Na Mwandishi Wetu, ANDERLECHT
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza kwa dakika zote 90 leo timu yake, KRC Genk ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Anderlecht katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Katika mchezo huo wa mchujo wa kuwania ya kucheza michuano ya Ulaya mwakani uliofanyika Uwanja wa Constant Vanden Stock mjini Brusells, Ubelgiji mabao ya Genk yalifungwa na Wabelgiji, beki Dries Wouters dakika ya 35 na mshambuliaji Leandro Trossard dakika ya 37.
Bao la kufutia machozi la wenyeji, Anderlecht lilifungwa na mshambuliaji kutoka Poland, Lukasz Teodorczyk dakika ya 53 na kwa matokeo hayo, Genk ianamaliza nafasi ya tano kwenye msimamo na Jumapili ijayo watamenyana na ama Lokeren au Zulte Waregem kuwania tiketi ya mwisho ya Ulaya.
Mbwana Samatta (katikati) akishangilia na wenzake ushindi wa 2-1 dhidi ya Anderlecht leo
Samatta leo amecheza mechi yake ya 89 tangu Nahodha huyo wa Taifa Stars ajiunge na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kati ya hizo akiwa amefunga mabao 25.
Kikosi cha Anderlecht kilikuwa; M. Sels, O. Deschacht, A. Najar/ F. Amuzu dk46, U. Spajic, S. Kums, R. Morioka/ A. Lokonga dk84, K. Mbodji, A. Trebel, P. Gerkens, A. Saelemaekers na L. Teodorczyk.
KRC Genk; D. Vukovic, B. Nastic, O. Colley, D. Wouters/ S. Berge dk64, J. Aidoo, Pozuelo/ S. Schrijvers dk79, I. Seck, Clinton Mata, L. Trossard, M. Samatta na D. N'Dongala/ T. Buffel dk85.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2IX4E0m
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms