Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BEKI anayecheza nafasi zote za ulinzi na kiungo, Shomari Kapombe jana aliumia mazoezini kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Uwanja wa Taifa Dar es Salaam inayojiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zikazofanyika baadaye mwezi huu nchini Misri.
Kapombe, beki wa Simba SC ni miongoni mwa wachezaji 39 walioitwa kwenye kikosi cha awali cha Taifa Stars kilichoingia kambini juzi hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam kwa maandalizi ya awali ya AFCON kabla ya kikosi kwenda Alexandria Juni 7.
Kapombe ameitwa Taifa Stars akitoka kuwa nje kwa zaidi ya miezi saba akiuguza majareha aliyoyapata mwezi Novemba mwaka jana nchini Afrika Kusini alipokuwa mazoezini pia na kikosi cha timu ya taifa kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON dhidi ya Lesotho.
Pole; Shomari Kapombe yuko hatarini kuzikosa Fainali za AFCON baada ya kuumia mazoezini Taifa Stars
Kocha Emmanuel Amunike aliamua kumjumuisha katika kikosi hicho cha awali kilichotangaza mwezi Mei mwaka huu, baada ya mchezaji huyo kupona majeraha yake na kuanza mazoezi tayari kwa kurudi dimbani licha ya klabu yake ya Simba kutomtumia katika mechi za mwisho za Ligi Kuu Tanzania Bara.Leo Afisa Habari wa TFF Cliford Ndimbo amethibitisha kuwa mchezaji huyo amejitonesha majeraha hayo wakati akiendelea na mazoezi katika kambi ya Taifa Stars iliyoanza rasmi Juni 01, 2019 kwenye Hoteli ya White Sands hivyo kwa sasa anasubiri hatma yake kwenye kikosi cha mwisho kitakachotajwa hivi karibuni.
“Shomari Kapombe amejitonesha wakati akiendelea na programu ya timu ya taifa hivyo kwasasa hayuko na wenzake lakini anaendelea kufuatilia programu ya mazoezi mpaka hapo mwalimu atakapotaja kikosi cha mwisho”, amesema Ndimbo.
Taifa Stars itaondoka na wachezaji 32 kwenda kambini mjini Alexandria, Misri baada ya kuchujwa saba na kati ya hao ni 23 tu watashiriki AFCON.
Wachezaji wengine wataendelea kubaki kambini kwa maandalizi ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Kikosi cha kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kitaanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wa AFCON, Misri Juni 13, mwaka huu Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.
Baada ya hapo Taifa Stars itacheza mechi zake tatu za Kundi C mfululizo ikianza na Senegal Juni 23, Kenya Juni 27 na kumaliza na Algeria Julai 1 kuangalia matokeo yake kama yataipeleka hatua ya mtoano.
Kikosi kilichoingia kambini leo kinaundwa na makipa; Aishi Manula (Simba SC), Metacha Mnata (Mbao FC), Suleiman Salula (Malindi SC) na Aaron Lulambo (Tanzania Prisons).
Mabeki; Claryo Boniface (U20), Hassan Kessu (Nkana FC, Zambia), Vincent Philipo (Mbao FC), Shomari Kapombe, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni (Simba SC), Kelvin Yondan, Gardiel Michael (Yanga SC), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Ally Ally (KMC) na Kennedy Wilson (Singida United).
Viungo ni Feisal Salum, Ibrahim Ajibu (Yanga SC), Jonas Mkude (Simba SC), Shiza Kichuya (ENNPI, Misri), Simon Msuva (Difaa Hassan El-Jadidi Morocco) na Farid Mussa (Tenerife, Hispania).
Washambuliaji ni Yahya Zayd (Ismailia, Misri), Shaaban Iddi Chilunda (Tenerife, Hispania), Rashid Mandawa (BDF, Botswana), Ayoub Lyanga (Coastal Union), Kassim Khamis (Kagera Sugar), Kelvin John (Serengeti Boys), Adi Yussuf (Solihull Moors, England), John Bocco (Simba SC), Thomas Ulimwengu (JS Saoura, ALgeria) na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji).
Wachezaji wengine beki Ally Mtoni, kiungo Freddy Tangalu wa Lipuli FC na mshambuliaji Miraj Athumani ‘Madenge’ wa Lipuli FC, mabeki David Mwantika, Aggrey Morris, viungo Frank Domayo na Mudathir Yahya wa Azam FC watajiunga na wenzao kesho baada ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mbali na Taifa Stars kupangwa Kundi C AFCON 2019 pamoja na jirani zao, Kenya, Algeria na Senegal – wenyeji, Misri wapo Kundi A pamoja na na Zimbabwe, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kundi B linaundwa na Burundi, Madagascar, Guinea na Nigeria, Kundi D linaundwa na Namibia, Afrika Kusini, Ivory Coast na Morocco, wakati Kundi E kuna Angola, Mauritania, Mali na Tunisia na Kundi F ni Guinea Bessau, Benin, Ghana na mabingwa watetezi, Cameroon.
Taifa Stars imefuzu AFCON ya mwaka huu baada ya kumaliza nafasi ya pili kwenye Kundi L kwa pointi zake nane, nyuma ya jirani zao wa Afrika Mashariki, Uganda walioongoza kwa pointi zao 13 wakizipiku Lesotho iliyomaliza na pointi sita na Cape Verde pointi tano.
Mwaka huu, Tanzania itashiriki AFCON kwa mara ya pili tu kihistoria baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria ambako ilipangwa Kundi A pamoja na wenyeji, Nigeria, Misri na Ivory Coast na kushika mkia.
Mwaka 1980 ilifungwa mechi mbili, 3-1 na Nigeria na 2-1 na Misri kabla ya kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast na kuishia Raundi ya kwanza tu, wakati timu nane tu zinashiriki michuano hiyo.
Michuano itaanza Juni 21 hadi Julai 19 na Taifa Stars itachezea mechi zake Uwanja wa Juni 30 na Al Salam mjini Cairo.
Na katika CHAN, Taifa Stars itaanzia nyumbani dhidi ya Sudan Julai 26 kabla ya kurudiana Agosti 2 na ikifuzu mtihani huo itamenyana na mshindi kati ya Kenya na Burundi.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://bit.ly/2WC2dqT
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms