Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
BAO pekee la mshambuliaji mpya, Mohammed Rashid limeipeleka Simba SC fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya AS Ports ya Djibouti Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Rashid aliyesajiliwa kutoka Tanzania Prisons mwezi uliopita alifunga bao hilo dakika ya 65 kwa shuti ka kiutaalamu akimchambua kipa hodari wa Ports, Lumiya Sulait baada ya pasi ya beki Mghana, Nicholas Gyan aliyepanda kusaidia mashambulizi.
Na Rashid alifunga bao hilo dakika sita tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake mpya Simba SC, Adam Salamba aliyesajiliwa mwezi uliopita pia kutoka Lipuli FC ya Iringa.
Mohammed Rashid (kulia) akikimbia kushangilia na Meddie Kagere baada ya kufunga bao pekee leo
Meddie Kagere (kulia) akiwatoka wachezaji wa AS Ports leo Uwanja wa Taifa
Ports watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi nzuri za kufunga kipindi cha kwanza, ikiwemo ile ya dakika ya 44 ambayo mshambuliaji Doualeh Mohamoud Elabeh alipiga nje akiwa amebaki yeye na kipa Deogratius Munishi ‘Dida’.
Kwa matokeo hayo sasa, Simba itakut ana na Gor Mahia katika Nusu Fainali Jumatano Uwanja wa Taifa tena, baada ya timu hiyo ya Kenya kuitoa Vipers ya Uganda kwa kuichapa mabao 2-1 katika mchezo uliotangulia jioni ya leo.
Mchezo huo utakuwa ni marudio ya fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup Juni 10, mwaka 2018 Gor Mahia ikiichapa Simba 2-0, mabao ya Meddie Kagere dakika ya sita na Jacques Tuyisenge dakika ya 55 Uwanja wa Afraha mjini Nakuru.
Na baada ya mashindano hayo, Simba SC ikamchukua mshambuliaji Meddie Kagere ambaye Jumatano atacheza dhidi ya timu yake ya zamani.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Deogratius Munishi ‘Dida’, Nicholas Gyan, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Paul Bukaba, Pascal Wawa, James Kotei, Said Ndemla/Muzamil Yassin dk43, Mwinyi Kazimoto, Meddie Kagere, Adam Salamba/Mohammed Rashid dk59 na Mercel Kaheza/Rashid Juma dk68.
AS Ports: Lumiya Sulait, Mohammed Bourhan, Franck Ndayisenga, Ibrahim Aden Warsama, Mohammed Abdourahman/Mohamed Salem dk80, Wais Daoud Wais, Hamza Abdi Idleh, Moussa Helem Mohamed, Bangnie Guessebo Junior/Abdoulrazak Mahamoud dk78, Doualeh Mohamoud Elabeh na Mahdi Houssein Mahabeth.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2MXRRJf
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms