TIMU ya taifa ya Madagascar anapotokea rais wa CAF, Ahmad imefuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga Equatorial Guinea 1-0 nyumbani jana.
na baadaye, Misri, Senegal na Tunisia wakafanikiwa kuungana na Madagascar pia kukamilisha timu tano, kati ya 24 zinazotarajiwa kwenda Cameroon, nyingine ni wenyeji, Simba Wasiofungika.
Huku timu mbili zinafuzu kutoka kila kundi kati ya yote 12, Madagascar ilikuwa ina nafasi nzuri ya kufuzu baada ya kuanza mechi zao za Kundi A kwa ushindi wa ugenini dhidi ya Sudan mwaka jana.
Madagascar imefuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
Na pamoja na ushindi wa nyumbani na ugenini wa 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea siku tano zilizopita na bao pekee la Njiva Rakotoharimalala jana mjini Antananarivo mambo safi sasa.
Senegal ilishinda 1-0 nchini Sudan, shukrani kwa mfungaji, Sidy Sarr katika mchezo ambao Simba wa Teranga walimkosa mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane aliyeumia dole gumba.
Pamoja na kumkosa mshambuliaji wake nyota, Mohamed Salah ambaye ni majeruhi, lakini Misri ilishinda 2-0 ugenini dhidi ya Swatini, zamani Swaziland, na ushindi wa 2-1 wa Tunisia mjini Niger ulivihakikishia vigogo hivyo vya Kaskazini kmwa Afrika kufuzu kutoka Kundi J.
Mabao yote ya Tunisia yalifungwa na Firas Chawat akiichezea timu yake ya taifa kwa mara ya kwanza.
Uganda inahitaji pointi moja zaidi kujihakikishia tiketi ya Cameroon mwakabi baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Lesotho ugenini jana na Guinea nayo ipo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu licha ya sare ya 1-1 na Rwanda jana.
Nyota wa Liverpool, Naby Keita alitolewa baada ya kipindi cha kwanza kufuatia kuumia misuli.
Ivory Coast bado wana kazi ya kufanya , kwani jana walilazimishwa sare ya 0-0 ugenini na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), lakini inapewa nafasi kubwa ya kufuzu kutoka Kundi H pamoja na Guinea.
Pamoja na kumkosa mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang, Gabon ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini mjini Juba, bao pekee la Andre Biyogo Poko.
Vibonde Shelisheli walitoa sare ya 0-0 na na Afrika Kusini katika kisiwa hicho cha bahari ya Hindi, wakati mshambuliaji Odion Ighalo aliifungia mabao mawili Nigeria katika ushindi wa 3-2 mjini Sfax akitoka kupiga hat trick dhidi ya Libya mwishoni mwa wiki.
Nigeria sasa inaongoza Kundi E kwa pointi zake tisa ikifuatiwa na Afrika Kusini pointi nane na Libya nne.
Hata hivyo, Afrika Kusini wana michezo mgumu dhidi ya Nigeria nyumbani mwezi ujao na Libya ugenini mwezi Machi mwakani, hivyo wako hatarini kuzikosa fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2yjUTTu
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms