Na Somoe Ng'itu, TUNIS
TIMU ya Soka ya Taifa ya Wanawake ( Twiga Stars) imeendelea kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la UNAF baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Algeria katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Kram jijini Tunis nchini hapa.
Kwa ushindi huo, Twiga Stars imefikisha pointi sita na kuongoza katika msimamo wa mashindano hayo yanayoshirikisha nchi tano za Kanda ya Kaskazini na Tanzania wakiwa wageni waalikwa.
Bao la kwanza la Twiga Stars lilifungwa na Mwanahamisi Omary "Gaucho" katika dakika ya 11 na dakika ya 22 Algeria walisawazisha kupia Dellidj Anissa.
Dakika ya 44 Affak Horiya aliifungia Algeria bao la pili na sekunde chache kabla ya kwenda mapumziko, Gaucho, mshambuliaji wa Simba Queens aliisawazishia Twiga Stars kwa kufunga bao la pili.
Diana Msewa aliwanyanyua mashabiki wa Twiga Stars baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya lala salama na kuipa timu yake pointi tatu muhimu.
Kocha wa Twiga Stars, Bakari Shime amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana kusaka ushindi katika mchezo huo wa pili mfululizo.
"Kila timu inavyocheza inazidi kuimarika, kuna makosa yapo tumeyabaini, tutayarekebisha kwa ajili ya mechi inayofuata, tunaendelea kujifunza na kuwapa uzoefu wachezaji wetu kupitia michuano kama hii, inawaimarisha kwa ajili ya mechi za mashindano," alisema Shime.
Twiga Stars itashuka tena dimbani kesho kucheza dhidi ya Morocco ambayo nayo iliwafunga Tunisia katika mchezo wa kwanza na itamaliza dhidi ya wenyeji hao Februari 22, mwaka huu.
Jana jioni Tunisia ilishuka dimbani kuwakaribisha Mauritania, timu zote zikiwa na kumbukumbu ya kufungwa katika mechi zao za kwanza.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2vABeju
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms