Na Salum Vuai, ZANZIBAR
TIMU ya Singida United imeingizwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi na itakuwa Kundi A pamoja na Yanga SC, Zimamoto, Mlandege, JKU na Taifa ya Jan’gombe.
Kundi linabaki kuwa na timu za Simba, Azam FC, URA, Jamhuri na Mwenge baada ya kuondolewa kwa Taifa ya Jang’ombe iliyohamishiwa Kundi B ambako imeondolewa Shaba.
Michuano ya Mapinduzi itaanza kesho kwa mechi kati ya Mlandege na JKU Saa 8:30 mchana, kabla ya Jamhuri kumenyana na Mwenge Saa 10:30 jioni na Zimamoto kupepetana na Taifa ya Jan’gombe Saa 2:15 usiku, zote zikichezwa Uwanja wa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mabingwa watetezi, Azam FC wataanza mashindano Jumapili kwa kumenyana na Mwenge Saa 10:30 jioni kabla ya Jamhuri kumenyana na URA Saa 2:15 usiku, wakati vigogo Simba na Simba wao wataanza mashindano Janauri 2, 2018.
Simba wataanza na Mwenge Saa 10:30 jioni wakati Saa 2:15 usiku Yanga watapepetana na Mlandege, mechi ambazo zitatanguliwa na mchezo kati ya Singida United na Zimamoto.
Azam watarudi tena uwanjani Januari 3, 2018 kumenyana na Jamhuri SC Saa 10:30, baadaye URA Januari 5, 2018 Saa 10:30, kabla ya kukutana na Simba Januari 6 Saa 2:15 usiku kukamilisha mechi zake za Kundi A.
Simba watarudi uwanjani Januari 4 kumenyana na Jamhuri Saa 2:15 usiku, kabla ya kukutana na Azam Januari 6 na kuhitimisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na URA Januari 8, 2018 Saa 10:30 jioni.
Yanga wao watarudi uwanjani Januari 4 Saa 10:30 jioni kumenyana na JKU, kabla ya kupepetana na Taifa ya Jan’gombe Saa 2:15 usiku Januari 5, Zimamoto Saa 2:15 usiku Januari 7 na kukamilisha mechi zake za Kundi B Januari 8 kwa kumenyana na Singida United.
Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Januari 8, wakati Januari 9 itakuwa mapumziko na Nusu Fainali zitafuatia Januari 10, kabla ya kilele mashindano kwa mchezo mtamu wa fainali Januari 13, ambao utahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo, Dk. Ali Mohammed Shein.
MAKUNDI:
KUNDI A: URA; Jamhuri; Mwenge; Azam; Simba.
KUNDI B: Zimamoto; Mlandege; Yanga; JKU; Taifa ya Jan’gombe; Singida United.
RATIBA KAMILI:
Desemba 29, 2017
Mlandege vs JKU (Saa 8:30 mchana)
Jamhuri vs Mwenge (Saa 10:30 jioni)
Zimamoto vs Taifa ya Jan’gombe (Saa 2:15 usiku)
Desemba 30, 2017
Zimamoto vs JKU (Saa 10:30 jioni)
Taifa ya Jan’gombe vs Mlandege (Saa 2:15 usiku)
Desemba 31, 2017
Azam vs Mwenge (Saa 10:30 jioni)
Jamhuri vs URA (Saa 2:15 usiku)
Januari 1, 2018
Mlandege vs Zimamoto (Saa 10:30 jioni)
JKU vs Taifa ya Jan’gombe (Saa 2:15 usiku)
Januari 2, 2018
Singida United vs Zimamoto (Saa 8:30 mchana)
Simba SC vs Mwenge (Saa 10:30 jioni)
Yanga vs Mlandege (Saa 2:15 usiku)
Januari 3, 2018
URA vs Mwenge (Saa 8:30 mchana)
Azam FC vs Jamhuri (Saa 10:30 jioni)
Taifa Jan’gombe vs Singida United (Saa 2:15 usiku)
Januari 4, 2018
JKU vs Yanga (Saa 10:30 jioni)
Simba vs Jamhuri (Saa 10:30 jioni)
Januari 5, 2018
Mlandege vs Singida United (Saa 8:30 mchana)
URA vs Azam (Saa 10:30 jioni)
Yanga vs Taifa Jan’gombe (Saa 2:15 usiku)
Januari 6, 2018
JKU vs Singida United (Saa 10:30 jioni)
Simba vs Azam FC (Saa 2:15 usiku)
Januari 7, 2018
Zimamoto FC vs Yanga SC (Saa 10:30 jioni)
Januari 8, 2018
Simba SC vs URA (Saa 10:30 jioni)
Yanga SC vs Singida United (Saa 10:30 jioni)
Januari 9, 2018
MAPUMZIKO
Januari 10, 2018
NUSU FAINALI
Mshindi Kundi A Vs Mshindi wa Pili Kundi B (Saa 10:30 jioni)
Mshindi Kundi B Vs Mshindi wa Pili Kundi A (Saa 2:15 usiku)
Januari 13, 2018
FAINALI
(Saa 2:00 usiku)
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2E6Ixz8
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms