Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
AZAM FC imeshindwa kutumia vyema Uwanja wa nyumbani baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 15, ingawa inaendelea kukaa nafasi ya tatu, nyuma ya Azam FC yenye pointi 30 na Simba SC pointi 32.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Israel Mujuni Nkongo aliyeyesaidiwa na washika vibendera Josephat Bulali na Soud Lila, hadi mapumziko tayari Yanga walikuwa wamekwishatengeneza ushindi wao huo.
Lakini ilibidi Yanga watoke nyuma baada ya mshambuliaji chipukizi, Shaaban Iddi Chilunda kutangulia kuifungia Azam FC bao la kuongoza dakika ya nne tu akimalizia krosi ya Mzimbabwe, Bruce Kangwa aliyemtoka beki Hassan Kessy pembeni na kuingia ndani.
Mzambia Obrey Chirwa akaisawazishia Yanga dakika ya 30 baada ya kupokea pasi ya kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajib na kumpiga chenga kipa wa Azam, Mghana Razack Abalora aliyetoka bila maarifa ya ziada.
Katika mastaajabu ya wengi, kocha wa Azam FC, Mromania Aristica Cioaba alimtoa mshambuliaji Mghana, Bernard Arthur aliyekuwa anacheza vizuri na kuwatia misukosuko mabeki wa Yanga, akamuingiza kiungo Salmin Hoza.
Haikuwa ajabu Yanga walipouteka mchezo kwa kasi na mashambulizi mfululizo hadi wakafanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na beki Gardiel Michael Mbaga aliye katika msimu wake wa kwanza Jangwani tangu asajiliwe kutoka Azam aliyefunga kwa shuti la umbali wa mita 30 baada ya pasi ya Mkongo, Papy Kabamba Tshishimbi.
Ushangiliaji wa Gardiel kana kwamba alijua ndio bao la ushindi, lakini ulitosha kupeleka ujumbe kwa viongozi wa Azam FC kwamba walikosea kumuacha.
Kipindi cha pili mchezo ulinoga zaidi, Azam FC wakisaka bao la kusawazisha na Yanga ambayo leo iliongozwa na kocha wake, Mzambia George Lwandamina ikitafuta bao la pili.
Cioaba akasahihisha makosa yake baada ua kurudisha mshambuliaji uwanjani na kutoa kiungo, akimuingiza Mbaraka Yussuf kwenda kuchukua nafasi ya Stephan Kingue Mpondo.
Azam FC ilipata pigo dakika ya 79 baada ya kiungo wake, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu beki wa Yanga, Hassan Kessy. Sure boy alionyeshwa kadi ya kwanza ya njano dakika ya 22 alipomchezea Emmanuel Martin.
Kutoka hapo, Yanga wakauteka kabisa mchezo, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi tu.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Mwadui FC imelazimishwa sare ya 2-2 na Njombe Mji FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mbeya City imelazimishwa sarte ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Kagera Sugar imetoka 0-0 na Lipuli FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Kikosi cha AzamFC; Razack Abalora, Himid Mao, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephane Kingue/Mbaraka Yussuf dk55, Joseph Mahundi, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Bernard Arthur/Salmin Hoza dk36, Shaaban Iddi/Paul Peter dk62 na Atta- Agyei.
Yanga SC; Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Andrew Vincent, Kevin Yondan, Said Juma ‘Makapu’, Raphael Daudi, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib/Juma Mahadhi dk68 na Emmanuel Martin/Geoffrey Mwashiuya dk62.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE http://ift.tt/2Egc8qe
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms