KLABU ya Barcelona imemtangaza Ernesto Valverde kuwa kocha wao mpya, mtu mzima huyo wa umri wa miaka 53 akisaini mkataba wa miaka miwili.
Rais wa klabu, Josep Maria Bartomeu ametangaza uteuzi wa kocha huyo mpya katika mkutano na waandishi wa habari leo, ikiwa ni siku mbili baada ya Luis Enrique, aliyeshinda mataji tisa kati ya 13 ndani ya misimu mitatu kuondoka kwenye klabu hiyo.
Valverde atatambulishwa rasmi Alhamisi. Bartomeu amesema: "Nimezungumza naye leo amefurahi sana kwa sababu na changamoto maalum sana kwake. Anastahili, kwa kujua na kwa uzoefu alionao,".
Ernesto Valverde anarithi nyayo za Luis Enrique kwa kuwa kocha mpya wa vigogo wa La Liga, Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Valverde anafuata nyayo za Pep Guardiola, Tito Vilanova na Luis Enrique ambao kwanza walianza kama wachezaji wa klabu hiyo kabla ya kuwa makocha.
Wote walishinda mataji ya Ligi katika misimu yao ya kwanza na jukumu la kwanza la Valverde kuwarejeshea Barcelona taji hilo baada yaa msimu huu kuchukuliwa na Real Madrid.
Atakuwa na muda mfupi sana kabla ya kumenyana na Real Madrid mara tatu – kwanza kwenye ziara ya klabu ya kujiandaa na msimu mpya na baadaye mara mbili kwenye Super Cup ya Hispania nyumbani na ugenini.
Valverde aliichezea Barcelona kwa miaka miwili, kuanzia 1998 hadi 2000 akicheza jumla ya mechi 20 na kufunga mabao manane kama mshambuliaji akishinda mataji ya Kombe la Washindi na Kombe la UEFA, kabla ya kusaini Bilbao ambako alicheza kwa miaka sita.
Uteuzi wake wa sasa unatimiza ndoto za pande zote mbili kufanya kazi pamoja, kwani ndiye aliyekuwa chaguo halisi wakati Tata Martino anaondoka Barcelona mwaka 2014, lakini ghafla Barca ikamgeukia Enrique.
Mwanzoni mwa msimu wakati Enrique alipoiambia bodi ya Barcelona hataongeza mkataba mwishoni mwa msimu, wakamuambia Valverde asiongeze mkataba Athletic Bilbao ili ahamie Nou Camp kiulaini.
Ametua na wasaidizi wake mwenyewe katika benchi la ufundi huku aliyekuwa Msaidizi wa Enrique namba mbili, Juan Carlos Unzue akihamia Celta Vigo na Jon Aspiazu akiwa msaidizi wa Valverde.
Amejiunga akitokea Bilbao kama kocha wa mazoezi ya viungo, Jose Antonio Pozanco.
Hii si mara ya kwanza kwa Valverde kufanya kazi mjini Barcelona, kwa sababu aliifundisha Espanyol kuanzia mwaka 2006 hadi 2008 ambako aliiwezesha klabu kushika nafasi ya pili kwenye Kombe la UEFA.
Kisha baadaye akashinda mataji matatu ya ligi na vikombe viwili akiwa na Olympiacos nchini Ugiriki.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2qv3E6X
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang ERNESTO VALVERDE NDIYE KOCHA MPYA WA BARCELONA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/05/ernesto-valverde-ndiye-kocha-mpya-wa.html. Terimakasih atas perhatiannya.