Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MCHEZO wa Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya wenyeji, Abajalo FC na Tanzania Prisons umeshindwa kuanza hadi sasa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Timu zote mbili zimefika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kukaguliwa tayari kuanza, mchezo lakini wachezaji saba wa Abajalo wakazuiwa kucheza kwa sababu hawakuwa na leseni za TFF
Mwenyekiti wa Abajalo, Edgar Chibura alisema kwamba wachezaji waliozuiwa wote ni halali na ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo.
Chibura amesema ilishindikana kupata leseni kwa ajili ya wachezaji hao kwa sababu mfumo wa usajili wa njia ya mtandao wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), maarufu kama TMS ulikorofisha.
“Na tangu jana sisi tulikuwa ofisi za TFF ili tuidhinishiwe wachezaji wetu na kupewa leseni, lakini TFF wamekuwa wakituzungusha tu hadi kufika hapa,”alisema.
Inafahamika Desemba 15, mwaka huu mfumo wa usajili kwa njia ya TMS ulifeli hali iliyosababisha klabu kushindwa kukamilisha usajili kwa wakati kupitia mfumo huo.
TFF iliagiza klabu ziwasilishe moja kwa moja usajili wake makao makuu ya shirikisho, Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Lakini jana TFF ikasema kwamba TMS imefunguliwa tena baada ya marekebisho ya hitilafu zilizojitokeza kufuatia shirikisho hilo kuwasiliana na waendeshaji wa mfumo huo walioko Tunis, Tunisia na klabu zitaendelea kusajili hadi Desemba 23 dirisha litakapofungwa tena.
Kikosi cha Abajalo kichotarajiwa kuanza leo kilikuwa; Aaron Kalambo, Sharifu Mkangala, Laurian Mpalile, Jumanne Elfadhil, Nurdin Chona, Dotto Ramadhani, Adam Chimbongwe, Julius Kwanga, Salum Bosco, Mohammed Rashid na Eliuter Mpepo.
Prisons; Athumani Nyamaka, Bakari Mahadhi, Lawrence Mugia, Waziri Jitukali, Ally Abdallah, Majjid Shaaban, Kelvin Julius, Mohammed Maruzuku, Amir Ally, Ally Athumani na Hilal Bingwa.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2Bathze
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms