NYOTA wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki wa Yanga usiku wa jana ameshinda Tuzo nne ikiwemo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu uliopita.
Katika Hafla ya utoaji wa Tuzo kwa wachezaji, Maafisa na timu zilizofanya vizuri msimu uliopita wa kabumbu nchini zilizofanyika ukumbi wa The Super Dome, Masaki Jijini Dar es Salaam, Aziz Ki pia alishinda Tuzo za Kiungo Bora, Mfungaji Bora na Kikosi Bora cha wachezaji 11.
Katika Tuzo ya Mchezaji Bora aliwapiku makipa; Djigui Diarra (Yanga), Leyi Matampi (Coastal Union), mabeki Ibrahim Abdallah Hamad 'Bacca' (Yanga), Kouassi Attohoula Yao (Yanga), Mohammed Hussein 'Tshabalala' (Simba) na viungo Kipré Junior Jr na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ wote wa Azam FC.
Katika Tuzo ya Kiungo Bora Aziz Ki aliwashinda Feisal na Kipre Junior, wakati kwa kumaliza na mabao 21 mawili zaidi ya Feir Toto amekuwa Mfungaji Bora wa Ligi Kuu na akajumuishwa kwenye orodha ya wachezaji wa kuunda kikosi cha Bora cha msimu.
Ukawa usiku mzuri zaidi kwa klabu ya Yanga baada ya Muargentina, Miguel Angel Gamondi kushinda Tuzo ya Kocha Bora dhidi ya Mfaransa, Bruno Ferry wa Azam FC na Mkenya, .David Ouma wa Coastal Union.
Naye Ibrahim Hamad 'Bacca' akabeba Tuzo ya Beki Bora wa Ligi Kuu dhidi ya Muivory Coast, Kouassi Yao wa Yanga pia na Mohamed Hussein 'Tshabalala' wa Simba.
Mabeki wa Yanga, Dickson Job, Kouassi Yao wakaingia kweye kikosi cha msimu, pamoja na viungo, Aziz Ki, Mudathir Yahya na Maxi Mpia Nzengeli.
Mkongo Leyi Matampi alishinda Tuzo ya Kipa Bora Diarra na Ayoub Lakred wa Simba, Kipre Junor akasinda Tuzo ya Bao Bora la Msimu, Diarra akashinda Tuzo ya Uokoaji Bora, Mtibwa Sugar iliyoshuka Daraja ndiyo timu yenye Nidhamu dhidi ya Ihefu FC na Kagera Sugar, wakati Ahmed Arajjiga ameshinda Tuzo ya Refa Bora wa mara nyingine,
Ni usiku uliojumuisha Tuzo za Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la CRDB, ambalo kama Ligi ni Yanga waliotwaa taji hilo pia.
Mshambuliaji wa Yanga, Clement Francis Mzize ndiye Mfungaji Bora wa CRDB Cup dhidi ya Edward Songo JKT Tanzania, Diarra Kipa Bora dhidi ya Khomein Abubakar wa Ihefu na Msudan, Mohamed Mustapha wa Azam FC, Feisal Salum Mchezaji Bora dhidi ya Aziz Ki, Mzize, Bacca na Kipre Jr.
Nahodha wa timu ya taifa, Mbwana Ally Samatta wa PAOK ya Ugiriki akashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Anayecheza nje dhidi ya Himid Mao wa Ghazl El Mahalla ya Misri na Novatus Dismas Miroshi wa Shakhtar Donetsk ya Ukraine.
Naye Aisha Masaka aliyehamia Brighton & Hove Albion kutoka BK Häcken ya Sweden meshinda Tuzo ya Mchezaji wa Kike anayecheza nje dhidi ya Clara Luvanga wa Al Nasr ya Saudi Arabia na Opa Clement aliyehamia Henan FC ya China kutoka Beşiktaş ya Uturuki.
Katika Ligi ya Wanawake, Aisha Mnunka wa Simba Queens ndiye Mchezaji Bora na Mfungaji Bora, Kipa Bora Caroline Lufo wa Simba Queens, Kocha Bora Juma Mgunda wa Simba Queens, Timu yenye Nidhamu ni Bunda Qeens, Refa Bora Amina Kyando.
GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/LeADowl
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang AZIZ KI ABEBA TUZO NNE IKIWEMO YA MCHEZAJI BORA LIGI KUU. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2024/08/aziz-ki-abeba-tuzo-nne-ikiwemo-ya.html. Terimakasih atas perhatiannya.