Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WAKATI kikosi cha Azam FC kikiwa kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo ujao dhidi ya Yanga, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Idd Nassor Cheche, amesema kuwa amepanga kuonyesha mchezo mzuri na kulipa kisasi cha kufungwa ule wa kwanza.
Mchezo huo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) unatarajia kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatatu hii saa 2.00 usiku.
Cheche amesema kwambawanaiheshimu Yanga akiamini kuwa mchezo utakuwa mgumu na mzuri huku akiwaomba mashabiki wa soka wajitokeze kushuhudia burudani.
Gardiel Michael wa Yanga (kulia) na winga Mghana, Ennock Atta-Agyei wa Azam FC katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu baina ya timu hizo
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa Azam Complex, Azam FC iliteleza na kufungwa mabao 2-1, bao la Azam FC likifungwa na mshambuliaji Shaaban Idd huku yale ya Yanga yakitupiwa na Gardiel Michael na Obrey Chirwa.
“Mechi ya kwanza imeshapita, japokuwa inamajeraha kwetu lakini tuna mechi ya marudiano hii nafikiri tunaenda kulipiza lile deni ambalo tuliokuwa nalo, kwa sababu walituachia deni hatuna budi kulilipa kuhakikisha tunalipa mabao waliyotufunga ikiwezekana kuongeza zaidi ya yale,” alisema.
Azam FC imetoka kushinda mechi mbili mfululizo, ikiichapa Majimaji (2-0) na Tanzania Prisons (4-1), akizungumzia siri ya mafanikio hayo, alisema imetokana na ushirikiano na umoja ulioko kwenye timu hiyo.
“Ni umoja tu katika kazi kwenye kazi mkiwa wamoja mnashirikiana, mnafanya kazi pamoja, mnapendana nafikiri matokeo yanapatikana, ushirikiano na umoja ndio unatusaidia katika haya yote,” alisema.
Hadi kuelekea mchezo huo wa mwisho wa ligi, timu hizo ziko kwenye vita kali ya kuwania nafasi ya pili, Azam FC ikiwa inaishikilia kwa pointi zake 55 ikiizidi pointi nne Yanga yenye mechi mbili mkononi.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2KUQeLn
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms