Na Mwandishi Wetu, IRINGA
OFISI za klabu ya Lipuli FC mjini Iringa zimevamiwa na watu wasiojulikana ambao wameiba jezi zote za timu hiyo zilizotengwa maalum kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation (ASFC).
Taarifa ya Lipuli FC kwa vyombo vya Habari leo imesema kwamba wezi hao walifanikiwa kuingia kwenye ofisi za klabu baada ya kuvunja kufuli la mlango wa ofisi kwa kutumia nondo.
“Kumetokea tukio la wizi katika ofisini zetu za klabu ya Lipuli Fc usiku wa kuamkia leo na kufanikiwa kuiba jezi zote za FA CUP pamoja na mavazi ya kusafiria. Wezi hao wamevunja kufuli la mlango wa ofisi kwa kutumia nondo,” imesema taarifa hiyo.
Uongozi wa Lipuli umesema kwamba Sekretarieti ya klabu imechukua hatua muhimu ya kuripoti tukio hilo kwa vyombo vya usalama, kwa maana ya jeshi la Polisi na kupewa taarifa ya tukio, ijulikanayo kama RB namba 6605/20/8.
Wezi hao walitumia mwanya wa uongozi wa klabu kuwa na timu mjini Dar es Salaam ambako juzi walicheza mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania na kupata sare ya 0-0 na wenyeji, Azam FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2Qk6nN3
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms