TIMU ya Ahmad, rais mpya wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Madagascar imefuzu hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2019 baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sao Tome & Principe jana mjini Antananarivo.
Matokeo hiyo yanakifanya kisiwa hicho kisonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Jumatano.
‘Les Barea’ ilipata bao la kuongoza sekunde ya 60 kupitia kwa Paulin Voavy, ambaye alifunga na la pili dakika ya 17.
Rais mpya wa CAF, Ahmad (katikati) timu yake imefuzu hatua ya makundi
Harramiz Ferreira Soares akawafungia Sao Tome bao moja dakika ya 28, kabla ya Carolus Andriamahitsinoro kuifungia Madagascar dakika ya 81 na Jose da Silva Varela kuiongezea bao Tome dakika ya 84.
Madagascar sasa inaingia Kundi A kuungana na Senegal, Equatorial Guinea na Sudan, wakati nafasi nyingine mbili zitapata washiriki leo baada ya mechi kati ya Mauritius na Comoros na Sudan Kusini dhidi ya Djibouti.
Wakati huo huo: Katibu Mkuu wa CAF, Mmorocco, Hicham el Amrani mwenye umri wa miaka 38, amejiuzulu jana kwa kuwasilisha barua baada ya uongozi mpya kuingia madarakani.
Amrani anaondoka ofisi za CAF, Cairo nchini Misri baada ya miaka nane ya kufanya kazi chini ya Rais Mcameroon, Issa Hayatou aliyeshindwa na Ahmad katika uchaguzi.
Amrani na Hayatou wapo chini ya uchunguzi juu ya mauzo ya haki za Televisheni kwa kampuni ya Kifaransa, Lagardere.
Ratiba na matokeo mechi za awali
Jumapili Machi 26, 2017
Madagascar 3-2 Sao Tome & Principe (1-0)
Jumanne Machi 28, 2017
Mauritius vs Comoros (0-2)
Sudan Kusini vs Djibouti (0-2)
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2nWaNzn
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms