Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA), limeipa Simba SC kibali cha muda cha kumtumia kiungo Mzambia, Cletus Chama kufuatia klabu yake, Dynamos ya Lusaka kugoma kufanya hivyo.
Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Simba SC zimesema kwamba FIFA imewaandikia TFF, Shirikisho la Soka Tanzania wairuhusu klabu hiyo kumtumia Chama hadi hapo hapo suala lake litakapopatiwa suluhu na kupatiwa Hati rasmi ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC).
Pamoja na kukamilisha taratibu zote za usajili wake Simba SC, akisaini mkataba wa miaka miwili, lakini Dynamos imegoma kumpa Chama ITC ikidai inamdai fedha kulingana na makubaliano yao nje ya mkataba.
FIFA imeipa Simba SC kibali cha muda cha kumtumia kiungo Mzambia, Cletus Chama (kushoto)
Na baada ya FIFA kupelekewa kesi hiyo, imeiagiza TFF imruhusu Chama kuendelea kucheza Simba SC kulinda kipaji chake, huku ikiitaka Dynamos kuwasilisha kesi juu ya malalamiko.
Katika hatua nyingine, Simba SC imefanikiwa kupata ITC ya kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ aliyekuwa anachezea timu ya Chuo Kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini.
Na baada ya kufanikiwa kutatua matatizo ya kiusajili ya wachezaji wake hao wawili, Simba SC imeiandikia barua TFF na Bodi ya Ligi ikiomba iruhusiwe mechi yake ya Septemba 1, mwaka huu dhidi ya Lipuli FC ya Iringa Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Hiyo ni baada ya Bodi kuahirisha mechi tatu, nyingine zikiwa ni kati ya Azam FC na Ruvu Shooting ya Pwani Septemba 1, Uwanja wa Azam Complex na Septemba 2 kati ya Mwadui FC na Yanga SC Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Mechi hizo zimeahirishwa kwa sababu ya wachezaji wengi wa Azam, Simba na Yanga kuchaguliwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa Kundi L kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Uganda ‘The Cranes’ mjini Kampala Septemba 8, mwaka huu.
Simba SC inaamini kwa kikosi chake kipana haitaathirika kucheza bila kipa wake namba moja, Aishi Manula, mabeki Shomari Kapombe na Erasto Nyoni, viungo Jonas Mkude, Shiza Kichuya na Hassan Dilunga na mshambuliaji na Nahodha, John Bocco.
Wachezaji wa Yanga SC waliopo kwenye kikosi cha kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike ni Benno Kakolanya, mabeki Gardiel Michael, Kelvin Yondan na Andrew Vincent ‘Dante’ na kiungo Feisal Salum wakati wa Azam FC ni beki ni Aggrey Morris na mshambuliaji Yahya Zayed.
Amunike aliyeng’ara na Super Eagles katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani akicheza wingi ya kushoto, mtihani wake wa kwanza utakuwa ni mchezo dhidi ya Uganda Septemba 8, mwaka huu mjini Kampala, kabla ya kuwafuata Cape Verde Oktoba 10 kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Na hiyo ni baada ya Taifa Stars kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Lesotho Juni 10, mwaka jana Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ikiwa chini ya kocha mzalendo, Salum Mayanga.
from BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE https://ift.tt/2wla8KN
best mesothelioma law firms, mesothelioma attorneys, mesothelioma
lawyer, mesothelioma lawsuits, mesothelioma lawyers, mesothelioma
lawsuit, mesothelioma attorney, mesothelioma settlement, mesothelioma
lawsuit settlements, mesothelioma settlements, mesothelioma law firm,
lawyer mesothelioma, get a online mesothelioma law firm today,
mesothelioma claims, mesothelioma claim, malignant mesothelioma,
mesothelioma law, mesothelioma law firm california, mesothelioma
compensation, mesothelioma law firms, asbestos settlement, asbestos
claim, mesothelioma, asbestos lawsuit, asbestos lung cancer,
mesothelioma law suit, asbestos claims720, asbestos attorney,
mesothelioma lung cancer, mesothelioma causes, asbestos lawyer390,
mesothelioma cancer, asbestos lawsuits, asbestos lawyers, causes of
mesothelioma, asbestos cancer, mesothelioma law suits, what is
mesothelioma, law offices, mesothelioma symptoms