Na Shamimu Nyaki –WHUSM, DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema kuwa katika uongozi wake atahakikisha heshima ya michezo hapa nchini inarejea.
Bashungwa ameyasema hayo jana Jijini Dar es Salaam ambapo alifanya kikao na makocha pamoja na wanamichezo wa zamani na ameeleza kuwa Serikali imeanza kutenga fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Michezo.
"Lengo la kikao hiki ni kupokea mawazo kutoka kwenu namna bora ya kuendesha michezo ili tupate mafanikio kama ambayo tulipata hapo zamani wakati nyie mkilitumikia taifa letu katika soka" alisema, Waziri Bashungwa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa akisalimiana na mmoja wa mchezaji wa zamani baada ya kikao na Wachezajia pamoja na Makocha wa zamani kuhusu maendelo ya michezo nchini
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa (katikati), Naibu Waziri Abdallah Ulega wakiwa katika picha ya pamoja na Wachezaji pamoja na Makocha wa zamani baada ya kikao hicho
Bashungwa ameongeza kuwa marekebisho yaliyofanywa katika Sheria za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya mwaka 1967 kuhusu michezo ya ridhaa na kulipwa, Kwa hivi sasa inatambua michezo ya kulipwa ambapo kuna wachezaji zaidi ya 2000 wanaocheza michezo ya kulipwa ndani ya nchi na wanamichezo takriban 28 wanacheza michezo ya kulipwa nje ya nchi.
Aidha, Waziri Bashungwa amewapongeza wachezaji wa zamani kwa jinsi walivyojituma kwa nidhamu na moyo wa kizalendo kuipigania nchi na kufanikiwa kufuzu katika mashindano ya AFCON mwaka 1979.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara hiyo Abdallah Ulega ameiagiza Idara ya Michezo kusimamia maazimio yote ya kikao hicho kufanyiwa kazi na matokeo yaonekane.
"Nia yetu ni kuendeleza michezo, na hili tutalisimamia vyema hivyo tunaomba mawazo mazuri kutoka kwenu namna ya kuendeleza michezo" alisema Ulega.
Ulega ameongeza kuwa dhamira ya vikao na wadau wa michezo ni kutathmini michezo ilipotoka, ilipo na wapi ielekee kwa maslahi ya taifa.
Naye kiungo wa zamani wa Yanga na timu ya taifa, Ally Mayai Tembele ameishukuru Serikali kwa kuandaa vikao vya kukutana na wadau kupokea mawazo kuhusu maendeleo ya michezo nchini, huku akieleza kuwa michezo inahitaji nidhamu na kuwekeza kwa Watoto wa shule za msingi na sekondari, vifaa vya michezo na miundombinu bora ya michezo.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/3hpAAsZ
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms