MAPEMA mwaka 2012, tasniya ya Habari ilipata ugeni wa chombo kipya rasmi cha habari mtandaoni, bongostaz.blogspot.com ambacho kilikuwa maalum kwa habari za michezo, sanaa na burudani.
Bogostaz ilijikita zaidi kwenye habari za soka, ikiripoti kwa weledi, usawa na kwa ujumla kuzingatia miiko ya taaluma ya Uandishi wa Habari.
Na hiyo ni kwa sababu, mwanzilishi na mmiliki wake, Mahmoud Ramadhani Zubeiry ni Mwandishi wa Habari halisi, aliyepitia mikononi mwa magwiji wa taaluma ya Habari akina Jenerali Twaha Ulimwengu, Salva Rweyemamu, Johnson Mbwambwo, Francis Chirwa na wengine waliompika akaiva kitaaluma.
Mtendaji Mkuu wa Bin Zubeiry Sports - Online anawapa '5' wasomaji wote wa tovuti hii
Na hivi ndivyo Bin Zubeiry Sports - Online inavyosomwa, watu zaidi ya 100,000 wanaingia kila siku mfululilizo
Bongostaz ilijitahidi kuwa ya kipekee, kwanza kuanzisha mfumo wa kupandisha habari kila wakati, kila siku, kutoka mfumo uliokuwapo wakati huo wa kupandisha habari wenye chombo chao wakijisikia, wakati mwingine hata wiki nzima ilipita bila habari au taarifa mpya.
Changamoto hiyo ikapokewa vizuri na vyombo vya habari vya mitandaoni tulivyovikuta, ikiwemo Michuzi Blog ya mkubwa wetu na mwasisi wa mambo haya ya habari za mitandaoni nchini, Muhiddin Issa Michuzi na nyinginezo.
Bongostaz haikusita kutumia gharama yoyote katika kuhakikisha inapata habari, iwe ndani au nje ya nchi na kwa sababu hiyo ndani ya muda mfupi, hiyo ikawa blogu namba ya michezo Tanzania.
Ujio wa blogu nyingine za michezo zilizokuja na sera tofauti zikiwemo zisizozingatia miiko na maadili ya Taaluma ya Habari zaidi ya maslahi, haukuiyumbisha Bongostaz na ikabaki kusimama kama chombo mfano wa kuigwa cha habari za mitandaoni.
Tumepitia vipindi tofauti na katika kukuwa kwetu kama taasisi, tulilazimika kuongeza wafanyakazi, na kuna wakati tulijikuta tunaajiri watu wasio waadilifu, waaminifu na wakataka kuchafua sifa ya chombo chetu.
Lakini tulisimama imara na kuiaminisha jamii kilichotokea ni bahati mbaya, kwa kuhakikisha kila asiyestahili katika safari yetu tunamteremsha jahazini. Na ndivyo ilivyofanyika na watu wakaendelea kuwa na imani nasi.
Wakati mwingine zilifanyika mbinu chafu za watu wenye roho mbaya kujaribu kutaka kuishusha Bongostaz, kwa kuwachafua baadhi yetu akiwemo Mtendaji Wetu Mkuu, Mahmoud Zubeiry – lakini hekima na busara vilituongoza kustahmili na kupuuza maudhi yote, huku tukiendelea na uwajibikaji wetu mzuri uso na shaka.
Ukawadia wakati, Mei mwaka jana tukaamua kutoka kwenye blogu na kuwa tovuti rasmi ya habari za michezo, www.binzubeiry.co.tz maarufu kama Bin Zubeiry Sports – Online na sasa umetimia mwaka mmoja.
Ni mafanikio makubwa kwa mwonekano wa ndani na nje – Bin Zubeiry Sports – Online ni kitu kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi. Kila kitu kinajieleza chenyewe kuhusu sisi, kama mtu mmoja mmoja na kama taasisi.
Hatuna cha kusema zaidi ya kwanza kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha na pili kwenu nyinyi wasomaji wetu kwa namna mlivyotuamini na heshima kubwa mliyotupa. Tunashukuru sana.
Bin Zubeiry Sports – Online kwa sasa tunajivunia kuwa tovuti bora zaidi ya habari za michezo kwa lugha ya Kiswahili duniani.
Tunajivunia siyo tu kutangaza kwa wingi habari za michezo za nyumbani na wachezaji wetu hususan soka, lakini pia kukitangaza Kiswahili, lugha yetu mwanana.
Pamoja na hayo, Bin Zubeiry Sports – Online hatutalewa sifa kwa mafanikio ya awali, bali tutaendelea kusimamia dhamira tulizojiwekea ili kuendelea kuwa bora kwa vitendo, kwa maana zote na sifa zote njema.
Tunawashukuru kwa kutuamini na kuendelea kuwa nasi, na tunaomba muendelee kutuamini, kwani mambo mazuri zaidi yanakuja. Asanteni. Furahia mwaka mmoja wa Bin Zubeiry Sports – Online.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2rQ8bF2
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang NI MWAKA MMOJA TANGU BIN ZUBEIRY IWE TOVUTI RASMI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2017/05/ni-mwaka-mmoja-tangu-bin-zubeiry-iwe.html. Terimakasih atas perhatiannya.