Na Mwandishi Wetu, LIEGE
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Saamtta usiku wa jana amefunga bao moja, timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Standard Liege katika mchezo wa hatua ya pili ya Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege.
Samatta alifunga bao la pili dakika ya 53 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Ruslan Malinovskiy, kufuatia kiungo Bryan Heynen kufunga la kwanza dakika ya 42 akimalizia pasi ya mshambuliaji, Mbelgiji mwenzake, mshambuliaji Leandro Trossard.
Bao la tatu la KRC Genk lilifungwa na Trossard dakika ya 80 safari hiyo naye akisetiwa na Heynen, wakati bao pekee la Standard Liege lilifungwa na kiungo Mromania, Razvan Gabriel Marin dakika ya 82 akimalizia pasi ya kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Merveille Bope Bokadi.
Kipa Mmexico wa Standard Liege, Guillermo Ochoa akiwa amedaka mbele ya Mbwana Samatta wa KRC Genk jana
Kwa ushindi huo wa nne katika mechi tano ikiwa imepoteza mchezo mmoja wa Championship Round baada ya kuongoza vizuri hatua ya kwanza ya ligi hiyo ijulikanayo kama Regular Season, Genk inajoongezea nafasi ya kutwaa ubingwa huku Samatta akizidi kukikaribia kiatu cha dhahabu baada ya kufunga bao la 22 la msimu.
Kwa ujumla Samatta mwenye umri wa miaka 26, usiku huu ameifungia bao la 61 Genk akicheza mechi yake ya 151 kwenye mashindano tangu amejiunga nayo Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 118 sasa na kufunga mabao 46 na kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi tisa na kufunga mabao mawili na Europa League amecheza mechi 24 na kufunga mabao 14.
Kikosi cha Standard Liege kilikuwa; Ochoa, Vanheusden, Kosanovic, Cimirot, Carcela, Halilovic/Lestienne dk76, Marin, Djenepo, Fai, Laifis na Mpoku/Bokadi dk76.
KRC Genk; Vukovic, Uronen, Lucumi, Dewaest, Maehle, Heynen, Berge, Malinovskyi/Wouters dk86, Ito, Trossard/Ndongala dk87 na Samatta.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2Iuvw7X
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms