Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
VIGOGO, Simba SC wametinga Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya kuwachapa watani wao, Yanga SC kwa mabao 4-2.
Simba SC sasa inakwenda fainali na itakutana na Namungo FC iliyoitoa Sahare All Stars kwa kuichapa 1-0, mchezo ambao utapigwa Agosti 2 Uwanja wa Mandela, Sumbawanga.
Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na viungo Mbrazil, Gerson Fraga Mzambia, Clatous Chama, Luis Miquissone kutoka Msumbiji na Mzawa Muzamil Yassin.
Fraga aliifungia bao la kwanza Simba SC kwa shuti kali dakika ya 20 akimalizia krosi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama, ambaye alifunga la pili dakika ya 49 akimalizia pasi ya Nahodha John Bocco.
Miquissone akaifungia bao la pili Simba SC dakika ya 52 akimalizia mpira uliookolewa kwa kichwa na Nahodha wa Yanga SC, Papy Kabamba Tshishimbi baada ya krosi ya kiungo Mkenya, Francis Kahata.
Yanga SC wakapata bao lao pekee kupitia kwa kiungo wao, Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 70 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na beki wa kulia, Juma Abdul.
Kiungo Muzamil Yassin akashindilia msumari wa moto kwenye jeneza la Yanga SC kwa kufunga bao la nne dakika ya 88 akimalizia mpira uliotemwa na kipa Metacha Mnata baada ya shuti la mshambuliaji Mnyarwanda, Meddie Kagere.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussen ‘Tshabalala’, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Luis Miquissone, Gerson Fraga/Muzamil Yassin dk81, John Bocco/Meddie Kagere dk72, Clatous Chama na Francis Kahata/Hassan Dilunga dk71.
Yanga SC; Metacha Mnata, Juma Abdul, Jaffar Mohamed, Lamine Moro, Said Juma ‘Makapu’, Ppay Kabamba Tshishimbi/Kelvn Yondan dk55, Feisal Salum, Haruna Niyonzima/Ditram Nchimbi dk55, Deus Kaseke, David Molinga na Bernard Morrison/Patrick Sibomana dk64.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/3fmlrqp
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms