Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KOCHA Mnigeria wa Tanzania, Emmanuel Amunike hajawajumuisha beki Erasto Nyoni na winga Shiza Kichuya katika kikosi chake cha wachezaji 30 kuelekea mechi mbili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Cape Verde.
Taifa Stars watakuwa wageni wa Cape Verde katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON Oktoba 12 mjini Praia kabla ya kurejea Dar es Salaa kwa mchezo wa marudiano na wapinzani wao hao Oktoba 16.
Na Amunike leo ametaja kikosi cha awali cha wachezaji 30 kwa ajili ya mechi hizo, akiwaweka kando nyota kadhaa, wakiwemo Nyoni na Kichuya.
|
Shiza Kichuya (kulia) amekuwa mchezaji muhimu wa Taifa Stars kabla ya ujio wa Emmanuel Amunike |
Kwa kiasi kikubwa ameita wachezaji waliomsaidia kupata sare ya ugenini Septemba 8 mjini Kampala na Uganda, ingizo jipya wakiwa ni mabeki Shomari Kapombe wa Simba SC, Abdallah Kheri wa Azam FC, Andrew Vicent na kiungo Feisal Salum wote wa Yanga SC.
Kikosi kamili cha Taifa Stars kilichotajwa leo ni makipa; Aishi Manula (Simba SC), Beno Kakolanya (Yanga SC) na Mohamed Abdulahman (JKT Tanzania).
Mabeki; Hassan Kessy (Nkana FC/Zambia), Shomari Kapombe (Simba SC), Salum Kimenya (Tanzania Prisons), Gardiel Michael (Yanga SC), Paulo Ngalema (Lipuli FC), Ally Sonso (Lipuli FC), Aggrey Morris (Azam FC), David Mwantika (Azam FC), Abdallah Kheri (Azam FC), Kelvin Yondani (Yanga SC), Andrew Vicent (Yanga SC) na Abdi Banda (Baroka FC).
Viungo ni Himid Mao (Petrojet/Misri), Simon Msuva (Difaa Hassan El –Jadida/Morocco), Mudathir Yahya (Yanga SC), Frank Domayo (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Feisal Salum (Yanga SC), Salum Kihimbwa (Mtibwa Sugar) na Farid Mussa (CD Tenerife/Hispania).
Washambuliaji; Mbwana Samatta (Nahodha, KRC Genk/Ubelgiji), Thomas Ulimwemgu (Al Hilal/Sudan), John Bocco (Simba SC), Yahya Zayd (Azam), Kelvin Sabato (Mtibwa Sugar), Rashid Mandawa (BDF XI/Botswana) na Shaaban Iddi Chilunda (CD Tenerife/Hispania).
Tanzania inashika nafasi ya tatu katika Kundi L ikiwa na pointi mbili tu baada ya sare zote katika mechi zake mbili za mwanzo, 1-1 na Lesotho nyumbani mwaka jana na 0-0 na Uganda ugenini mapema mwezi huu.
Uganda wanaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi zao nne, wakifuatiwa na Lesotho mbili sawa na Tanzania na mabao mawili ya kufunga, wakati Cape Verde wanashika mkia kwa pointi yao moja.
Kihistoria Tanzania imecheza fainali moja tu za AFCON, mwaka 1980 nchini Nigeria, tena enzi hizo bado zinajulikana kama Fainali za kombe la Mataifa Huru ya Afrika.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2xU2g2P
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms