KLABU ya Yanga imesaini mkataba wa ubia na kampuni ya GSM kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa kisasa makao makuu ya klabu hiyo eneo la Jangwani, Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila imefanyika asubuhi ya leo kwenye eneo la mradi, Jangwani, Kampuni ya GSM ikiwakilishwa na Rais wake, Bilionea Ghalib Said Mohamed na Maafisa wengine, Yanga ikiwakilishwa na Rais wake, Mhandisi Hersi Ally Said na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
“Nathibitisha rasmi leo kuwa Young Africans S.C. imeingia katika makubaliano ya ubia wa umiliki wa uwanja wetu mpya kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50 na GSM Group,”alisema, Rais wa Yanga SC Hersi.
Katika ubia huo wa Asilimia 50 kwa 50 za umiliki wa Uwanja huo, Yanga wametoa eneo la mradi, yaani ardhi wakati GSM Group wanatoa fedha za ujenzi huo.
Hersi amesema kwamba matarajio yao ni kwamba ujenzi wa uwanja huu utakamilika na kuzinduliwa rasmi ndani ya kipindi cha miezi 18 hadi 20 ijayo wakiwa na matumaini makubwa kwamba mradi huu utakamilika kwa wakati uliopangwa na kuwa sehemu muhimu ya historia ya klabu yao.
“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mara nyingine kwa Ghalib Said Mohamed pamoja na familia yake, kwa maamuzi yao makubwa na ya kizalendo waliyochukua kwa ajili ya kusaidia kutimiza ndoto ya muda mrefu ya Young Africans S.C.” Eng. Hersi Ally Said,”.
“Kwa kipindi cha takribani miaka 90, klabu hii imeendelea kubeba ndoto na dhamira ya dhati ya kuwa na uwanja wake binafsi. Sisi, kama Wananchi tunajivunia mno maono, juhudi na uzalendo wa viongozi waliotutangulia. Viongozi hao walijitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanatuachia msingi imara unaobeba historia, heshima na utambulisho wa klabu yetu,”.
“Kupitia juhudi zao, klabu ilifanikiwa kumiliki eneo la ardhi lenye ukubwa wa mita za mraba 35,000 hazina ambayo imehifadhiwa kwa zaidi ya miaka 50. Leo hii, kwa fahari kubwa Wananchi tunaelekea kutimiza ndoto hiyo ya kihistoria kwa kuanza safari ya kujenga uwanja wetu wenyewe,” amesema Hersi aliyeingia madarakani Jumamosi ya Julai 9, mwaka 2022.
Rais huyo wa Yanga dhamira yake wakati anaingia katika uongozi ilikuwa ni kuhakikisha klabu inajenga Uwanja wake, lakini alibaini kuwa kabla ya kufikia hatua hiyo kulikuwa kuna umuhimu wa kwanza kuipa klabu mafanikio ya ndani ya Uwanja ili kuvutia wawekezaji.
“Tulipoanza kufanya vizuri na kupata mafanikio, watu wengi walivutiwa kuwekeza ndani ya klabu yetu. Hali hiyo ikaamsha ari, hamasa na matumaini mapya ya kutimiza ndoto ya kuwa na uwanja wetu wenyewe. Aidha, idadi ya wanachama imeongezeka kwa kiasi kikubwa, ndani na nje ya nchi,”.
“Tulipotangaza zabuni ya ujenzi wa uwanja, wawekezaji wengi walijitokeza kuonesha nia ya kushiriki katika mradi huo. Baada ya kupitia mchakato husika, Kamati Kuu hatimaye iliidhinisha GSM Group kuwa mbia mkuu wa ujenzi wa uwanja huo,” amesema Hersi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya GSM, Mama Aisha Mohammed alisema baada ya kusaini mkataba huo wa ujenzi wa uwanja wa kisasa na Yanga SC, watahakikisha utekelezaji wake unazalisha Uwanja ulio bora na wa kipekee kwa Wananchi.
Kwa upande wake, Rais wa GSM, Ghalib Said Mohammed hakuwa na mengi wakati wa kuzungumza ulipowadia kwa kusema tu; “Yanga Bingwa” kama ilivyo kawaida yake kwenye hafla mbalimbali za klabu hiyo.Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert John Chalamila akizungumza kwenye Hafla hiyo iliyohudhuriwa na wadau wengine mbalimbali wakiwemo viongozi wa TFF na wachezaji wa zamani wa klabu hiyo, alimpongeza Ghalib kwa uwekezaji wake Yanga SC kwa ujumla.
“Watu kama GSM ni wa kuwalinda sana. Ukiona mtu anachukua timu, kelele za mishahara zinapotea, timu inasajili vizuri, halafu inaachana na heka heka za vilio ghafla wanahamia kwenye ujenzi wa uwanja, basi ujue klabu hiyo imepata mtu sahihi. Wananchi mnapaswa kumlinda sana Ghalib Said Mohamed,”.
“Nafikiri mmeona mchango wa GSM kwa Klabu yetu, hatimaye anatujengea uwanja. Klabu hii haiendeshwi kwa mdomo na makelele pekee. Hatuwezi kutegemea wafadhili pekee yake. Huwezi kuwa mtu ambaye unakosoa tu timu ikifungwa, fukuza makocha lakini huchangii chochote. Ni muda sasa kuchangia klabu hii ili kusaidia klabu kupiga hatua,” alisema Chalamila na kuongeza;
“Ujenzi wa uwanja wa wa Yanga unahitaji sana miundo mbinu ya eneo la Jangwani kuwa imara. Rais wa Jamhuri ya Muungano Dokta Samia Suluhu alitenga zaidi ya mabilion 10 kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Jangwani. Tunamshukuru sana Mh Rais kwa kuondoa adha ya mafuriko eneo hilo ili kutoa fursa ya ufanisi wa ujenzi wa uwanja wa Yanga SC,”.
from BIN ZUBEIRY SPORTS — ONLINE https://ift.tt/4rTtDeo
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms