HISTORIA imewekwa jana jana kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 nchini Gabon 2017, wakati Mali ilipokuwa nchi ya kwanza kutwaa taji mara mbili mfululizo, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Black Starlets ya Ghana.
Katika mchezo mzuri wa fainali uliofanyika Uwanja wa d'Angondjé au l'Amitie kama unavyofahamika pia, Seme Camara ndiye aliyefunga bao pekee kwa mkwaju wa penalti dakika ya 20 na Mali inaungana na nchi kama Nigeria, Ghana na Gambia zilizotwaa taji hilo mara mbili kila moja tangu mwaka 1995 ilipoanzishwa michuano hiyo.
Mchezo ulikuwa mkali tangu mwanzo na timu zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu, lakini washambuliaji pacha wa Mali, Seme Camara na Hadji Drame waliipa wakati mgumu mno safu ya ulinzi ya Ghana.
Dakika ya 30 Mali walipata penalti nyingine, lakini kipa wa Black Starlets, Danlad Ibrahim akapangua mkwaju wa Mamadou Samake na mwisho wa mchezo, Nahodha wa mabingwa, Mohammed Camara akatajwa Mchezaji Bora wa Mechi.
Mabingwa Mali kwa pamoja na washindi wa pili, Ghana, washindi wa tatu Guinea na Niger walioshika nafasi ya nne, wataiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia la FIFA la U-17 nchini India mwezi Oktoba.
Mapema katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, Guinea iliifunga Niger 3-1 na kumalia nyuma ya Ghana. Mabao ya Guinea yamefungwa na mshambuliaji Djibril Fandje Toure mawili moja kila kipindi na Eldadj Abdourahamane Bah, wakati la Niger lilifungwa na Ibrahim Boubacar Marou.
Michuano hiyo, ilishirikisha timu nane kuanzia ngazi ya makundi, Kundi A likiundwa na Gabon, Ghana, Guinea na Cameroon, wakati Kundi B liliundwa na Angola, Niger, Mali na Tanzania iliyokuwa inashiriki kwa mara ya kwanza.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2s5iO4e
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang NI MALI WAFALME WA SOKA YA VIJANA AFRIKA TENA. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/05/ni-mali-wafalme-wa-soka-ya-vijana.html. Terimakasih atas perhatiannya.