Na Mwandishi Wetu, MBEYA
VINARA, Yanga SC wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na wenyeji, Mbeya City jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Ilibaki kidogo tu Yanga inayofundishwa na kocha Mrundi, Cedric Kaze kuondoka na ushindi kamam kama Mbeya City kusawazisha kwa penalti dakika ya 90 na ushei.
Refa Ludovick Charles aliwapa penalti Mbeya City dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimia dakika 90 kufuatia kushauriana na msaidizi wake namba mmoja, Ferdinand Chacha, wote wa Mwanza wote wakijiridhisha beki wa Yanga, Yassin Mustapha aliunawa mpira kwenye boksi.
Na mshambuliaji Pastory Athanas akaenda kuisawazishia Mbeya City kwa mkwaju mzuri wa penalti uliompita kipa, Metacha Boniphace Mnata.
Wachezaji wa Yanga SC waliwafuata marefa kuwazonga baada ya mchezo huo kabla ya kuzuiwa na viongozi wao akiwemo kocha Msaidizi, Nizar Khalfan.
Dakika 45 za kwanza za mchezo huo zilimalizika kwa timu hizo kutofungana na kipindi cha pili zikiwa zimesalia dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho, mtokea benchi Deus Kaseke akaifungia Yanga SC bao la kuongoza.
Zilikuwa ni juhudi binafasi za Kaseke aliyepasua katikati ya mabeki wa Mbeya City kabla ya kufumua shuti ambalo mabeki wa wenyeji walijaribu kuokolea ndani, lakini refa Ludovick Charles akawa makini.
Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; Haroun Mandanda, Kenneth Kunambi, Mpoki Mwakinyuki, David Mwasa, Babilas Chitembe, Edgar Mbembela, Pastory Athanas, Mathew Robert, Jean Didier/Abasarim Chidiebere dk88, Hamisi Thabit/Herbet Lukindo dk76 na Kato Yayo/Juma Shamvuni dk59.
Yanga SC; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong, Fiston Abdul Razak/Ditram Nchimbi dk74 na Farid Mussa/Deus Kaseke dk67.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/37b6Lsq
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms