TP Mazembe imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, CAPS United Uwanja wa Taifa mjini Harare, Zimbabwe.
Kwa matokeo hayo, Mazembe inatolewa hatua ya 32 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa bao la ugenini, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Lubumbashi.
Na sasa inaungana na Yanga SC iliyotolewa na Zanaco ya Zambia na wote watamenyana na timu zilizovuka 32 Bora ya Kombe la Shirikisho kuwania tiketi ya hatua ya makundi.
Jesse Were (juu) ameendelea kuifungia mabao Zesco United michuano ya Afrika
Yanga pia imetolewa kwa bao la ugenini kama Mazembe, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kwenda kulazimishwa sare ya 0-0 Lusaka.
Timu nyingine ya Zambia, Zesco United imeendelea kufanya vizuri hata baada ya kocha wake wa msimu uliopita, George Lwandamina kuchukuliwa na Yanga.
Zesco jana ilifuzu hatua ya makundi ya Ligi Mabingwa Afrika inayoshirikisha timu 16, baada ya kulazimisha sare ya 2-2 ugenini na Le Messager Ngozi nchini Burundi.
Mabao yote manne yalipatikana kipindi cha pili jana Uwanja wa Prince Louis mjini Bujumbura na kufanya mabingwa wa Zambia wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa iliyopita mjini Ndola.
Oliver Sabumukama alianza kuifungia Le Messager Ngozi dakika ya 49, kabla ya mshambuliaji Mkenya Jesse Were kuisawazishia Zesco dakiak ya 61.
Wenyeji wakapata bao la pili kupitia kwa Abdoul Amini dakika ya 86, kabla ya Zesco kusawazisha tena kupitia kwa beki Mkenya, David Owino.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2midcnZ
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms