechi ya mzunguko wa kwanza ya Ligi Kuu msimu uliopita Oktoba 28, mwaka jana Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam ilichezeshwa na Heri Sasii timu hizo zikifunga bao 1-1.
Wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari wiki iliyopita kuitangaza mechi hiyo, Afisa Habari wa Yanga, Dissmass Ten aliasa mashabiki wasiende kuvunja viti akiwapiga vijembe watani, lakini Manara akajibu kwamba marefa nao wachezeshe kwa haki kuepusha hilo.
Hiyo ni kwa sababu athari nyingi za uwanjani wakati wa mechi za watani husababishwa na uchezeshaji mbovu wa marefa wetu, ama kwa bahati mbaya au kwa hila nyingine labda za kibinadamu piaa.  
Mwaka jana Manara aliwawekea Waandishi wa Habari video ya mchezo wa Oktoba 28 kuwaonyesha namna ambavyo refa Sasii hakutoa penalti licha ya mpira kuwagonga mikononi beki, Kevin Yondan na kiungo Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi Jumamosi.
Huo ulikuwa mwendelezo wa malalamiko dhidi ya marefa wa Tanzania kwenye mechi za watani wa jadi, ambao kwa hakika kwa asilimia kubwa wamekuwa hawaitendei haki mechi hiyo kwa uchezeshaji wao.
Rejea Oktoba 1, mwaka 2016, refa Martin Saanya aliyechezesha mechi ya watani hao wa jadi, alifungiwa miaka miwili kwa pamoja na Msaidizi wake, namba moja, Samuel Mpenzu kwa kuvurunda.
Na pamoja na kuwafungia waamuzi huo kwa makosa ya kutoa maamuzi ya utata, pia Kamati ya Masaa 72 ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilifuta Kadi nyekundu ya mchezaji Jonas Mkude baada ya kubaini hakufanya kosa.
Maamuzi ya utata ya Saanya yalisababisha vurugu Uwanja wa Taifa Jumamosi ya Oktoba 1, mwaka jana baada ya Yanga kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Tambwe alifunga bao hilo dakika ya 26, akimalizia pasi ndefu ya beki Mbuyu Twite na kugeuka mbele ya beki wa Simba, Novat Lufunga kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Vincent Angban.
Bao hilo lilizua kizaazaa, wachezaji wa Simba wakimvaa refa Martin Saanya wakidai mfungaji, Tambwe aliushika mpira kabla ya kufunga. Na katika vurugu hizo, Saanya alimtoa kwa kadi nyekundu Nahodha wa Simba SC, Jonas Mkude dakika ya 29 kwa sababu ndiye aliyekuwa mstari wa mbele.
Kwa hali hiyo, mchezo ukasimama kwa takriban dakika tano baada ya mashabiki wa Simba kuanza kufanya vurugu waking’oa viti na kutupa uwanjani. Polisi walitumia milipuko ya gesi za kutoa machozi kuwatuliza mashabiki hao na mchezo ukaendelea hadi Simba SC wakasawazisha dakika ya 87 kwa bao la Shizza Kichuya.
Awali, Mpenzu alikataa bao safi la Simba lililofungwa na Ibrahim Ajib mapema kipindi cha kwanza akidai aliotea.
Mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu baina ya miamba hiyo ulichezeshwa na refa Mathew Akrama kutoka Mwanza Februari 25, mwaka huu pale pale Taifa na winga Shiza Ramadhani Kichuya, kwa mara nyingine aliibuka shujaa wa Simba baada ya kutokea benchi na kuisaidia timu yake kushinda 2-1.
Kichuya aliyempokea beki Novatus Lufunga dakika ya 55, kwanza alimsetia mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo kuifungia bao la kusawazisha Simba dakika ya 66 kabla ya yeye mwenyewe kufunga la ushindi dakika ya 81.
Kama Oktoba 1, na Februari 25 Yanga SC walitangulia kwa bao la mapema tu dakika ya tano la Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti, baada ya kiungo Mzambia, Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi na Lufunga.
Akrama alimtoa nje kwa kadi nyekundu beki Mkongo wa Simba, Janvier Besala Bokungu dakika ya 55 baada ya kumuonyesha kadi ya pili ya njano kufuatia kumchezea rafu Chirwa.
Akrama alikuwa mwiba kwa timu zote mbili siku hiyo kutokana na maamuzi yake ya kufuata sheria 17 za soka bila kusita pale tu lilipotokea kosa, hali ambayo ilisababisha wachezaji wenyewe waamue kuwa na nidhamu uwanjani.
Na kazi nzuri ya Akrama Oktoba 1 ilikuwa sawa na kusahihisha makosa yake ya Oktoba 3, mwaka 2012 alipochezesha kwa mara ya kwanza mechi ya watani hao wa jadi, ikiwa ya Ligi Kuu pia timu hizo zikitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa. 
Katika mchezo huo ulioanza Saa 1:02 usiku, Akrama alimtoa kwa kadi nyekundu winga Simon Msuva wa Yanga dakika ya 77 kwa kumrudishia rafu beki wa Simba, Juma Nyosso.
Siku hiyo, Simba ndiyo walitangulia kwa bao la kiungo Amri Kiemba dakika ya pili, kabla ya mshambuliaji Said Bahanuzi kuisawazishia Yanga dakika ya 63 kwa penalti baada ya beki Paul Ngalema kuunawa mpira kwenye boksi.
Lakini Akrama alilaumiwa kwa kumuonyesha kadi ya njano badala ya nyekundu kiungo wa Simba, Haruna Moshi ‘Boban’ licha ya kumchezea rafu mbaya beki wa Yanga, Kevin Yondan hadi akashindwa kuendelea na mchezo, na nafasi yake ikachukuliwa na Juma Abdul.
Na pia alilaumiwa kuwa kutomchukulia hatua yoyote kipa Juma Kaseja aliyeonekana kupoteza muda tangu mwanzo, na alimpa onyo tu zaidi ya mara tatu.
Haikuwa ajabu Oktoba 6 Akrama alipoondolewa kwenye orodha ya wamuzi wa kuchezeaha Ligi Kuu baada ya kuvurunda mechi hiyo namba 80, huku aliyekuwa mshika kibendera namba mbili, Ephrony Ndissa wa Dar es Salaam akipewa onyo.
Lakini bado kazi nzuri ya Akrama Februari 25 haiwezi kunibadilisha msimamo wangu wa muda mrefu wa kutaka mechi za watani hawa wa jadi zichezeshwe na marefa wa nje – ila kwa kuwa wenye mamlaka, TFF na Bodi ya Ligi hawajaona umuhimu wa hilo chochote nitakachoandika kitakuwa sawa na kelele za chura, hazitamzuia ng’ombe kunywa maji. 
Lakini ukweli unabaki pale pale, marefa wetu wamesababisha adha kubwa kwenye mechi za watani, achilia mbali za Oktoba 1, mwaka jana kuna matukio mengine makubwa ya kihistoria yamewahi kutokea na kuhatarisha hata maisha ya viongozi wetu wakubwa wa nchi.
Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi alinusurika katika tukio la hatari Machi 31, mwaka 2002 katika fainali ya Kombe la Tusker, Simba ikishinda 4-1.
Siku hiyo refa Abdulkadir Omar ‘Msomali’ aliivuruga mechi na kuhatarisha amani uwanjani pia kwa madudu yake.
Mechi hiyo ya fainali ambayo Alhaj Mwinyi maarufu kama Mzee Ruksa alikuwa mgeni rasi – chupuchupu  ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka Suleiman kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. 
Rais wa Yanga wakati huo, Tarimba Abbas aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na FFU ndipo akaendeleza mchezo. 
Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. Baada ya hapo, alifungiwa na Chama cha Soka Tanzania, (FAT), sasa TFF kabla ya kujiuzulu uongozi wa klabu hiyo baadaye.
Ni marefa wachache sana wamewahi kuziongoza vizuri mechi za Simba na Yanga na zikamalizika bila manung’uniko, akiwemo mwanamama mwenye beji ya FIFA, Donisya Rukyaa wa Kagera anayefuata nyayo za marefa wakongwe kama Nassor Hamdoun wa Kigoma.
Tathmini mbalimbali za kitaalamu za vyombo vya habari vya kimataifa zimekwishaipitisha mechi ya Simba na Yanga kama moja ya mechi kubwa mno za watani wa jadi Afrika.
Tatizo kubwa ni marefa, kweli ilipofikia na kama kweli lengo ni kuiongezea msisimko zaidi mechi ya watani, waamuzi wa Tanzania wawekwe kando na watumike waamuzi kutoka nje ya nchi, tena ikibidi nje kabisa ya nchi tatu za Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.
Rejea hata mchezo wa Machi 5, mwaka 2011 Uwanja wa Taifa, refa Orden Mbaga aliivuruga mno mechi hiyo, kutokana tu na pengine mchecheto ama kutaka kufanya kile ambacho kinaitwa ‘kubalansi’ mchezo au kukwepa lawama, matokeo yake akafanya madudu.
Dakika ya 58 Juma Said Nyosso alimkwatua Mzambia Davies Robby Mwape kwenye eneo la hatari akawapa penalti Yanga na kilichofuatia wengi walijua beki huyo wa Simba atatolewa nje kwa kadi nyekundu, badala yake akampa kadi ya njano.
Ngumu kuamini Mbaga, refa mwenye beji ya Shrikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) hajui alipaswa kufanya nini kwa Nyosso, lakini kwa sababu ni refa wa nyumbani na aliongoza wapinzani wa jadi katika mechi ya nyumbani, alihofia kumtoa mchezaji kwa kadi nyekundu angeshushiwa lawama nzito. Marefa hufanyiwa fujo na kupigwa na mashabiki, labda alihofia hali hiyo pia.
Dakika ya 73 Simba walipata bao safi la kusawazisha lililofungwa kwa kichwa na Mussa Hassan Mgosi, aliyeuwahi mpira uliotemwa na kipa Mghana Yaw Berko kufuatia shuti la mpira wa adhabu, lililogonga mwamba wa juu na kudondokea nyavuni kabla ya kuokolewa na mabeki wa Yanga.
Halikuwa bao lenye shaka yoyote, hakukuwa na kuotea wala dosari yoyote, lakini haieleweki kwa nini Mbaga alilikataa bao hilo awali.
Ilikuwa offside au mpira haukutinga nyavuni hadi akalikataa kwanza? Haijulikani, lakini alilikubali baada ya wachezaji wa Simba kumuambia aangalie kwenye TV kubwa iliyopo uwanjani marudio ya tukio lile na baada ya hapo akaenda kujadiliana na msaidizi wake, ndipo akalikubali.
Tujiulize, kusingekuwa na ile TV, Simba wangedhulumiwa bao lao? Mbaga alichemsha- lakini si Mbaga tu, marefa wengi wa Tanzania waliwahi kutokota kabla yake na nitakumbushia baadhi ya mechi.   
Agosti 18, mwaka 2002 Simba na Yanga zikitoka sare ya 1-1 katika mechi ya Ligi Kuu, refa Victor Mwandike aliwaacha mashabiki wa Simba midomo wazi kwa kuwapa Yanga penalti ya utata dakika ya 89 na ushei, ambayo Sekilojo Chambua aliitumia vema kuisawazishia bao timu yake, baada ya Simba kutangulia kufunga kupitia kwa Madaraka Suleiman dakika ya 65.
Oktoba 24, mwaka 2007, refa Osman Kazi alikataa mabao matatu yaliyofungwa na Yanga, yote akidai kipa Juma Kaseja alisukumwa na wachezaji wa Yanga, lakini kwa yeyote atakayerudia kuangalia DVD ya mchezo ule, hawezi kuona ukweli wa madai ya Kazi.
Awali ya hapo, Kazi aliwahi kupuliza filimbi ya kumaliza dakika 45 za kipindi cha kwanza katika Nusu Fainali ya Kombe la Tusker mwaka 2005 mjini Mwanza, wakati mchezaji wa Yanga, Said Maulid ‘SMG’ amekwishawatoka mabeki wa Simba na anakwenda na mpira mbele yake amebaki Juma Kaseja tu.
Refa ni mwamuzi wa mwisho- lakini kwa wana Yanga walijutia mno tukio lile kwenye mchezo ambao mwishowe walifungwa 2-0, kwa mabao ya kipindi cha pili ya Emmanuel Gabriel na Mussa Mgosi.
Aprili 19, mwaka 2009, Jerry Tegete aliifungia Yanga bao la kusawazisha kwa mkono na kutengeneza sare ya 2-2, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Refa makini asingeweza kukubali bao lile, hivyo kwa haya yote lazima tukubali marefa wa Tanzania hawawezi tena kuchezesha mechi za watani wa jadi.
Sababu nyingine za marefa wetu kuzishindwa mechi hizo ni hiyo ya mapenzi yao kwa moja ya timu hizo, kitu ambacho Misri wamekiepuka na mechi ya Zamalek na Ahly inachezeshwa na marefa kutoka nje ya nchi yao.
Nakumbuka refa kutoka Uganda, Dennis Bate aliyechezesha fainali ya mwisho ya Kombe la Tusker mwaka 2009 kati ya Simba na Yanga, aliiongoza vizuri mechi hiyo na akadhibiti ujanja wote wa wachezaji kutaka kumdanganya na hatimaye aboronge.
Kuna wachezaji wanaitwa wazoefu wa mechi za Simba na Yanga na hawa wamekuwa wakiwapoteza sana marefa kwa uzoefu wa kucheza mechi hizo, lakini kama marefa watatoka nje ya Tanzania, tena wa kiwango cha beji za FIFA, uhondo wa mechi za watani utaongezeka maradufu. 
Nitaendelea kuamini hivyo, nitaendelea kuliandikia hilo hadi siku viongozi wetu watakapoondoa nta masikioni mwao. Pamoja na yote niwatakie kila la heri na kazi njema marefa wa leo, wakiongozwa na mwanamama Jeonisya Rukyaa – tu wakumbuke sheria 17 na kauli mbiu kuu ya FIFA, kuchezesha kwa haki, wajue wakipindisha maamuzi yao watahatarisha amani uwanjani. 


from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2Na0XCA best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang KAZI NJEMA JEONISYA RUKYAA, KUMBUKA SOKA NI SHERIA 17 TU. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2018/09/kazi-njema-jeonisya-rukyaa-kumbuka-soka.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 19.31
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    VIUNGO, Muivory Coast Aubin Kramo Kouamé (kushoto) na José Luis Miquissone wa Msumbiji wakiwa kwenye mazoezi ya Simba leo Uwanja wa Mo Si...
  • Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Stand a chance to win your share of R100 000 cash! Play R5 or more using your Hollywoodbets account on the selected Lucky Numbers draws an...
  • Lucky Numbers Draw Times & Results
    Lucky Numbers Draw Times & Results
    All the information you need for the 501 Lotto draws offered by Hollywoodbets for Lucky Numbers and Powa Numbas betting! Get closing times...
  • MOHAMED SALAH ANAVYOFURAHIA MAISHA LIVERPOOL
    Kiungo Mohamed Salah akifurahia kwenye mazoezi ya Liverpool leo Uwanja wa  Melwood kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England ...
  • Bafana held by Nigeria in AFCON Qualifier
    Bafana held by Nigeria in AFCON Qualifier
    Bafana Bafana moved one step closer to the 2019 Africa Cup of Nations with a point in their 1-1 draw with Nigeria at the FNB Stadium on Sa...
  • TUZO ZA LIGI KUU ZABORESHWA, SASA WACHEZAJI KUPEWA NA KING'AMUZI CHA AZAM TV
    Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB) Boniface Wambura, akionyesha tuzo atakayokuwa akipewa Mchezaji bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Vod...
  • Winning Form Promotion - Jockey Trainer Combo
    Winning Form Promotion - Jockey Trainer Combo
    You could win a R200 Hollywoodbets betting voucher. Simply comment on the competition post who is your favourite jockey, trainer combo of ...
  • PGA Tour: The Sony Open Preview
    We take a look at the Sony Open set to take place between 11 January and 14 January at the Waialae Country Club.  With news of Tiger Woods...
  • UK Racing Best Bets - Saturday 28 September 2019
    UK Racing Best Bets - Saturday 28 September 2019
    Neil Morrice walks you through the front runners for Saturday's feature races at Cambridgeshire, Newmarket and the Cheveley Park Stake...
  • Spanish La Liga: Week 27 Preview
    Our football writer previews matchday 27 of the 2016/17 Spanish La Liga campaign. The title race in La Liga is looking ever-so-tight wit...
Copyright Viral Sports: KAZI NJEMA JEONISYA RUKYAA, KUMBUKA SOKA NI SHERIA 17 TU