Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba leo imezawadiwa kitita cha Sh. Milioni na wadhamini wao, kampuni ya SportPesa Tanzania kufuatia kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
SportPesa Tanzania, ambao pia ni wadhamini wa mahasimu wa Simba, Yanga imetekeleza kipengele cha mkataba wao kinachosema timu itakayotwaa ubingwa wa Ligi Kuu itapewa kiasi hicho cha fedha.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla ya kukabidhi fedha hizo iliyofanyika kwenye ofisi za Sports Pesa Tanzania, Oysterbay, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa kampuni hiyo, Tarimba Abbas aliwapongeza viongozi na wachezaji wa Simba kwa kaz nzuri.
Tarimba, Rais wa zamani wa Yanga alisema kwamba ubingwa huo umewapa heshima kubwa wana Msimbazi na kubwa zaidi ni heshima waliyowapa wao kama wadhamini wao wakuu.
“Awali ya yote niwapongeze viongozi na wachezaji kwa ujumla kwa kupambana hadi kuweza kuchukua ubingwa wa Ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 na sisi kama wadhamini wenu wakuu tunatekeleza ile ahadi tuliyoiweka kuwa Timu inayodhamiwa na Kampuni yetu itapewa Shilingi Milioni 100 na leo tumelitimiza hilo,”.
“Simba imeitendea haki nembo yetu ya SportsPesa na Kampuni inaamini kuwa kwa SportsPesa kuwa wadhamini wakuu imekuwa nimoja ya chachu iliyosababisha Simba SC kuchukua ubingwa msimu huu" amesema Tarimba
Wakati huo huo; Tarimba amewataka Viongozi kupeleke kikosi kamili kwenye michuano ya SportsPesa Super Cup inayotarajia kuanza Juni 3 hadi 10 nchini Kenya, ili kuweza kufanya vizuri katika michuano hiyo kuwa Mabingwa na kurudi nyumbani na kitita cha dola za Kimarekani 30,000 pamoja na kupata nafasi ya kwenda nchini Uingereza kucheza na Everton FC ya Ligi Kuu ya England Uwanja wa Goodison Park.
Kwa upande wake Kaimu Makamu wa Rais wa Simba SC, Iddi Kajuna ameishukuru Kampuni ya SportsPesa kwa kuleta mabadiliko kwenye soka nchini ambayo wao kama klabu wameyaona kwa upande wao.
“Moja ya mambo ambayo Simba inajivunia msimu huu ni kuwa na mdhamini kama SportsPesa, ambaye mbali na udhamini, pia tumekuwa tukishirikiana naye katika shughuli mbalimbali za kiuongozi, tulifanya maandalizi mazuri msimu huu kuanzia kwenye ngazi ya uongozi hadi benchi la ufundi na ndio maana siyo jambo la ajabu Simba kuchukua Ubingwa, kwani tulishaandaa mikakati ya kushinda kwa kushirikiana na wadhamini wetu" amesema Kajuna
Simba SC ni miongoni mwa timu nne kutoka Tanzania zitakazoshiriki michuano ya SportsPesa Super Cup itakayofanyika nchini Kenya kuanzia Juni 3 hadi 10 ikishirikisha time nane kutoka nchini Tanzania na Kenya.
Timu nyingine ni pamoja na Yanga, Singida United na JKU ya Zanzibar, Gor Mahia, AFC Leopards, Kakamega Home Boys na Kariabangi Sharks za Kenya. Gor Mahia ndiye bingwa mtetezi wa michuano hiyo baada ya kuwafunga watani wao wao jadi, AFC Leopard katika fainali mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2kl6dHn
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms