• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Disclaimer
  • Sitemap
  • Privacy Policy

Viral Sports

MENU

  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BLOG
  • BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE
  • Hollywoodbets Sports Blog

Mengenai Saya

admin blog
Lihat profil lengkapku

Arsip Blog

  • ►  2025 (242)
    • ►  Juli (1)
    • ►  Juni (8)
    • ►  Mei (44)
    • ►  April (66)
    • ►  Maret (36)
    • ►  Februari (57)
    • ►  Januari (30)
  • ►  2024 (832)
    • ►  Desember (57)
    • ►  November (49)
    • ►  Oktober (54)
    • ►  September (67)
    • ►  Agustus (63)
    • ►  Juli (78)
    • ►  Juni (68)
    • ►  Mei (84)
    • ►  April (92)
    • ►  Maret (77)
    • ►  Februari (65)
    • ►  Januari (78)
  • ►  2023 (1299)
    • ►  Desember (79)
    • ►  November (75)
    • ►  Oktober (88)
    • ►  September (95)
    • ►  Agustus (112)
    • ►  Juli (125)
    • ►  Juni (126)
    • ►  Mei (117)
    • ►  April (148)
    • ►  Maret (135)
    • ►  Februari (82)
    • ►  Januari (117)
  • ►  2022 (1404)
    • ►  Desember (71)
    • ►  November (79)
    • ►  Oktober (117)
    • ►  September (120)
    • ►  Agustus (115)
    • ►  Juli (119)
    • ►  Juni (121)
    • ►  Mei (123)
    • ►  April (121)
    • ►  Maret (119)
    • ►  Februari (130)
    • ►  Januari (169)
  • ►  2021 (2522)
    • ►  Desember (170)
    • ►  November (124)
    • ►  Oktober (138)
    • ►  September (190)
    • ►  Agustus (154)
    • ►  Juli (141)
    • ►  Juni (133)
    • ►  Mei (134)
    • ►  April (252)
    • ►  Maret (348)
    • ►  Februari (355)
    • ►  Januari (383)
  • ►  2020 (4463)
    • ►  Desember (387)
    • ►  November (405)
    • ►  Oktober (348)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (435)
    • ►  Juli (433)
    • ►  Juni (372)
    • ►  Mei (244)
    • ►  April (248)
    • ►  Maret (355)
    • ►  Februari (392)
    • ►  Januari (450)
  • ►  2019 (4532)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (367)
    • ►  Oktober (420)
    • ►  September (394)
    • ►  Agustus (411)
    • ►  Juli (364)
    • ►  Juni (318)
    • ►  Mei (360)
    • ►  April (382)
    • ►  Maret (419)
    • ►  Februari (365)
    • ►  Januari (404)
  • ►  2018 (5483)
    • ►  Desember (328)
    • ►  November (450)
    • ►  Oktober (535)
    • ►  September (484)
    • ►  Agustus (487)
    • ►  Juli (481)
    • ►  Juni (431)
    • ►  Mei (483)
    • ►  April (393)
    • ►  Maret (435)
    • ►  Februari (419)
    • ►  Januari (557)
  • ►  2017 (5921)
    • ►  Desember (477)
    • ►  November (567)
    • ►  Oktober (506)
    • ►  September (518)
    • ►  Agustus (555)
    • ►  Juli (535)
    • ►  Juni (465)
    • ►  Mei (471)
    • ►  April (459)
    • ►  Maret (448)
    • ►  Februari (441)
    • ►  Januari (479)
  • ▼  2016 (2138)
    • ►  Desember (445)
    • ▼  November (509)
      • Vaal Thursday 1 December 2016 Best Bets
      • SHIME KOCHA MPYA JKT RUVU, KIBADENI BADO MKUU WA B...
      • PHIRI SASA ROHO KWATU MBEYA CITY
      • HERCULES 1-1 BARCELONA
      • REAL MADRID 6-1 CULTURAL LEONESA
      • ARSENAL 0-2 SOUTHAMPTON
      • MAN UNITED 4-1 WEST HAM UTD
      • BARCA YAKABWA KOO NA KITIMU CHA SEGUNDA B, SARE 1-1
      • TOTO LA ZIDANE LAANZA KUNG'ARA REAL MADRID
      • ARSENAL 'YAFA KIUME' KOMBE LA LIGI, YAPIGWA 2-0 EM...
      • UKISIKIA 'KUFA NA KUPONA' NDIYO HUKU....ROONEY ALI...
      • IBRA, MARTIAL KILA MMOJA APIA MBILI MAN UNITED YAU...
      • SAMATTA AFUNGA MAWILI GENK YASHINDA 3-1 UGENINI
      • HAYE ATAKA KUZIPIGA KAVU KAVU NA BELLEW
      • SOUTHGATE ASAINI MIAKA MINNE KUFUNDISHA ENGLAND
      • SIMBA YAWASILISHA RISITI ZA MISHAHARA YA KESSY BENKI
      • BABU NGASSA AWASHAURI TOTO KUSAJILI
      • MTIBWA SUGAR YASAJILI KIFAA CHA ZENJI
      • KESI YA AKINA CHACHA, MATANDIKA YAPIGWA KALENDA
      • MALINZI AWAPA POLE WABRAZIL KWA MSIBA MZITO
      • KIPA MPYA WA SIMBA KUTOKA GHANA TAYARI YUPO MJINI
      • South African NFD: Week 13 Preview
      • Italian Serie A: Week 15 Preview
      • German Bundesliga: Week 13 Preview
      • La Liga: Week 14 Preview
      • MICHO AMBEBA JUUKO KIKOSI CHA UGANDA AFCON
      • La Liga: Barcelona v Real Madrid Preview
      • MWAKILISHI WA TANZANIA MISS AFRIKA AREJEA
      • EPL: Week 14 Preview
      • EPL: Manchester City v Chelsea Preview
      • The Hero Golf Challenge 2016 Preview
      • Kenilworth Wednesday 30 November Best Bets
      • LIVERPOOL 2-0 LEEDS UNITED
      • NI NIGERIA NA CAMEROON FAINALI KOMBE LA AFRIKA WAN...
      • LIVERPOOL YAENDA NUSU FAINALI KOMBE LA LIGI, DOGO ...
      • AJALI MBAYA YAUA 76 WAKIWEMO WACHEZAJI WA BRAZIL
      • YANGA WAWAKIMBIA SIMBA POLISI, KESHO MAZOEZI GYMKHANA
      • WAZIRI MWIGULU AKIWA NA 'MIDO' MPYA MZAMBIA WA YAN...
      • CSA T20 Challenge: Wednesday 30 November Preview
      • NASSOR 'FATHER' MWENYEKITI MPYA AZAM FC
      • SIMBA, YANGA WATAKIWA KUWALIPA WADAI WAKE
      • KASEJA, BANKA WAJITOA TIMU YA TAIFA YA UFUKWENI
      • Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM KAMATI ya Nidhamu...
      • MALINZI AMPONGEZA MTAKA
      • Israel Double Lotto - Lucky Numbers
      • Russia Gosloto 5/36 - Lucky Numbers
      • Australia Powerball - Lucky Numbers
      • EFL Cup: Arsenal v Southampton Preview
      • EFL Cup: Manchester United v West Ham United Preview
      • COUTINHO 'ANUSURIKA KISU', HUENDA AKAWAHI MECHI NA...
      • NUSU FAINALI KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WANAWA...
      • NAPE ALIPOMPOKELEA ZAWADI RAIS MAGUFULI JANA
      • SIMBA WANAKUTANA LEO POLISI, MAZOEZI KUANZA KESHO
      • Over 1.4 Million won on Pick 6!
      • KAKOLANYA AKAMATWA AMEPANDA BODA BODA BILA KUVAA H...
      • Football League Championship: Week 19 Preview
      • WAKUU WAPYA WA IDARA YA UFUNDI YANGA WALIVYOANZA K...
      • WACHEZAJI MBEYA CITY WAANZA KUKUSANYIKA KWA KAMBI
      • Vaal Tuesday 29 November 2016 Best Bets
      • PROFESA JAY NA SUGU WALIVYOZINDUA MASHINDANO JANA ...
      • Flamingo Park Monday 28 November 2016 Best Bets
      • BARCELONA MAMBO MAGUMU, SARE TENA 1-1 NA REAL SOCI...
      • REAL SOCIEDAD 1-1 BARCELONA
      • SERIKALI INAZITAKIA NINI SIMBA NA YANGA?
      • MBELE KWA MBELE SAMATTA, HAINA KUFELI
      • BADRU: BUTUA BUTUA INAUA SOKA ZANZIBAR
      • AZAM FC YAMTEMA MUIVORY COAST MWINGINE
      • KESSY SASA AITOA JASHO SIMBA
      • MAN UNITED 1-1 WEST HAM
      • MAN UNITED YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA WEST HAM
      • ARSENAL 3-1 BOURNEMOUTH
      • SAMATTA AGONGA ZOTE 90, LAKINI GENK YAFA 6-0 UGENINI
      • ULIMWENGU: MIPANGO YA ULAYA INAENDELEA
      • SANCHEZ APIGA MBILI, ARSENAL YASHINDA 3-1 EMIRATES
      • HATIMA YA KESSY NI LEO
      • WACKO JACKO NA MZEE MWINYI DAR ES SALAAM 1992
      • YANGA IKIMTUMIA KWA FAIDA PLUIJM ITATAMANI KUWA NA...
      • CHELSEA 2-1 TOTTENHAM
      • VICTOR MOSES AING'ARISHA CHELSEA, YAILAZA 2-1 SPURS
      • RONALDO AFUNGA MABAO YOTE, REAL MADRID YASHINDA 2-1
      • LIVERPOOL 2-0 SUNDERLAND
      • REAL MADRID 2-1 SPORTING GIJON
      • BUNLEY 1-2 MAN CITY
      • LIVERPOOL YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND
      • 2016 Summer Cup Winner
      • AGUERO APIGA ZOTE MBILI, MAN CITY YASHINDA 2-1
      • SAMATTA: NIKO KATIKA WAKATI MGUMU KWA SASA
      • BALOTELLI KUKOSEKANA MECHI TATU NICE
      • WAYNE ATAKA KUONDOKA AZAM AKACHEZE KWA MKOPO KUPAT...
      • LWANDAMINA: NAMI NI MUUMINI WA SOKA YA PASI NYINGI
      • BINTU HUYU WA KIBONGO ATAKUWA MISS AFRIKA KESHO?
      • TEGETE KUAMUA MUSTAKABALI WAKE MWADUI MWAKANI
      • Writers' Weekend Treble
      • LWANDAMINA: SITABADILI CHOCHOTE KWENYE BENCHI LA U...
      • Greyville Sunday 27 November 2016 Best Bets
      • End of The Year Tour: Ireland v Australia Preview
      • UTAMBULISHO WA WAKUU WAPYA WA IDARA YA UFUNDI YANGA
      • Turffontein Saturday 26 November 2016 Best Bets
      • Kenilworth Saturday 26 November Best Bets
      • ROMA 4-1 VIKTORIA PLZEN
    • ►  Oktober (482)
    • ►  September (466)
    • ►  Agustus (236)
Diberdayakan oleh Blogger.
Home » BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE » YANGA IKIMTUMIA KWA FAIDA PLUIJM ITATAMANI KUWA NAYE DAIMA MILELE

YANGA IKIMTUMIA KWA FAIDA PLUIJM ITATAMANI KUWA NAYE DAIMA MILELE

NI vigumu kwa namna yoyote jina la Tambwe Leya (sasa marehemu) kukosekana kwenye historia ya klabu ya Yanga.
Yanga ilimpata kocha huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwaka 1974 ilipokwenda Brazil kwa ziara ya mafunzo.
Ilimkuta akiwa anasomea ukocha nchini humo na ili kukwepa gharama za kummiliki kocha wake wa wakati huo, Profesa Victor Stanslescu, aliyefanya kazi ya kihistoria Jangwani, iliamua kumchukua Mkongo huyo.
Mshahara aliokuwa akilipwa Tambwe haukufika hata nusu ya mshahara wa kocha Mromania, Dk Victor. Victor naye ni kocha wa kihistoria pia Jangwani, alianzisha mpango mzuri wa soka vijana. 
Alikuwa akichukua mipira yake mingi na kuwaita vijana, ili waonyeshe uwezo wao mbele ya macho yake. Waliomkuna kwa vipaji vyao aliwachukua na kwenda kuunda kikosi cha vijana kilichokuwa madhubuti cha klabu hiyo.
Kwa mtaji huo, ndiyo walipatikana wanasoka nyota Tanzania kama Juma Pondamali 'Mensah', Mohamed Adolph Rishard, Mohamed Yahya 'Tostao', Kassim Manara, Mohamed Mkweche, Jaffar Abdulrahaman, Hamisi Swedi, Gordian Mapango na wengineo. 
Wakati huo, Mwenyekiti wa Yanga alikuwa ni Mangara Tarbu (sasa marehemu).
Baada ya Tambwe kutua Yanga, alitaka kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza, akitaka kutumia wachezaji vijana, akisema kwamba wakongwe uwezo wao unaelekea ukingoni. 
Lakini ni kipindi hicho Yanga ilikuwa inatawala soka ya Tanzania, imetoka kutwaa ubingwa mfululizo tangu mwaka 1968 hadi 1972. 
Mwaka 1973 watani wao wa jadi, Simba, ndio waliotwaa taji hilo, lakini mwaka 1974 Yanga walitwaa tena ubingwa wa nchi.
Mwaka 1975, Yanga ilitwaa ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati, sasa Kombe la Kagame, ikiifunga Simba kwenye fainali mabao 2-0 visiwani Zanzibar. 
Wafungaji wa mabao hayo walikuwa wale wale wauaji wa fainali ya Klabu Bingwa ya Taifa mwaka 1974, Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza, Sunday Manara na Gibson Sembuli (marehemu), katika ushindi wa 2-1, bao la Simba likifungwa na Adamu Sabu (sasa marehemu).
Kwa sababu hiyo, ilikuwa ngumu kuwashawishi watu kwamba wachezaji wa Yanga wamezeeka.
Kipindi hicho wakongwe wa Yanga walikuwa akina Elias Michael 'Nyoka Mweusi', Muhidini Fadhili na Patrick Nyaga, wote makipa, mabeki Boy Iddi Wickens, Athumani Kilambo 'Baba Watoto', Badi Saleh, Hassan Gobbos, Omar Kapera, viungo Abdurahman Juma, Abdurahman Lukongo, Sunday Manara 'Computer', Leonard Chitete, na washambuliaji Gibson Sembuli, Kitwana Manara 'Popat' na Maulid Dilunga.  
Lakini pamoja na ubishi huo, baada ya kushindwa kutetea Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki mjini Mombasa, Kenya, uliibuka mgogoro mkubwa na wa kihistoria ndani ya klabu hiyo.
Yanga ilianza vizuri tu katika kundi lake B, ikiifunga 2-1 Mseto SC ya Morogoro, kabla ya kuitandika Green Bufalloes ya Zambia 2-0, Bata Bullets ya Malawi 3-1, iliongoza kundi hilo, ikifuatiwa na Mseto, mabingwa wa Tanzania mwaka 1975.
Katika Nusu Fainali, Yanga iliifunga 3-0 Express ya Uganda wakati Mseto iliona cha mtema kuni kwa Luo, baada ya kutandikwa 5-0. Yanga iliuacha ubingwa Mombasa, baada ya kulala 2-1 kwa Luo kwenye fainali.
Timu iliporejea nyumbani, mgogoro ukaibuka, wanachama walikuja juu na kutaka kumpiga Mwenyekiti wao wakati huo, mzee Mangara, ambaye aliokolewa kwa kutoroshewa mlango wa nyuma. 
Vyanzo vinasema kwamba, wanachama walifika na bakora Jangwani wakitaka kumchapa Mangara. Walikuwa wanataka hesabu za mapato na matumizi ya klabu, lakini walikuwa wenye ghadhabu wakifanya fujo, hivyo ili kuepuka balaa hilo, Mangara alitoroshwa na kuwaacha ‘solemba’ waliokuwa wanamsubiri nje wamchape bakora. 
Mgogoro wa Yanga Kandambili na Yanga Raizoni uliitafuna Yanga kwa miaka minne.
Kipindi hicho Yanga ilikuwa safi kiuchumi, ilikuwa ina mabasi matano yaliyokuwa yakiingizia fedha klabu, Uwanja wa Kaunda uliojengwa kwa mkopo wa Sh 500,000 wa Benki ya Nyumba (THB) ulikuwa bado mpya unavutia watu wengi wakati wa mazoezi ya timu hiyo.  
Yanga ilisaidiwa pia fedha na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Hayati Abeid Karume kiasi cha Sh milioni 2.7 kwa ajili ya ujenzi.
Aidha, Yanga ilikuwa ina mfadhili wake, aliyekuwa akiwasaidia fedha nyingi, Shiraz Sharrif, ingawa naye baada ya mgogoro alihamia Pan African, kwa sababu alikuwa ana imani na Mangara.
Kutokana na jinsi Mangara alivyoishi vizuri na wachezaji wa klabu hiyo, alikuwa akiwapenda akiwafanya marafiki, basi wachezaji wote waliamua kumfuata na kuachana na Yanga. Walifikia hatua hiyo, baada ya jitihada za kushinikiza Mangara arejeshwe, ikiwemo kuandamana, kushindikana. Kwa jeuri, Yanga nayo ilisema acha waende na itaunda timu mpya.
Hadi leo, ukiwauliza watu wa Yanga sababu za kugombana na mzee Mangara, wapo watakaosema wanachama walikuwa wakorofi na wengine watasema mzee huyo alikuwa akinufaika kwa kupitia mgongo wa Yanga.
Katika sakata hilo, wachezaji wakongwe waliokuwa Yanga ili wasikae bure msimu wa 1976, walikwenda Morogoro kujiunga na klabu iliyokuwa ikiitwa Nyota Afrika, wakafanikiwa kuipandisha daraja, wakati wachezaji chipukizi awali walikwenda kujiunga na timu ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), iliyokuwa ikiitwa Breweries wakati huo.
Lakini baadaye wachezaji waliokwenda Nyota walirejea Dar es Salaam kuungana na wadogo zao, kuanzisha timu iliyokuja kuwa tishio kwenye soka ya Tanzania, Pan African. Timu hiyo ilianzishwa chini ya Mangara, aliyekuwa Mwenyekiti wa kwanza klabu hiyo.
Mbali na Mangara, wengine walioasisi timu hiyo ni Omar Muhajji, Sammy Mdee, Shiraz Sharrif, aliyekuwa mfadhili wa Yanga ambaye alihamishia noti zake kwa klabu ya Mtaa wa Swahili.
Pan ilipata mashabiki wengi kwa sababu wengi waliokuwa wapenzi wa Yanga walihamia Pan. Walihamia kuwafuata wachezaji bora waliokuwa Yanga kuanzia wakongwe hadi chipukizi.
Ni katika kipindi hicho, Yanga iliyumba sana na kupoteza makali yake katoka soka ya Tanzania. Haikuwa ajabu ilipotandikwa mabao 6-0 na watani wao wa jadi, Simba Julai 19, mwaka 1977.
Wakati ikiwa katika harakati za kujiweka sawa, serikali ilitoa tamko la kuzuia makocha wa kigeni nchini, hivyo Tambwe Leya na aliyekuwa kocha wa Simba, Nabby Camara, raia wa Guinea aliyeifanya Simba icheze soka safi mno, waliondoka nchini.
Baada ya miaka, Tambwe alirejea nchini mwishoni mwa mwaka 1994, lakini wakati huo aliikuta Yanga ipo chini ya kocha Nzoyisaba Tauzany kutoka Burundi, ambaye alikuwa anafanya vizuri.
Wakati huo, Mwenyekiti wa Yanga Dk. Jabir Idrisa Katundu alimpokea vizuri Tambwe na wakajadiliana cha kufanya. Dk. Katundu akamuacha Tauzany aendelee na Yanga kubwa na Tambwe akapewa timu ya vijana, ambayo mwenyewe aliipa jina Black Star.
Alikusanya vijana wenye vipaji na kuanza kuwapika ‘kimya kimya’ akaenda nao kwenye kambi ya Zanzibar kuwajenga kwa mazoezi ya fiziki kabla ya kuanza kuonyesha makali yake kwenye michezo ya kirafiki ikizifunga timu za huko.
Black Star ya Tambwe ikaja kuwa timu ya kwanza ya Yanga mwaka mmoja tu baadaye ikiongezewa nguvu na wakongwe wachache waliokuwa chini ya Tauzany.
Hiyo ilifuatia Yanga kuvunja tena kikosi mwaka 1994, baada ya kuwatuhumu wachezaji wake nyota kuhujumu mechi dhidi ya Simba timu ikafungwa 4-1. Ilidaiwa wachezaji wa Yanga walihongwa na mfadhili mmoja wa klabu hiyo aliyekuwa hapatani na uongozi wa klabu hiyo ili wafungishe kuukomoa uongozi. 
Baadhi ya wachezaji waliobakizwa kikosini baada ya wengine nyota kama Said Mwamba ‘Kizota’, Salum Kabunda ‘Ninja’ (wote marehemu) kutupiwa virago ni Kenneth Mkapa, Constantine Kimanda, Sekilojo Chambua, Sanifu Lazaro ‘Tingisha’ na Mohammed Hussein ‘Mmachinga’, wengine wote walitimuliwa kwa tuhuma hizo.
Baada ya hapo, Yanga iliundwa na wachezaji waliokuwa wakiandaliwa na Tambwe Leya (sasa marehemu) katika kikosi cha pili, ambao ni pamoja na Godwin Mashoto (sasa marehemu), Mzee Abdallah, Anwar Awadh, Maalim Saleh ‘Romario’, Nonda Shaaban na wengineo, waliosajiliwa kutoka timu mbalimbali kuimarisha kikosi kama Bakari Malima, Reuben Mgaza waliotoka Pan African.
Haikuchukua muda kikosi cha yosso wa Yanga kikawa tishio hata kikaweza kufika Robo Fainali ya Kombe la Washindi barani Afrika, mwaka 1996 na kutolewa na Blackpool ya Zimbabwe. 
Yosso hao wangeweza kufanya maajabu zaidi, kama si viongozi wakati huo kuendekeza imani za kishirikina na kuacha kuwapa maandalizi bora vijana, kwani wakihitaji ushindi wa 1-0 ili waingie Nusu Fainali kwenye mechi ya nyumbani baada ya kufungwa 2-1 ugenini, walijikuta wakifungwa tena 2-1 nyumbani.
Mchezaji mmoja wa Yanga alifichua siri kwamba, wachezaji walibughudhiwa usiku kucha kwa mambo ya kishirikina na hawakulala vizuri, matokeo yake wakaamka wamechoka na kufungwa nyumbani.
Awali, Yanga ilianza vyema kwa kuitoa Vaal Reef Professionals ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-3, ikianza kulazimisha sare ya 2-2 ugenini, kabla ya kushinda 2-1 nyumbani.
Katika raundi ya pili, Yanga ilikutana na Tamil Cadets Club ya Mauritius na kuitoa kwa jumla ya mabao 4-2, ikishinda ugenini  3-1 na kutoa sare ya 1-1 nyumbani, hivyo kukata tiketi ya Robo Fainali.
Kwa nini nimemkumbuka Tambwe Leya? Wiki hii Yanga ilitambulisha wakuu wake wapya wa benchi la Ufundi, aliyekuwa kocha Mkuu Mholanzi, Hans van der Pluijm akihamia kwenye Ukurugenzi wa Ufundi na nafasi yake akimuacha Mzambia, George Lwandamina.
Maofisa wengine katika benchi la Ufundi la Yanga wanabaki katika nafasi zao kama kabla ya mabadiliko haya.
Baada tu ya tetesi za Pluijm kuhamishiwa kwenye Ukurugenzi, binafsi nilimuuliza kama atakuwa tayari kwa majukumu mapya, na majibu yake yalikuwa; “Sipendelei hiyo kazi. Nataka kufanya kazi na wachezaji kila siku kwa matakwa ya moyo wangu,”alisema.
Na Pluijm kwa hiari yake alitaka kuondoka Yanga, ila baada ya kubembelezwa na klabu na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba shabiki wa klabu hiyo, amekubali kubaki katika majukumu mapya.
Lakini kimsingi Pluijm hajakubali Ukurugenzi wa Ufundi kwa utashi wake, bali shinikizo la klabu. Najiuliza kwa nini Yanga isimpe Pluijm kitu anachopenda, ambacho ni kufundisha wachezaji?
Naona ni wakati mwafaka sasa Yanga kuwa na programu rasmi ya vijana kwa kumpa majukumu ya timu ya vijana Pluijm na anaweza akawasaidia kuwazalishia vipaji vizuri na kuwaepushia matumizi ya fedha nyingi za kusajili kila dirisha linapowadia.
Yanga ikimtumia vizuri Pluijm itatamani kuendelea kuwa naye milele, lakini kwa kumlazimisha nafasi ya Ukurugenzi sitarajii kama atakuwa na maisha marefu Jangwani.


from BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE http://ift.tt/2fApcsL best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm, lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today, mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma, mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer, mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney, mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390, mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms
Tweet

Terimakasih anda telah membaca artikel tentang YANGA IKIMTUMIA KWA FAIDA PLUIJM ITATAMANI KUWA NAYE DAIMA MILELE. Jika ingin menduplikasi artikel ini diharapkan anda untuk mencantumkan link https://viralsport.blogspot.com/2016/11/yanga-ikimtumia-kwa-faida-pluijm.html. Terimakasih atas perhatiannya.

Related Posts

di 20.21
Label: BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE

{ 0 komentar... read them below or add one }


Posting Komentar

Posting Lebih Baru Posting Lama Beranda

Popular Posts

  • SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    SIMBA SC INAVYOJIANDAA KUIKABILI POWER DYNAMOS NDOLA
    VIUNGO, Muivory Coast Aubin Kramo Kouamé (kushoto) na José Luis Miquissone wa Msumbiji wakiwa kwenye mazoezi ya Simba leo Uwanja wa Mo Si...
  • Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Lucky Numbers Promotion: Stand a Chance to Win a Share of R100 000
    Stand a chance to win your share of R100 000 cash! Play R5 or more using your Hollywoodbets account on the selected Lucky Numbers draws an...
  • Lucky Numbers Draw Times & Results
    Lucky Numbers Draw Times & Results
    All the information you need for the 501 Lotto draws offered by Hollywoodbets for Lucky Numbers and Powa Numbas betting! Get closing times...
  • MOHAMED SALAH ANAVYOFURAHIA MAISHA LIVERPOOL
    Kiungo Mohamed Salah akifurahia kwenye mazoezi ya Liverpool leo Uwanja wa  Melwood kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya England ...
  • PGA Tour: The Sony Open Preview
    We take a look at the Sony Open set to take place between 11 January and 14 January at the Waialae Country Club.  With news of Tiger Woods...
  • UK Racing Best Bets - Saturday 28 September 2019
    UK Racing Best Bets - Saturday 28 September 2019
    Neil Morrice walks you through the front runners for Saturday's feature races at Cambridgeshire, Newmarket and the Cheveley Park Stake...
  • TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JUMAMOSI HOTELI YA WHITE SANDS MAANDALIZI YA AFCON
    TAIFA STARS KUINGIA KAMBINI JUMAMOSI HOTELI YA WHITE SANDS MAANDALIZI YA AFCON
    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars itaingia kambini Juni 1 katika hoteli ya White Sands mjini ...
  • Daily Predictor Game: Stand A Chance To Win Your Share of R10 000 In Cash And Betting Vouchers
    Daily Predictor Game: Stand A Chance To Win Your Share of R10 000 In Cash And Betting Vouchers
    Stand a chance to win your share of R10 000 in cash and betting vouchers by playing our new Daily Predictor Game. R200 betting vouchers da...
  • Erwee now very earnestly knocking on the Proteas door
    Erwee now very earnestly knocking on the Proteas door
    It may be very early days in the South African domestic season but Hollywoodbets Dolphins opener Sarel Erwee has put his hand up with the f...
  • YANGA SC 6-1 KENGOLD (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)
    YANGA SC 6-1 KENGOLD (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)
      from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/Rr0NtG3
Copyright Viral Sports: YANGA IKIMTUMIA KWA FAIDA PLUIJM ITATAMANI KUWA NAYE DAIMA MILELE