MWANARIADHA wa Kenya, Eliud Kipchoge ameweka rekodi mpya ya dunia kwenye mbio ndefu, Marathoni kwa kutumia saa mbili, dakika moja na sekunde 39 katika mbio za Berlin.
Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33 ameipiku rekodi ya awali kwa zaidi ya dakika ya moja ambayo iliwekwa na Mkenya mwenzake, Dennis Kimetto aliyetumia Saa 2:02:57 mjini Berlin mwaka 2014.
"Nakosa maneno ya kuzungumza katika siku hii," alisema Kipchoge. "Niko vizuri mno, nafurahi kuvunja rekodi ya dunia,".
Mshindi wa mbio za wanawake ni Gladys Cherono wa Kenya pia aliyetumia muda wa Saa 2:18:11. Kipchoge anatambulika kama mmoja wa wanariadha wakubwa wa mbio ndefu wa muda wote.
Alishinda mbio za London Marathon kwa mara ya tatu mapema mwaka huu na ni bingwa wa Olimpiki katika mbio hizo.
"Ilikuwa vigumu," amesema Kipchoge. "Nakimbia mbio zangu mwenyewe, Nawaamini walimu wangu, programu zangu na kocha wangu. Hicho ndicho kinachonifanya nimalize kilomita,".
Mwaka 2017, Kipchoge alikosa kwa sekunde 26 tu kuwa mwanariadha wa kwanza kukimbia Marathoni ndani ya saa mbili.
Mkenya huyo alitumia muda wa Saa 2:00.25, lakini kwa sababu ya vipimo ambavyo havikuthibitishwa vilivyotumika, muda huo haukuhesabiwa kama rekodi ya dunia.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2MBGWUU
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Terimakasih anda telah membaca artikel tentang KIPCHOGE AWEKA REKODI MPYA YA DUNIA YA MARATHONI. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2018/09/kipchoge-aweka-rekodi-mpya-ya-dunia-ya.html. Terimakasih atas perhatiannya.