Na Esther Msonge, DAR ES SALAAM
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli amemteua aliyewahi kuwa Msemaji wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.
Akilihutubia taifa kupitia Televisheni ya Taifa, TBC1 leo, Rais Magufuli pia amemtangaza mrembo, mwanamitindo na mwigizaji wa filamu, Jokate Mwegelo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
Mabadiliko mengine ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), Patrobas Katambi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli amewateua Jerry Muro (picha ndogo kulia) na Jokate Mwegeleo (picha ndogo kushoto) kuwa Wakuu wapya wa Wilaya
Naye Lengay Ole Sabaya ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Kilimanjaro, wakati Mbunge wa zamani wa upinzani, kupitia chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
Aidha, Rais Magufuli amemhamisha mkoa wa Katavi, aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla katika mabadiliko yaliyotangazwa leo.
Muro alikuwa Msemaji wa klabu ya Yanga kuanzia Septemba mwaka 2014 hadi Julai mwaka jana alipoondolewa na nafasi yake kupewa Dissmas Ten ambaye awali alikuwa klabu ya Mbeya City.
Lakini umaarufu wake ulianzia akiwa mtangazaji wa vituo vya Televisheni vya ITV na baadaye Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
Na Jokate aliyezaliwa Machi 20, mwaka 1987 mjini Washington, D.C, aliibukia kwenye shindano la Miss Tanzania, akianzia kuwa Miss Kurasini mwaka 2006, baadaye Miss Temeke na kwenda kushika nafasi ya pili kwenye Miss Tanzania, nyuma ya Wema Sepetu.
Baadaye akajikita kwenye uanamitindo, ubunifu, uigizaji na ujasiriamali akijipambanua zaidi kwa kuifanya alama yake ya kuzaliwa nayo kuwa nembo yake ya kibiashara, Kidoti.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2NRfpjy
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms