KLABU ya Real Madrid imemfukuza kocha wake, Julen Lopetegui na kumpandisha kocha wa timu B, Santiago Solari kuiongoza timu kwa muda.
Bodi ya Madrid imetofautiana juu ya mbadala wa Lopetegui. Rais, Florentino Perez anamtaka kocha wa zamani wa Chelsea, Antonio Conte lakini mahitaji yake ya mkataba wa miaka miwili na nusu na na wasaidizi hadi watano, vinaweza kumfanya kocha wa Ubelgiji, Roberto Martinez achukue nafasi kiulaini.
Klabu pia inafikiria kumuacha Solari aendelee an kazi hadi mwezi ujao wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa itakapofanya uteuzi wa mwalimu wa kudumu.
Real Madrid imemfukuza Julen Lopetegui baada ya kipigl cha 5-1 kwenye El Clasico Jumapili PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Conte hakubaliki na wachezaji wa sasa na Nahodha, Sergio Ramos amesema: "Heshima inahitaji kuwepo, na si kuletwa," alisema aliopoulizwa juu ya uteuzi wa kocha asiyependa utovu wa nidhamu.
Kocha wa zamani wa Everton na Wigan, Martinez ana nafasi ya kurejea kwenye klabu hiyo baada ya kufika Nusu Fainali kwenye Kombe la Dunia akiwa na Ubelgiji.
Klabu pia inafikiria juu ya Conte kutofautiana na Eden Hazard, ambaye inataka kumchukua msimu ujao kama ataendelea kugoma kusaini mkataba mpya Chelsea.
Conte ameshinda mataji ya Ligi Italia na England, lakini ukali wake ulisababisha atofautiane na wachezaji tegemeo wa Chelsea,. Diego Costa na Hazard ambao walichoshwa na kuchezeshwa nafasi zisizo zao.
Yeyote atayechukuliwa atakuwa kocha wa tano wa Gareth Bale katika miaka yake mitano ya kuwa na klabu hiyo ya Hispania.
Lopetegui alitambulishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid Juni 14 baada ya kufukuzwa timu ya taifa ya Hispania kufuatia kuvuja kwa habari za yeye kujiunga na klabu hiyo huku akiwa na timu ya taifa nchni urusi.
Lakini katika mechi 14 alizoiongoza timu, ameshinda sita tu. Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 52 anaiacha timu ikiwa nafasi ya tisa kwenye msimamo wa La Liga baada ya kipigo cha 5-1 Jumapili kutoka kwa Barcelona Uwanja wa Camp Nou.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2ERLesL
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms