Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KRC Genk imeanza vibaya hatua ya makundi ya Europa League baada ya kufungwa mabao 3-2 na wenyeji Rapid Viena katika mchezo wa Kunfi F Uwanja wa Allianz, Viena, Austria.
Hicho kinakuwa kipigo cha pili mfululizo kwa timu hyo ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta baada ya mwishoni mwa wiki kufungwa mabao 2-0 na Standard Liege katika Ligi ya Ubelgiji Jumapili Uwanja wa Maurice Dufrasne mjini Liege.
Mabao ya Genk yamefungwa na Leon Bailey yote, la kwanza dakika ya 29 na la pili dakika ya 90 kwa penalti.
Mbwana Samatta akipambana katika mchezo wa leo mjini Viena
Mabao ya wenyeji, Rapid Viena yamefungwa na Stefan Schwab dakika ya 51, Joelinton Cassio Apolinario de Lira maarufu tu kama Joelinton dakika ya 59 na Omar Colley aliyejifunga dakika ya 60.
Mchezo mwingine wa kundi hilo, wenyeji Sassuolo wameshinda 3-0 dhidi ya Athletic Athletic Bilbao ya Hispania Uwanja wa Citta del Tricolore, mabao ya Pol Lirola dakika ya 60, Gregoire Defrel dakika ya 75 na Matteo Politano dakika ya 82.
Tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, Samatta amecheza jumla ya mechi 25 za mashindano yote, 18 msimu uliopita na saba msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
Katika mechi hizo, ni 14 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tatu msimu huu, wakati 11 alitokea benchi nane msimu uliopita na tatu msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
Kikosi cha Rapid Wien kilikuwa; Strebinger, Schösswendter, Schrammel, Schwab, Schaub, Dibon, Szanto/Hofmann dk61, Pavelic Traustason/Murg dk79 Mocinic na Joelinton/Kvilitaia dk86.
KRC Genk : Bizot, Walsh, Dewaest, Colley, Uronen, Heynen/Susic dk78, Ndidi, Pozuelo, Bailey, Buffalo/Trossard dk64 na Samatta/Karelis dk78.
from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2cqHM5D
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms