Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KESI inayowakabili vigogo wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), aliyekuwa Rais Jamal Malinzi na wenzake wane imeahirishwa hadi Desemba 5, mwaka huu kutokana na Wakili wa Serikali, Leonard Swai anayeendesha shauri hilo kuwa na shughuli nyingine za kiofisi.
Washitakiwa wote walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, wakati shauri lilipotajwa kwa ajili ya kuendelea na ushaidi upande wa mashitaka.
Wakili wa Serikali Pendo Temu, aliomba mahakama tarehe nyingine ya kutajwa kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji upande wa mashitaka.
"Naiomba mahakama kuahirisha shauri hilo kwani Wakili Swai amekuwa na shughuli nyingine za kiofisi," alidai.
Baada ya hoja hiyo, Wakili wa utetezi Richard Rweyongeza, alikubaliana na ombi hilo ambapo aliomba mahakama shauri hilo lipangiwe tarehe ya karibu hata kama iwe leo.
Hakimu Mashauri alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 5, mwaka huu kwa kuendelea ambapo washitakiwa walirudishwa rumande.
Mbali na aliyekuwa rais TFF, Jamal Malinzi(57) wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo Mwanga(27).
Meneja wa Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao Kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017 yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa fedha wa USD 173,335 na sh. 43,100,000.
Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wapo rumande kwa kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji wa fedha kuwa miongoni mwa mashtaka ambayo kwa mujibu wa sheria hayana dhamana huku wenzao Miriam na Flora wapo nje kwa dhamana.
Katika kesi hiyo tayari mashahidi wanane wa upande wa mashitaka wamekwishatoa ushahidi kwenye kesi hiyo.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2Fzl1zJ
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms